Aliyemtumia Rais Samia taarifa za wizi wa Mahindi ya NFRA atafutwa na Polisi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Jeshi la polisi wilayani Handeni mkoani Tanga linamsaka aliyetuma ujumbe kwa Rais Samia wa kuibiwa mahindi ya msaada ya NFRA kwa kutumia jina la Mwenyekiti wa kijiji.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe leo Desemba 30,2022 alipokuwa kwenye kikao na wananchi wa kijiji cha Kwedizinga, kuhusu tuhuma ya kuibiwa mahindi hayo ambapo amesema ujumbe huo umebainika sio wa Mwenyekiti.

Amesema aliyetuma ujumbe huo kwa mujibu wa sheria ya mtandao anatafutwa, kwani ametoa tuhuma kwa viongozi kwa majina na namba zao wakati wenyewe hawafahamu lolote.

Mkuu wa wilaya ameongeza kuwa kupitia jeshi la polisi tayari mtu huyo ameanza kutafutwa, kwani mwenyekiti aliyetajwa humo amekanusha kuhusika na tukio hilo.

"Sisi kama serikali kupitia kamati ya ulinzi na usalama tayari kupitia sheria ya mtandao tunamtafuta mwenye ule waraka, ni nani na atakapokamatwa sheria itachukua mkondo wake amewachafua viongozi wa serikali", amesema Mchembe.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kwedizinga Waziri Bakari Maleka amesema yeye hahusiki na ujumbe uliosambaa mtandaoni kwenda kwa Rais Samia bali aliyeandika ametumia jina na namba yake ya simu.

"Ujumbe huo ambao umesambaa kumueleza mama Samia mtandaoni mimi sina na siutambui, mwisho wamenitaja mimi hii ni kunichafua na kunipa taarifa ambayo sihusiki nayo", amesema Waziri.

Afisa wa NFRA Valeria Mwenda amesema, aliyesambaza ujumbe huo amesambaza baada ya kuona yapo magari makubwa yanabeba mahindi hayo bila kujua mzigo uliopo ni kwaajili ya kata zaidi ya tatu.

Mkuu wa kituo cha Polisi, Kabuku Elias Luambano amesema tayari wameshaanza ufuatiliaji kujua chanzo cha ujumbe huo kuwa umeandikwa na nani kwani amesababisha taharuki kwenye zoezi hilo.

Hivi karibuni ulionekana ujumbe mtandaoni ukimuomba Rais Samia msaada kutokana na uwepo wa wizi wa mahindi ya msaada kata ya Kwedizinga Handeni na sehemu ya ujumbe huo ilisomeka hivi;

"Tunakuomba Rais Samia Suluhu Hassan sisi wananchi wa Kwedizinga Handeni, Tanga tunahujumiwa mahindi ya msaada uliyoleta tuuziwe Sh800 kwa kilo sasa wanauziwa wafanyabiashara matajiri wanakuja kusomba na magari kwenda kuuza mijini," imesema sehemu ya ujumbe huo.

MWANANCHI
 
Stan K.(Mwenyezi Mungu akulinde na kukupa mapumziko mema),maana wewe pekee ndio ulikua whistblower shujaa nchi hii kushuhudia, ulitumia pen yako kishujaa, bila woga na alimkamata Bull kwenye pembe zake, ulitutoka kwenye mazingira tatanishi ila kuna watanzania hadi leo tunakukumbuka,Chairman anakanusha wakati simu/namba iliyotumika ni ya kwake!!!(kama hili Lina ukweli basi ni very strange),uoga wa kizuzu imeshamwingia na hawezi kutetea analoliamini. Tanzania 🇹🇿 ubabaishaji ukome wenzetu 🇿🇲 wanakimbiza maendeleo
 
Jeshi la polisi wilayani Handeni mkoani Tanga linamsaka aliyetuma ujumbe kwa Rais Samia wa kuibiwa mahindi ya msaada ya NFRA kwa kutumia jina la Mwenyekiti wa kijiji.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe leo Desemba 30,2022 alipokuwa kwenye kikao na wananchi wa kijiji cha Kwedizinga, kuhusu tuhuma ya kuibiwa mahindi hayo ambapo amesema ujumbe huo umebainika sio wa Mwenyekiti.

Amesema aliyetuma ujumbe huo kwa mujibu wa sheria ya mtandao anatafutwa, kwani ametoa tuhuma kwa viongozi kwa majina na namba zao wakati wenyewe hawafahamu lolote.

Mkuu wa wilaya ameongeza kuwa kupitia jeshi la polisi tayari mtu huyo ameanza kutafutwa, kwani mwenyekiti aliyetajwa humo amekanusha kuhusika na tukio hilo.

"Sisi kama serikali kupitia kamati ya ulinzi na usalama tayari kupitia sheria ya mtandao tunamtafuta mwenye ule waraka, ni nani na atakapokamatwa sheria itachukua mkondo wake amewachafua viongozi wa serikali", amesema Mchembe.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kwedizinga Waziri Bakari Maleka amesema yeye hahusiki na ujumbe uliosambaa mtandaoni kwenda kwa Rais Samia bali aliyeandika ametumia jina na namba yake ya simu.

"Ujumbe huo ambao umesambaa kumueleza mama Samia mtandaoni mimi sina na siutambui, mwisho wamenitaja mimi hii ni kunichafua na kunipa taarifa ambayo sihusiki nayo", amesema Waziri.

Afisa wa NFRA Valeria Mwenda amesema, aliyesambaza ujumbe huo amesambaza baada ya kuona yapo magari makubwa yanabeba mahindi hayo bila kujua mzigo uliopo ni kwaajili ya kata zaidi ya tatu.

Mkuu wa kituo cha Polisi, Kabuku Elias Luambano amesema tayari wameshaanza ufuatiliaji kujua chanzo cha ujumbe huo kuwa umeandikwa na nani kwani amesababisha taharuki kwenye zoezi hilo.

Hivi karibuni ulionekana ujumbe mtandaoni ukimuomba Rais Samia msaada kutokana na uwepo wa wizi wa mahindi ya msaada kata ya Kwedizinga Handeni na sehemu ya ujumbe huo ilisomeka hivi;

"Tunakuomba Rais Samia Suluhu Hassan sisi wananchi wa Kwedizinga Handeni, Tanga tunahujumiwa mahindi ya msaada uliyoleta tuuziwe Sh800 kwa kilo sasa wanauziwa wafanyabiashara matajiri wanakuja kusomba na magari kwenda kuuza mijini," imesema sehemu ya ujumbe huo.

MWANANCHI
Caught with pants down!mijizi imekutwa inaiba sasa ina haha
 
Waache sanaa.

Hiyo tuhuma ni kweli au la??
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089]
 
Maelezo yako yooooote hujasema kama ni kweli alichosema mtuma messeji kama mahilindi yanaibiwa?. Kimsingi hapo kuna kesi mbili

1. Aliyetuma ujumbe kwa kutumia jina/cheo cha mtu mwingine ni makosa
2. Taarifa yake kuwa mahindi yanaibiwa; kama ni kweli yanaibiwa amefanya kazi ya Whistle blower hivyo ni vizuri ili ifanyiwe kazi ILA kama amedanganya, anapata kosa la pili
 
na kwa Tanzania hii unadhani mtuma ujumbe anadanganya?
sipendi viongozi wakurupukaji,badala ya uchunguzi ufanyike lenyewe eti linamtafuta mtu aliyetuma habari
 
Kwanini atafutwe si uchunguzi ufanyike tu kama tuhuna sio za kweli yaishe
Hili jambo ni dogo sana na viongozi wa CCM hupenda kufuatilia mambo madogo kwani hawana kazi ya kufanya. Ilitakiwa uchunguzi mfupi sana ufanyike kama kweli kuna wizi, na kama hakuna kila mtu aendelee na shughuli zake.
 
7e86a91892aeb949fee35acf240c01f6.jpg
 
Back
Top Bottom