Aliyemuua askari Arusha adaiwa kufa akijaribu kuwatoroka polisi

Aliyemuua askari Arusha adaiwa kufa akijaribu kuwatoroka polisi

jambazi huyo alikamatwa julai 27 mwaka huu Mkoani Morogoro alikokuwa amejificha kukwepa polisi na walipofika eneo la Kisongo jijini Arusha akiwa kwenye gari amefungwa pingu mkononi alijaribu kuruka kuwakimbia polisi.
šŸ™‰šŸ™ˆ
 
Huu ni uongo uliowazi kabisa..

Ni kama wale wafungwa waliouliwa mafia kwa kupigwa then baadhi ya Askari waliandika vivohivyo kwamba wameruka kwenye gari.

Na wengine wakaandika ukweli wa kilichotokea.
Nusu ya Askari wakaenda mahabusu na nusu wakabaki.

Hilo jambazi wameliua kwa makusudi na linastahiri hicho kifo.
 
Hamna kuundwa kamati wala chchte, tunajua hakuruka kwenye gari wala nn ila amepata anachostahili, Hakika kifo chake kilikua chauchungu mno.
Karma.

Ni kama alivyokuwa akimpiga mwenzake mapanga, kama angefikiria yeye angejisikiaje basi asingefanya hivyo.

Wakati mwingine ni vizuri kupigana na moto kwa moto ili haya majitu yenye roho mbaya yapungue.
 
Jambazi aliyemuua kwa kumkata mapanga Askari polisi, H.2407 Constable Damasi Magoti wa kituo Cha polisi Mbughuni wilayani Arumeru, Jacob Kideko au Ramadhani Kichwa(43) Mkazi wa Makiba amefariki dunia katika jaribio la kuwatoroka polisi alipokuwa akimsafirishwa jijini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Arusha,jambazi huyo alikamatwa julai 27 mwaka huu Mkoani Morogoro alikokuwa amejificha kukwepa polisi na walipofika eneo la Kisongo jijini Arusha akiwa kwenye gari amefungwa pingu mkononi alijaribu kuruka kuwakimbia polisi.

Taarifa hiyo inadai kwamba mtuhumiwa alipata majeraha kichwani na michubuko kwenye mwili wake, Hata hivyo polisi walijaribu kuokoa Maisha yake kwa kumpeleke katika hospital ya Mkoa Mount Meru ,lakini alipoteza Maisha akiwa njiani.

Inadaiwa kuwa jambazi huyo alikuwa akisakwa na Askari wa gereza kuu la Arusha baada ya kufungwa miaka 16 ,Septembe 10 ,2008 lakini alitoroka mnamo April 1, 2017 akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza.

Marehemu Magoti aliuawa usiku Julai 23 mwaka huu wakati akitekeleza majukumu yake katika Kijiji Cha Makiba akijaribu kumkamata mtuhumiwa wa wizi nyumbani kwake, ndipo jambazi huyo alitokea jirani na eneo la tukio na kumshambulia kwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali na kupoteza Maisha.
KISONGO...... !!!!!!
 
Huyo marehemu anayeitwa jambazi ukute hakuwahi iba hata ufagio.

1. Nani anaweza prove kwamba alifungwa miaka 16 pale Kisongo kisha akatoroka ila akaendelea kuishi palepale Arusha
2. Kilichomfanya amuue askari kwa mapanga usiku kwa jirani yake aliyetakiwa kukamatwa ni nini. Hii kesi anayodaiwa kuvamia wala hakumuhusu
3. Huyo askari namna gani ameenda peke yake usiku kumkamata mtuhumiwa nyumbani kwake
4. Marehemu jambazi aliwezaje kuruka kwenye gari wakati yuko chini ya ulinzi na kafungwa pingu. Ina maana askari wetu ni wazembe kiasi hiki

Hii kesi bila hata kutumia akili ina ukakasi mwingi
 
Naomba wote tulio iamini hii taarifa kutoka Jeshi letu la polisi tukutane hapa!! Mimi naanza 100% hii taarifa ni ya kweli šŸ™„
hata Mimi mkuu naiamini hii taarifa Kama nilivyoamini Ile ya askari aliyepiga risasi juu ikakata Kona,ikajipinda na kwenda kumpiga Binti Akwilina!

Polisi wetu Wana weredi wa hali ya juu sana kuliko wale wa FBI!


Nadanganya?
 
Back
Top Bottom