Mashabiki wa Liverpool FC, Manchester United, FC Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, PSG, AC Milan, Al Ahly, Mamelodi Sundowns, TP Englebert Mazembe, Kaizer Chiefs FC na Simba SC hatuna haja sana ya kujua Mapato, ila tuna haja mno ya Ubingwa na Klabu zetu Kuzidi Kung'aa Locally na Internationally kama zing'aavyo sasa.
Hivi kwa Mfano kama Mimi GENTAMYCINE nasikia Simba SC inachukua Ubingwa wa VPL na ASFC tena mfululizo huku katika CAF CL najitahidi kufanya vyema na hata huyo ( hao ) Wababe wa Afrika akina Al Ahly na Kaizer Chiefs nawafunga na Moyo wangu Unaridhika huku nikinenepa kwa Furaha hizo Pesa za Mo au kama anatuibia Simba SC zinanihusu nini?
Halafu kuna Watu wengine ni Wapumbavu na mna Wivu wa Kiuswahili. Hivi kuna Mfanyabiashara ambaye anawekeza kisha nae asitafute mwanya wa Kupiga Hela na Kujifaidisha na Kujitajirisha zaidi? Mnafiki mkubwa Wewe na Chuki zako na Mawazo yako haya ya Kimasikini.
Unashangaa Mo Dewji Kujitajirisha kupitia Simba SC mbona hushangai GSM alivyowadanganyeni Yanga SC kuwa tokea aingie hapo amechapisha tu Jezi 80,000 wakati ukweli ni kwamba mpaka hivi sasa GSM amechapisha Jezi 250,000 za Yanga SC? au unataka sasa tunaoyajua ya ndani ya Yanga SC kupitia Viongozi wao Waandamizi ambao ni Marafiki zetu tuseme yanayoendelea huko Yanga SC Kwenu ili Amani itoweke na Mvurugane zaidi?
Mo tuibie Baba, ila tupe raha Simba SC!!