Aliyemuelewa Mo Dewji kuhusu uwekezaji Simba atujuze

Tuache kumtukana mo,alichofanya ni kizuri mno kwa maendeleo ta simba na soka,japo mie ni yanga

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Hilo jamaa kavulata ni jinga fulani hivi miaka yote simba ipo hakuna aliyethubutu kuweka mpunga
Huo ndio ujinga wako. Simba ilikuwepo tangu 1936 mbona ipo? Samani ya Simba ni kubwa sana. Wahindi wanaujuwa ukubwa wa simba na yanga kuliko wanachama wenyewe. Kuna wafanyabiashara ambao utajiri wao leo umetokana na simba na yanga. Hizi timu zina mashabiki kila mkoa kila wilaya na kila kitongoji. Lakini wanasimba waziona 20b eti ni nyiiiiiingi sana kiasi cha kutukana kila mtu anaehoji integrity ya mo kwenye uwekezaji huu. Huwezi kuweka mayai yako yoote kwenye kikapu kimoja lakini simba imempa mo hiza zote 49% peke yake na mtu asihoji; na mtu asiulize. Ina maana mo akijikwaa mayai yetu yoote yatavunjika. Ndio maana mo alivyotishia kujivua uwanachama kila shabiki na kila mwanachama alitoa punzi kwenye kila tundu la mwili wake. Manji alipopatwa na msukosuko tuliona mabakuli kila kona. Hatujifunzi tu? Nani katuroga ngozi nyeusi.
Hilo jamaa kavulata ni jinga fulani hivi miaka yote simba ipo hakuna aliyethubutu kuweka mpunga
 
YANGA TV 40B KWA MIAKA 10.
SIMBA 20B KWA MAISHA NANI HAPO MWENYE BONGO?
 
Mm sijaona tatizo la MO amesema amesema ashamalizana na FCC na bilioni 20 kaweka sasa tatizo ni nn?tunawasubiri mpili fc nao wakamilishe bila kulalamika
 
Mbumbumbu katika ubora wao muachwe na litimu lenu maana Mo anawapa mapenzi motomoto hamuoni wala hamtaki kusikia , kila kitakachohojiwa ni utopopolo.
Mngepewa nchi hii nyie mngeshatuuza watanzania wote kwa mabeberu maana so kwa upofu huo wa akili.
Hata uto si mna timu lenu mbona kutwa kuhangaika na nyumba ya jirani wakati wewe pia umeshindwa ku manage ya kwako
 
Hela kuitoa inauma wewe asikuambie mtu. Ushawahi kupewa hela na mkeo uone utakavyosimangwa?
Mo anahitaji kupongezwa sana.
Sure Ile ni economic resource kwa sio rahisi Kama mtoa post anahoji kirahisi akiwa kalala anasubiri chai kwa mama
 
Reactions: mmh
Kama ni hivyo basi asingeitisha press conference kumbe wadhamini wanafahamu kila kitu. Ametusumbua kutuita kwasababu gani kama kila kitu kinafahamika kwenye kamati. Mo peke yake ndiye katoa 20b za 49% ya hisa, kanuni inasema hivyo?
Unataka kanuni ipi brother,mwakyembe alishafafanua kuhusu hisa za mo sasa wewe unaturudisha nyuma kwa uzembe wako wa kutofuatilia toka mwanzo.
 
Tatizo kubwa wengi mnahoji baada ya kuweka hela mwanzoni mlikuwa mnahoji kwa nn haweki hizo bilioni 20,sasa hamueleweki mnataka nn?
 
YANGA TV 40B KWA MIAKA 10.
SIMBA 20B KWA MAISHA NANI HAPO MWENYE BONGO?
Acha kudanganya watu, 40B sio uwekezaji ni haki ya matangazo ambayo hata klabu nyingine zipo katika mazungumzo na Azam.

Usijelia siku ukisikia simba kachukua zaidi ya hiyo 40B katika haki hiyo maana ni timu yenye mafanikio makubwa zaidi
 
Yaap. Kikubwa timu ishinde tu..
 
Mbumbumbu katika ubora wao muachwe na litimu lenu maana Mo anawapa mapenzi motomoto hamuoni wala hamtaki kusikia , kila kitakachohojiwa ni utopopolo.
Mngepewa nchi hii nyie mngeshatuuza watanzania wote kwa mabeberu maana so kwa upofu huo wa akili.
Mkuu Mo atakuwa anatuibia unaonaje tukupe wewe hizo asilimia 49?..
 
Wasio na akili timamu utawasikia wakisema ili mradi timu yao inafanya vizuri viwanjani haya mengine hayawahusu.

Kumbe ni ujinga umewajaa kichwani na baadae huko mbele mambo yakienda mlama watashindwa kutafuta mchawi ni nani.
Mambo kwenda mrama kiaje? Embu tabiri kivipi unahisi mambo yanaweza kwenda mrama huko mbele ya safari?.
 
Wakati mpo mitandaoni mnatoa hoja Mo yupo simba anatoa pesa, hiyo ndio tofauti. Kwanini hajitokezi mtu akasema yeye atatoa bilioni 800 kwa hizo 49% shares?
Wanashangaza sana mkuu..
 
Hela kuitoa inauma wewe asikuambie mtu. Ushawahi kupewa hela na mkeo uone utakavyosimangwa?
Mo anahitaji kupongezwa sana.
Halafu mtu anatoa billions wanataka asilalamike na kuwakumbusha kuwa mpunga anatoa ni mwingi hivyo umakini unahitajika..
 
Reactions: mmh
Maswali

1. Hao wawekezaji wengine walikua wapi kabla ya Mo? Kwann hawakuwekeza?

2. Kama kuna pesa anatengeneza, kwann simba ilishindwa jiendesha yenyewe wakati hayupo?? Hizo pesa zilikua wapi muda huo zisionekane?
 
Wewe acha tu apige hela. Sisi simba hatuna faida nayo nyingine yoypte zaidi ya matokeo ya uwanjani. Aichukue hata bure kikubwa wachezaji walipwe na matokeo yaonekane uwanjani.
 
Wewe ni mjinga wa asili, yani wa kuzaliwa kabisa

Hiyo simba unayosema inafanya vizuri Africa mashariki na kati, ni nani kaiwezesha ifanye hivyo?? Au imetokea Kama miujiza tu sio?? Yani Mo aweke pesa yake timu ifanye vizuri alafu uje umhukumu kwa pesa yake hiyo hiyo???

Kabla ya Mo Simba ilikuaje?? Kwann haikufanya vizuri ?? Hiyo pesa inayopatikana saiv simba miaka minne nyuma ilikua wapi??

Kaa chini kitulize
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…