Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nadhani tutumie neno KUPANGA NI KUCHAGUA.Wajinga ndo waliwao...
Hata iweje lazima awauze miquson konde boy na chama avute mkwanja mrefu. Chezea mo wewe.Kuwekeza siyo kujitolea. Ni lazma uwekeze na upate faida ya uwekezaji. Mo hajawahi kuweka faida anayoipata kwa uwekezaji wake na kimsingi anapata pesa nyingi kuliko alichowekeza. Its just business si kwamba anaipenda sana Simba No ni source of income kwake. Cha msingi hapa simba wangeweka wazi ili hata wawekezaji wengine wawe huru kuwekeza.
Akina sisi tusioingia kwenye vikao vya management ya Simba tunapaswa kupata taarifa za club yetu kupitia press conferences kama hizi, website ya club, Instagram na Facebook ya club, Simba tv. Yale yote anayoyasema pale hayapo pahala popote kwenye official media za Simba. Hata kusaini huo mchakato wa kukamilisha mabadiliko ya club na uwekezaji angalau tungeona picha za viongozi wetu wakisaini kwenye website au Instagram. Lakini website, Instagram hazina taarifa ya uendeshaji ya aina yoyote.Press ya jana ilikua ni kuueleza umma juu ya walipofikia katika uwekezaji na mchakato wa mabadiliko ya Simba.
Haimaanishi kwamba jana ndio wameeleza kila kitu (further details) pale. Ndio maana nikashauri kama wewe unataka hizo deep info unaweza kuzipata kama ukifuatilia kwenye ngazi husika (FCC, kwenye vikao vya klabu, kupitia vyanzo mbalimbali vya habari vya klabu, n.k). Kama kukwambia ufanye hivi ni kumaanisha kwamba press ya jana haikua na umuhimu, basi unisamehe sana.
Nitoe mfano mdogo tu:
Udhamini wa bidhaa za Mo kwenye jezi za Simba ni wa kimkataba, ilifanyika press wakasaini na kutangaza kwa umma.
Sasa wewe unapotumia suala la udhamini huu kama ishara ya "utapeli" wa Mo, ina maana ama haufuatilii kinachoendelea, au umeamua tu kutuuliza "akina sisi" ili kama hatuna kumbukumbu juu ya hili tuungane nawewe katika kumlalamikia Mo.
Kwanini usingejiridhisha kwamba udhamini ule si wa kimkataba na klabu haipati pesa, ndipo hoja hiyo uijumuishe katika madai yako hapo juu ?
Ina maana unataka Mo aanze kuyazungumzia mambo haya kwenye press mkuu ?
Sikubezi katika hoja zako, ila naona kwamba mengi unayoyahoji unaweza kuyapatia majibu katika ngazi sahihi endapo ukiamua kufuatilia.
Kuhusu suala la MO PEKE YAKE kutoa 20B:
Kama kwenye structure ya Simba inaruhusu mtu mmoja kuweka 20B na akachukua 49% ya hisa, kosa la Mo hapa linakua ni lipi ?
Kama unafahamu kwamba structure ya Simba inataka wawekezaji wanne ndio wagawane hizo 49% sema hapa ili tujue kwamba Mo amekiuka kipengele hicho, na useme ni ibara ipi au sheria ipi iliyokiukwa.
Kama unafanya marejeo kwenye timu nyingine nadhani utakua unakosea na unalazimisha mambo yaende your way.
Ripoti za mapato na matumizi ya klabu zipo, unataka Mo aje kwenye press kuzisoma pale ili nawewe ufahamu kwamba deficit zilikua kiasi gani na akaongezea hela yake ?
Hivi ndivyo taasisi zinaendeshwa ?
Kusomeana mapato na matumizi kwenye vyombo vya habari ?
Ndugu yangu mambo mengi uliyoyahoji hapo unaweza kuyapatia majibu kirahisi sana, haujaamua tu. Niamini mimi.
Nadhani jamaa kasema hivyo akimaanisha kwamba, wanaosema hiyo hela (20B) ni ndogo basi wafahamu kwamba kwanza hiyo ni "concern" yao wanasimba wenyewe, hivyo ingeweze kuwa ndogo zaidi ya hapo (mfano wake ndio hiyo jero).Mkuu,kila mtu anakufa.
Hoja yangu ilitokana na comment iliyosema "hata akitoa jero,waanasimba wanataka furaha"
Yaan akiondoka ataacha nini kwa kutoa jero?
Suala la udhamini wa jezi lipo kwenye official Instagram page ya Simba, uwe unafuatilia mkuu.Hata iweje lazima awauze miquson konde boy na chama avute mkwanja mrefu. Chezea mo wewe.
Akina sisi tusioingia kwenye vikao vya management ya Simba tunapaswa kupata taarifa za club yetu kupitia press conferences kama hizi, website ya club, Instagram na Facebook ya club, Simba tv. Yale yote anayoyasema pale hayapo pahala popote kwenye official media za Simba. Hata kusaini huo mchakato wa kukamilisha mabadiliko ya club na uwekezaji angalau tungeona picha za viongozi wetu wakisaini kwenye website au Instagram. Lakini website, Instagram hazina taarifa ya uendeshaji ya aina yoyote.
KinachonishangazaMo tapeli Tu na sitashangaa Simba ikimshinda
Alishindwa Singida united akakimbia
Akashindwa Africa Lyon akakimbia..
Ana usanii mwingi
Hayo maswali watu wengi wanauliza..
Kubandika bidhaa zake .. kwenye magari na kesi..je Simba walitangaza bid?
Kampuni yake ndo highest bidder?
Au analazimisha kwa bei anayotaka?
Maswali mengi kuliko majibu
Tume ya Ushindani (FCC) imeanza uchunguzi wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Simba ambao inawahusu wadaawa watano.Umekaza sana kichwa, nice moves, kwaiyo wewe huwezi ku access vyanzo vya habari vya FCC hadi ushiriki vikao vya Simba mkuu ?
Sportpesa nayo ni ya Mo. Roho mbaya haijengi mkuu. Mbona Jersey za Ndala zimejaa matangazo ya GSM na hamna anayehoji!Kinachonishangaza
Hivi ukiwa muwekezaji binafsi ndio na kampuni zako zingine zinapata upenyo wa kujitangaza humo humo .
Jezi za Simba zimejaa kampuni za mo,je amelipia hizo au ndio kwenye hizo hizo hela anazotoa bili20
Je ikija kampuni ingine ikitaka kununua haki za kujitangaza kwenge jezi je mo atakubali .
Kufanya biashara na muhindi tegemea magumashi kila Kona?
Kuhusu kampuni zinazojitangaza kupitia jezi, tazama hii...Kinachonishangaza
Hivi ukiwa muwekezaji binafsi ndio na kampuni zako zingine zinapata upenyo wa kujitangaza humo humo .
Jezi za Simba zimejaa kampuni za mo,je amelipia hizo au ndio kwenye hizo hizo hela anazotoa bili20
Je ikija kampuni ingine ikitaka kununua haki za kujitangaza kwenge jezi je mo atakubali .
Kufanya biashara na muhindi tegemea magumashi kila Kona?
Subiri GSM afanye press conference na kuanza kulialia kuwa anapata hasara kuigaramia Yanga ndiyo ulete hoja yako hii.Mashabiki wa Liverpool FC, Manchester United, FC Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, PSG, AC Milan, Al Ahly, Mamelodi Sundowns, TP Englebert Mazembe, Kaizer Chiefs FC na Simba SC hatuna haja sana ya kujua Mapato, ila tuna haja mno ya Ubingwa na Klabu zetu Kuzidi Kung'aa Locally na Internationally kama zing'aavyo sasa.
Hivi kwa Mfano kama Mimi GENTAMYCINE nasikia Simba SC inachukua Ubingwa wa VPL na ASFC tena mfululizo huku katika CAF CL najitahidi kufanya vyema na hata huyo ( hao ) Wababe wa Afrika akina Al Ahly na Kaizer Chiefs nawafunga na Moyo wangu Unaridhika huku nikinenepa kwa Furaha hizo Pesa za Mo au kama anatuibia Simba SC zinanihusu nini?
Halafu kuna Watu wengine ni Wapumbavu na mna Wivu wa Kiuswahili. Hivi kuna Mfanyabiashara ambaye anawekeza kisha nae asitafute mwanya wa Kupiga Hela na Kujifaidisha na Kujitajirisha zaidi? Mnafiki mkubwa Wewe na Chuki zako na Mawazo yako haya ya Kimasikini.
Unashangaa Mo Dewji Kujitajirisha kupitia Simba SC mbona hushangai GSM alivyowadanganyeni Yanga SC kuwa tokea aingie hapo amechapisha tu Jezi 80,000 wakati ukweli ni kwamba mpaka hivi sasa GSM amechapisha Jezi 250,000 za Yanga SC? au unataka sasa tunaoyajua ya ndani ya Yanga SC kupitia Viongozi wao Waandamizi ambao ni Marafiki zetu tuseme yanayoendelea huko Yanga SC Kwenu ili Amani itoweke na Mvurugane zaidi?
Mo tuibie Baba, ila tupe raha Simba SC!!
Nimewawekea hapo juu mkuu, BINADAMU TUMEUMBIWA KUSAHAU.Sportpesa nayo ni ya Mo. Roho mbaya haijengi mkuu. Mbona Jersey za Ndala zimejaa matangazo ya GSM na hamna anayehoji!
Kwani hukuona ama kusikia Melt Group wakiingia mkataba wa udhamini na club ya Simba?
Watani zetu acheni roho mbaya haijengi. Tumieni makosa ya Simba kuimarisha club yenu.
FCC wameshawapa Go Ahead Simba kuendelea na mchakato wa mabadiliko, ina maana hayo tayari yameshafanyiwa kazi.Tume ya Ushindani (FCC) imeanza uchunguzi wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Simba ambao inawahusu wadaawa watano.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na FCC, wadaawa hao ni Simba Sports Club Holding Company Limited ambaye ni mdaawa wa kwanza, Mo Simba Company Limited (Mdaawa wa pili), Simba Sports Club Company Limited, Simba Sports Club na Mohammed Gulamabbas Hassanali Dewji.
Taarifa ya FCC imesema kuwa mdaawa wa tatu kwa kushirikiana na mdaawa wa kwanza, pili na tano walichukua mali na biashara za mdaawa wanne Tanzania Bara bila kuitaarifa tume hiyo kinyume na sheria ya ushindani kifungu cha 11 (2), 11 (6) (cha mwaka 2018) na kizingiti cha muunganiko wa makampuni cha mwaka 2017.
"Januari 6 mwaka huu, FCC ilifanya maamuzi kwa kutoa matokeo ya awali kuhusiana na tuhuma zinazowakabili wadaawa wote watano.
"Kitendo cha wadaawa wote watano kushindwa kuitaarifu FCC juu ya muunganiko huo wa makampuni kilisababisha kuinyima tume hiyo nafasi ya kutekeleza jukumu lake la kisheria la kufanya tathmini juu ya uhalali wa muunganiko huo unaotuhumiwa kutotaarifiwa kwake kwa mujibu wa sheria," imesema taarifa hiyo.
Hii ndiyo maana halisi ya mbumbumbu, mtu kaweka hoja we unaleta ushabikiWewe chura FC ukishajua itakusaidia nn?? Cc wanasimba ata akitoa jero tunaomba apewe timu yote aimiliki na akipenda abadilishe na jina iwe Mo FC muhimu mashabiki tunapata FURAHA timu inafanya maajabu basi tunafurahi ayo mengine ni kukompliketi mambo mwaisa
Upo sahihi, kwa maelezo ya Mwamedi nikama Simba haina kitu kabisaKuwekeza siyo kujitolea. Ni lazma uwekeze na upate faida ya uwekezaji. Mo hajawahi kuweka faida anayoipata kwa uwekezaji wake na kimsingi anapata pesa nyingi kuliko alichowekeza. Its just business si kwamba anaipenda sana Simba No ni source of income kwake. Cha msingi hapa simba wangeweka wazi ili hata wawekezaji wengine wawe huru kuwekeza.
True...lkn si mashabiki kwa sisi mashabiki wa Simba na Yanga huwa hatuelewi hiloNadhani tutumie neno KUPANGA NI KUCHAGUA.
Kinachoweza kuwa sumu kwako, ni chakula kwa mwingine.
Hakuna haja ya kushikana mashati kwa sababu tumeamua kufanya machaguo tofauti.
Kimfaacho mtu, ndicho chake.
Simba inaingia gharama kubwa za kujitakia kwa kukumbatia wachezaji wengi isiyowatumia. Lazima acknowledge hata kiwango kidogo cha mapato ya Simba badala ya kusema gharama zoooooooote analipa yeye. Hata gharama za kutangaza bidhaa zake zote anaitwisha Simba.Huyu jamaa sijui hata humo kichwani kwake zimo, eti ametaja kuuza wachezaji kama chanzo cha mapato cha Simba (akijumuisha na mapato ya mlangoni, nashukuru hili umemjibu).
Kwa misimu minne iliyopita Simba haijaingiza hata MILIONI 200 kwa kuuza wachezaji, wengi wameondoka free agents, sasa sijui anapata wapi ujasiri wa kusema kwamba simba imepata mapato kwa kuuza wachezaji.
Humu JF tunatakiwa kuvumiliana sana.
Mkuu hakusema gharama zote. Yeye alizungumzia kile alichokitoa yeye.Simba inaingia gharama kubwa za kujitakia kwa kukumbatia wachezaji wengi isiyowatumia. Lazima acknowledge hata kiwango kidogo cha mapato ya Simba badala ya kusema gharama zoooooooote analipa yeye. Hata gharama za kutangaza bidhaa zake zote anaitwisha Simba.
Sawa lakini wao hawalalamiki wanazihudumia timu zao. Mo alitishia kujivua uwenyekiti na udhamini wakati timu ilipofungwa. Hatujawahi kusikia mwekezaji wa arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester united anawajambisha wanachama na shabiki wa timu kwa kutishia kujiuzulu pale timu inapofungwa. Mmiliki ambae anataka timu yake ishinde tuuuuuuu mechi zote kwakuwa analipa pesa zake vinginevyo anajiuzulu ni mwekezaji gani? Ni ligi gani hiyo duniani ambayo timu lazima ishinde mechi zote?Mkuu, kwani wewe unatatizwa na watu kupata faida wakiwekeza sehemu ?
1. Mo akiwekeza Simba akapata faida, hupendi ?
2. GSM, Manji, Rostam wakiwekeza Yanga na wakapata faida, hupendi ?
3. Motsepe akiwekeza Mamelodi akapata faida, unaumia ?
4. Glaziers wakiwekeza Man Utd na wakapata faida, unateseka ?
5. Sheikh Mansour akiwekeza City na akapata faida, roho inakuuma ?
Wewe mwenyewe UKIWEKEZA kwenye KILIMO au sekta ya MADINI na UKAPATA FAIDA, huwa unaumia pia ?
Mbona kama inataka kuonekana kwamba habari njema kwako ni pale tu ambapo Mo atakua HAFAIDIKI kwa chochote kwenye uwekezaji wake pale Simba ?
Ujuaji, Wivu na Roho mbaya vitatumaliza watanzania (nikiwemo mimi).