Wachezaji wazuri hawawezi kuja Simba na Yanga tuseme ukweli. Tunaowasajili kutoka nje hawana thamani hiyo tunayowapa. Kuna watanzania ambao wanawazidi akina kagere, kahata, shikalo, sarpong, Wawa, Yacouba na wengine lakini hawapewi nafasi TU na makocba. Hata makocha wengine hawana uwezo wa kuwazidi akina Mkwasa lakini hawapewi nafasi.
Hivyo, tuwe makini na sajili zinazotuongezea gharama za kuendesha timu. Kama Tanzania kuna mchezaji mzuri lazima atapenda kuondoka kwenda timu nzuri kama Al-Ahly, Raja, Masri, Ulaya, nk.