Aliyemuua askari Arusha adaiwa kufa akijaribu kuwatoroka polisi

Aliyemuua askari Arusha adaiwa kufa akijaribu kuwatoroka polisi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
753
Reaction score
1,812
Jambazi aliyemuua kwa kumkata mapanga Askari polisi, H.2407 Constable Damasi Magoti wa kituo Cha polisi Mbughuni wilayani Arumeru, Jacob Kideko au Ramadhani Kichwa(43) Mkazi wa Makiba amefariki dunia katika jaribio la kuwatoroka polisi alipokuwa akisafirishwa jijini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda was polisi mkoa wa Arusha, Justine Masejo,jambazi huyo alikamatwa julai 27 mwaka huu Mkoani Morogoro alikokuwa amejificha kukwepa polisi na walipofika eneo la Kisongo jijini Arusha akiwa kwenye gari amefungwa pingu mkononi alijaribu kuruka kuwakimbia polisi.

Taarifa hiyo inadai kwamba mtuhumiwa alipata majeraha kichwani na michubuko kwenye mwili wake, Hata hivyo polisi walijaribu kuokoa Maisha yake kwa kumpeleke katika hospital ya Mkoa Mount Meru ,lakini alipoteza Maisha akiwa njiani.

Inadaiwa kuwa jambazi huyo alikuwa akisakwa na Askari wa gereza kuu la Arusha baada ya kufungwa miaka 16 ,Septembe 10 ,2008 lakini alitoroka mnamo April 1, 2017 akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza.

Marehemu Magoti aliuawa usiku Julai 23 mwaka huu wakati akitekeleza majukumu yake katika Kijiji Cha Makiba akijaribu kumkamata mtuhumiwa wa wizi nyumbani kwake, ndipo jambazi huyo alitokea jirani na eneo la tukio na kumshambulia kwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali na kupoteza Maisha.
 
Back
Top Bottom