Aliyemuelewa Mo Dewji kuhusu uwekezaji Simba atujuze

Yule boss wa FCC aliyekuwa anatia ngumu wamemtoa na kumuweka mtu ambaye atafanya mambo yaende, ametolewa na yule mzee anayemiliki timu huko mikoroshoni iliyobebwa mwaka jana, timu ambayo anachezea yule mchomekea bukta anayekera
 
Wajinga ndo waliwao...
Nadhani tutumie neno KUPANGA NI KUCHAGUA.
Kinachoweza kuwa sumu kwako, ni chakula kwa mwingine.

Hakuna haja ya kushikana mashati kwa sababu tumeamua kufanya machaguo tofauti.

Kimfaacho mtu, ndicho chake.
 
Hata iweje lazima awauze miquson konde boy na chama avute mkwanja mrefu. Chezea mo wewe.
Akina sisi tusioingia kwenye vikao vya management ya Simba tunapaswa kupata taarifa za club yetu kupitia press conferences kama hizi, website ya club, Instagram na Facebook ya club, Simba tv. Yale yote anayoyasema pale hayapo pahala popote kwenye official media za Simba. Hata kusaini huo mchakato wa kukamilisha mabadiliko ya club na uwekezaji angalau tungeona picha za viongozi wetu wakisaini kwenye website au Instagram. Lakini website, Instagram hazina taarifa ya uendeshaji ya aina yoyote.
 
Mkuu,kila mtu anakufa.

Hoja yangu ilitokana na comment iliyosema "hata akitoa jero,waanasimba wanataka furaha"

Yaan akiondoka ataacha nini kwa kutoa jero?
Nadhani jamaa kasema hivyo akimaanisha kwamba, wanaosema hiyo hela (20B) ni ndogo basi wafahamu kwamba kwanza hiyo ni "concern" yao wanasimba wenyewe, hivyo ingeweze kuwa ndogo zaidi ya hapo (mfano wake ndio hiyo jero).

Pili, kwa shabiki wa mpira, yeye furaha yake kubwa inaletwa na mpira mzuri uwanjani, mataji na utulivu wa timu (wachezaji kulipwa kwa wakati, n.k) hivyo hilo suala la price tag sio jambo la msingi sana (kwa shabiki yeyote yule, sio wa Simba peke yake).

Lakini pia, kama Simba wameenda ALL WAY WRONG, kuna mambo mawili:

1. Wao wenyewe ndio watakaolipa gharama za kukosea huko.

2. Hili litakua ni fundisho kwa vilabu vingine visifanye makosa kama inayodaiwa kuyafanya Simba. (Kwa muktadha huu Yanga wao wameamua kutofanya "hayo makosa yanayodaiwa kufanywa na Simba").

Na kama kutakua na chochote kibaya huko mbeleni, bado naona upo mwanya wa kurekebisha.
Hata kama wataamua "wao wenyewe" waachane na mambo ya uwekezaji na uendeshaji wa kisasa, watabidili mfumo na kujiendesha kama ilivyokua miaka ya 1970 (kama wataona inafaa).

Sioni kama ni jambo la busara kuwasakama katika hili.

Hivi mkuu, wewe hapo ukiamua kuuza nyumba yako, kwa hiyari yako, ukiwa na akili timamu, kwa shilingi elfu 30, kutakua na shida gani ?
 
Suala la udhamini wa jezi lipo kwenye official Instagram page ya Simba, uwe unafuatilia mkuu.


Miquessone na Chama aliwaleta mwenyewe, akiwauza mwenyewe sawa tu.
Ni sawa na GSM akiwauza Mukoko na Kisinda.

Sioni tatizo hapo.
 
Kinachonishangaza

Hivi ukiwa muwekezaji binafsi ndio na kampuni zako zingine zinapata upenyo wa kujitangaza humo humo .

Jezi za Simba zimejaa kampuni za mo,je amelipia hizo au ndio kwenye hizo hizo hela anazotoa bili20

Je ikija kampuni ingine ikitaka kununua haki za kujitangaza kwenge jezi je mo atakubali .

Kufanya biashara na muhindi tegemea magumashi kila Kona?
 
Umekaza sana kichwa, nice moves, kwaiyo wewe huwezi ku access vyanzo vya habari vya FCC hadi ushiriki vikao vya Simba mkuu ?
Tume ya Ushindani (FCC) imeanza uchunguzi wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Simba ambao inawahusu wadaawa watano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na FCC, wadaawa hao ni Simba Sports Club Holding Company Limited ambaye ni mdaawa wa kwanza, Mo Simba Company Limited (Mdaawa wa pili), Simba Sports Club Company Limited, Simba Sports Club na Mohammed Gulamabbas Hassanali Dewji.

Taarifa ya FCC imesema kuwa mdaawa wa tatu kwa kushirikiana na mdaawa wa kwanza, pili na tano walichukua mali na biashara za mdaawa wanne Tanzania Bara bila kuitaarifa tume hiyo kinyume na sheria ya ushindani kifungu cha 11 (2), 11 (6) (cha mwaka 2018) na kizingiti cha muunganiko wa makampuni cha mwaka 2017.

"Januari 6 mwaka huu, FCC ilifanya maamuzi kwa kutoa matokeo ya awali kuhusiana na tuhuma zinazowakabili wadaawa wote watano.

"Kitendo cha wadaawa wote watano kushindwa kuitaarifu FCC juu ya muunganiko huo wa makampuni kilisababisha kuinyima tume hiyo nafasi ya kutekeleza jukumu lake la kisheria la kufanya tathmini juu ya uhalali wa muunganiko huo unaotuhumiwa kutotaarifiwa kwake kwa mujibu wa sheria," imesema taarifa hiyo.
 
Sportpesa nayo ni ya Mo. Roho mbaya haijengi mkuu. Mbona Jersey za Ndala zimejaa matangazo ya GSM na hamna anayehoji!
Kwani hukuona ama kusikia Melt Group wakiingia mkataba wa udhamini na club ya Simba?
Watani zetu acheni roho mbaya haijengi. Tumieni makosa ya Simba kuimarisha club yenu.
 
Kuhusu kampuni zinazojitangaza kupitia jezi, tazama hii...


Kila kitu kiko wazi, sema labda haufuatilii au umeamua kwa makusudi "kumsagia kunguni" bwana Mohamed.
 
Subiri GSM afanye press conference na kuanza kulialia kuwa anapata hasara kuigaramia Yanga ndiyo ulete hoja yako hii.

Hao Liverpool mikataba yao imenyooka kama rula, hamna janjajanja kama ya mo. Shabiki yake furaha TU na kurukaruka kama pop corn kwenye kikaango timu ikishinda, lakini mwanachama lazima afahamu kila kitu kuhusu timu yake.
 
Nimewawekea hapo juu mkuu, BINADAMU TUMEUMBIWA KUSAHAU.
 
FCC wameshawapa Go Ahead Simba kuendelea na mchakato wa mabadiliko, ina maana hayo tayari yameshafanyiwa kazi.
Sasa wewe umeenda kutafuta taarifa za zamani, huko watu wameshatoka ndugu yangu.
Unakwama wapi ?
 
Hii ndiyo maana halisi ya mbumbumbu, mtu kaweka hoja we unaleta ushabiki
 
Upo sahihi, kwa maelezo ya Mwamedi nikama Simba haina kitu kabisa
 
Nadhani tutumie neno KUPANGA NI KUCHAGUA.
Kinachoweza kuwa sumu kwako, ni chakula kwa mwingine.

Hakuna haja ya kushikana mashati kwa sababu tumeamua kufanya machaguo tofauti.

Kimfaacho mtu, ndicho chake.
True...lkn si mashabiki kwa sisi mashabiki wa Simba na Yanga huwa hatuelewi hilo
 
Simba inaingia gharama kubwa za kujitakia kwa kukumbatia wachezaji wengi isiyowatumia. Lazima acknowledge hata kiwango kidogo cha mapato ya Simba badala ya kusema gharama zoooooooote analipa yeye. Hata gharama za kutangaza bidhaa zake zote anaitwisha Simba.
 
Apo suhala la kuhoji ni ayo mapato ya timu ata mm kwa upande wang sijaelewa timu ina mikataba zaid ya minne ukijumlisha na mengne inaweza kufka ata 2bl kwa mwaka,sasa mo anasema anatoa pesa kama yeye karbu 5 bl sio kama haiwezekan ila vzur angeelezea kwamba simba pamoja na mikataba yake na mapato yake yote kwa mwaka ni kias fulan matumiz ya timu kwa ujumla ni kias fulan kwaiyo apo ingekua rahis kujua kat ya mapato ya simba mo anaongezea kias gan ukisema ww unatoa kias fulan bila kusema timu inaingiza kias gan apo kuna ukakasi,ayo mengine sio kama mo analalamika ila ni anaongea kile anachofanya mtu ambae anatoa ela au ktu ikitokea siku anaongea hadharan lazma aseme kile anachofanya maana aliaid kufanya ayo anayosema kama atakaa kimya tu nan atajua sasa ,kama unakumbuka gsm walipishana kidogo kaur na uongoz wakatishia kujitoa ktk barua yao walielezea meng kuanzia mkataba wanachotakiwa kufanya lkn wakaongeza na mengine ambayo walisema wanafanya kwa mapenz nje ya mkataba sio kama waliongea vile kwa kulalamika ila umma ujue nin umuhimu wao na nn wanafanya
 
Mkuu hakusema gharama zote. Yeye alizungumzia kile alichokitoa yeye.

Kama ulivyoeleza kwamba Simba inaingia gharama kubwa kuwalipa wachezaji hata ambao haiwatumii, ni wazi hela ya Sportpesa, viingilio vya mlangoni, zawadi za kushinda mataji na kuingia makundi na robo fainali n.k isingeweza kutosha kumudu gharama za uendeshaji.

Mahitaji ya timu ni makubwa sana, kuna usajili, mishahara, posho, chakula, hoteli, usafiri, n.k

Kuna ubaya kusema aliongezea kiasi fulani ?
Labda kama utaniletea clip yoyote inayoonyesha kwamba alisema kwamba hiyo Bil 24 ndio ilikua hela pekee iliyoendesha klabu kwa miaka minne, kwenye press ya jana yule mtu hajayazungumza hayo.
 
Sawa lakini wao hawalalamiki wanazihudumia timu zao. Mo alitishia kujivua uwenyekiti na udhamini wakati timu ilipofungwa. Hatujawahi kusikia mwekezaji wa arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester united anawajambisha wanachama na shabiki wa timu kwa kutishia kujiuzulu pale timu inapofungwa. Mmiliki ambae anataka timu yake ishinde tuuuuuuu mechi zote kwakuwa analipa pesa zake vinginevyo anajiuzulu ni mwekezaji gani? Ni ligi gani hiyo duniani ambayo timu lazima ishinde mechi zote?
Mo atatuharibia mpira wetu kama tusipokuwa makini kwa kufanya "kila kitu" ili Simba ishinde kila mechi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…