Aliyeng'atwa na Nyoka afia Kituo cha Afya kisa hana 150,000 Wilayani Babati

Aliyeng'atwa na Nyoka afia Kituo cha Afya kisa hana 150,000 Wilayani Babati

Wasukuma Bagosha wanadawa za nyoka..

Kule mpaka Kuna majani yanaitwa MZIMA ukiweka mfukoni unakatiza msitu mzito hakuna Simba Wala nyoka wanakukwepa.
Hahaha naufahamu mzima ila sikujua kuhusu hili...

Kuhusu dawa za nyoka ni kweli zipo, maeneo yale mtu akiumwa nyoka haendi hospitali.
 
Ulipata bahati ya kugongngwa na nyoka asiye na sumu kali.
Kuna nyoka wana sumu kali balaa huyoboi kwenye dawa za ujanja ujanja.
Basi ukienda Tabora utashangaa zaidi...

Pale kuna wakati inahitajika nguo ya mgonjwa tu inatibiwa na mgonjwa anapona huko aliko...
 
Mboni wamesema 150,000
Vyovyote vile lkn jua hiyo ndiyo range ya bei zake (100k-300k).

Na vinahitajika vichupa mpaka 4 sometimes...

So ukifikiria kimoja tu ndugu wameshindwa kulipia, inakuwa kisanga..

Na protocol za uuzaje kwenye hospitali zote ni "Pre-Paid".
 
Hata hekima ya kawaida ya kiutu iliwafanya hao watatu waliokuwa na mgonjwa washindwe kupokea bond ya pikipiki ya mume wa mgonjwa ili matibabu yatolewe?

Ndiyo kwenye kazi kuna boss lakini ishu mezani ni nzito mtu anataka kufa kuna opti ya kufanya atibiwe malipo baadae hata huyo anayejiita dk mkuu angeelezwa tu mgonjwa kwa hali yake ilibidi mumewe aweke dhamana chombo chake funguo hii hapa atakuja kulipa basi wangekuwa wameokoa maisha tatizo hao hawakuumbwa wawe madaktari sometimes waliumbwa kuwa mafundi magari.
Mkuu, kuna baadhi ya protocols huko utumishi wa umma huwa ni ngumu sana kwa wafanyakazi wa chini.

Hapana lawama zote zinaenda kwa MGANGA MFAWIDHI.

Case kama hii yeye ndiyo anapaswa atoe go ahead ili wale wa chini waweze kutoa hiyo dawa.

Anaposema yuko mbali, wale walioko kazini ndiyo wafanye maamuzi ni anawauzia msala ambao yeye ndiyo anapaswa ausovu.
 

KATIKA hali ya kusikitisha, mkazi wa Magugu, Wilaya ya Babati, Juliana Obedy (44), amepoteza maisha baada ya wataalamu katika Kituo cha Afya Magugu, kudaiwa kumcheleweshea huduma kituoni hapo kutokana na kugongwa na nyoka.

Imedaiwa kuwa, sababu za kucheleweshwa kwa huduma hiyo ni wataalamu kutaka kulipwa Sh. 150,000 ikiwa ni gharama za matibabu.

Akisimulia mkasa huo jana, mume wa Juliana, Obedy Laizer, alisema Desemba 16, mwaka huu, akiwa anavunja jengo la Kanisa la Katoliki Magugu, mke wake alipita akiwa anachuma mboga za majani na kung'atwa na nyoka ambaye hakujua ni wa aina gani.

Laizer alisema baada ya muda mfupi mke wake kuondoka, alikuja mtoto wake na kumwambia anaitwa na mama yake ambaye alidai kung'atwa na nyoka, ndipo alipokimbia kumpeleka Kituo cha Afya Magugu.

Alipomfikisha kituoni hapo kulikuwa na foleni na kushauriana na mke wake waingie ndani na kujisajili, lakini wauguzi waliwaambia kuwa daktari alikuwa chumba cha wazazi na kuomba apigiwe simu ili kuja kumsaidia.

"Daktari alipigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, akapigiwa simu mara ya pili ndipo alipopokea akasema anakuja na alitoa huduma na mgonjwa kuandikiwa dawa," alisema Laizer.

Hata hivyo, alisema alipoenda duka la dawa aliambiwa anatakiwa kulipia Sh. 150,000 ambapo Laizer aliomba mgonjwa ahudumiwe na fedha itafuata, lakini wauguzi wawili na daktari mmoja waliokuwapo hawakukubali na kuamua kumpigia Mganga Mfawidhi simu na kujibiwa kuwa anatakiwa alipie Sh. 150,000 na kukata simu.

Laizer alisema baada ya kuvutana na wataalamu hao alitoka na kwenda kutafuta fedha aliporudi alitoa Sh. 130,000 na badala ya kuanza kutoa huduma, wataalamu hao walianza kupigiana simu ndipo mmoja alisikika akisema mgonjwa ahudumiwe.

Aidha, alisema baada ya kulipia fedha hiyo muuguzi anayehusika na dawa alimpeleka duka la dawa na kumpatia na walirudi kwa mgonjwa ambako alifukuzwa wodini, lakini aligoma akitaka kushuhudia mke wake akihudumiwa.

Alisema mgonjwa aliulizwa anajisikiaje naye akajibu kuwa anajisikia vibaya huku akisema “Bwana Yesu nisaidie” ghafla aliacha kuongea na ndugu na majirani waliokuwapo walianza kumwombea kwa kushirikiana naye bila mafanikio.

Alisema baada ya mke wake kukata kauli wauguzi waliendelea kumchua na kumwekea oksijen, lakini alipoona haisaidii aliwaambia waitoe.

"Baada ya kuona hivyo niliwaambia mke wangu ndio anaondoka hivyo, tulienda duka la dawa wakanipa dawa ya Sh. 6000 ya kumpunguzia maumivu na sikupewa risiti, wala ile ya 150,000 sikupewa," alisema.

Akiongea kwa uchungu alisema licha ya kuwaomba aweke rehani pikipiki yake na kuwapa funguo wauguzi ili wamhudumie mke wake waligoma na kudai akikimbia wao ndio wanawajibika.

Mtoto wa marehemu, Abednego Obedy, alisema mama yake alimwonesha mkono ukiwa umevimba na kumwambia ameng'atwa na nyoka na kumshauri kwenda kituo cha afya.

Aidha, Enoti Philipo ambaye alikuwa akimwita marehemu shangazi, alisema alitoka nyumbani kwake kuchuma mboga za majani na baadaye aliona mume wake anamkimbiza hospitali.

Mkazi wa kijiji hicho, Yona Laizer, alisema kitendo kilichofanywa na wataalamu hao ni uzembe na unyama ambao kama wakiendelea watasababisha vifo vingi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Magugu, Lohay Amos, alilaani tukio hilo na kuwataka wauguzi na madaktari kutii viapo vyao.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Magugu, Dk. Kusta Ndunguru, alikiri kupigiwa simu na Laizer huku akisema alijua anathibitisha malipo aliyoambiwa.

Dk. Ndunguru alisema alimwambia aongee na wataalamu waliopo hospitali ili wamsaidie kwa kuwa yeye yuko nje ya kituo na hakumrudia.

Alisema mtu aking'atwa na nyoka mwenye sumu kali haitakiwi kuzidi nusu saa kwasababu ikizidi anapoteza maisha ndio maana alimwambia awaeleze wataalamu ili wamsaidie asipoteze muda.

Chanzo: Nipashe
Kuna wajinga flani wanatoka vyuoni na kuajiriwa then wanapewa kuwa incharge kwenye vituo hivi vya afya , ni wajinga sana ,hajai uongonzi ,kazi kujipendekeza kwa kwa MaDMO , mfano katika case hii, uyu alikua ni mgojwa wa kulazwa ,kulikua na ulazima gani kimbizana na pesa ilihali mgojwa yupo apo kituoni badala ya kumpa huduma, Mhimbili watu wanatibiwa na bili sembuse huku chini.

Ndio kifo kipo ila angalau onesha kujali uhai wa mtu awapo mikononi mwako katika critical condition. May be wangeanza muona mapema hata kama huduma pale ilikua haitoshi wangeweza kutoa referal mapema.

Ifike mda kwa uzembe kama huu , wawe wanashitakiwa kwa majina yao binafsi ndo iwe dawa
 
Kimsingi ni kwamba Anti-Venom ni PRE-PAID.

Wale wahudumu hii sheria inawabana, wasingeweza kuitoa hata uwe umepeleza 100 bila go-ahead kutoka kwa mkubwa wao.

Hapo Mganga Mfawidhi kazingua big time, alipasws yeye ndiyo awapigie na kuwapa go ahead mgonjwa apewe dawa..
Anti -venon ndio 150k, ndugu yangu juzijuzi kang'atwa pale Kinyerezi akaenda hospitali akachomwa bure pale kituo cha afya. Alitoa hela ya dawa za maumivu na kadi tu.
 
Basi ukienda Tabora utashangaa zaidi...

Pale kuna wakati inahitajika nguo ya mgonjwa tu inatibiwa na mgonjwa anapona huko aliko...
Tabora na koboko wale? Sikubishii bali kama kuna antivenon za kiswahili za kutibu sumu ya koboko wazungu inatakiwa waende kujifunza huko Tabora,
Koboko ni moja ya nyoka wenye sumu kali sana
 
Tabora na koboko wale? Sikubishii bali kama kuna antivenon za kiswahili za kutibu sumu ya koboko wazungu inatakiwa waende kujifunza huko Tabora,
Koboko ni moja ya nyoka wenye sumu kali sana
Kwa Tabora, koboko atakuuwa kama umechelewa sana kwa mtaalamu...

Tena huwa wanaangalia nywele, koboko akikuuma baada ya mda flani ukivutwa nywele huwa zinang'oka...

Ikifika hali hiyo, inakua ngumu kukutibu...

Japo hao wazee wanakufaga na utaalamu wao.
 
Tujihadhari na nyoka wenye sumu kali ni hatari kwa maisha na uhai wa kila mwanadamu,

hata hivyo,
ni muhimu sana kuipa kipaumbele Afya yako kuliko iphone unayomiliki.
Ni jambo la maana sana kila familia kua na bima ya afya kuepuka fedheha linapokuja suala la kuugua na wakati huo uko tee, hauna jambo lolote mfukoni, lakini una iphone ya milioni 4 lakini huna bima ya lakini moja.

hakuna haja ya kuona fahari kuripoti msiba. Ni muhimu kila mdau kua na bima ya afya .

R.I.P Juliana
Kwa hiyo huyo juliana alijuwa na i phone ya milioni nne mfukoni mwake? Huku akisumbuka vichakani kuokoteza vimboga vya kuilisha familia yake? Kweli ma ccm mna roho mbaya kuliko shetani,ila siku yenu yaja, mtakufa kwa uchungu mkuu, tunaomba mkono wa Mungu uwaguse ili mjutie ukatili wenu, Amen
 
Hospital ukiwa na huruma unaweza jikuta unatumia mshahara wako
Sio kweli hospital ngapi za Rufaa watu ambao hawana uwezo wanatibiwa bure kupitia kitengo cha social, je huduma za hospital za rufaa ni sawa na za vituo vya afya , hawa vijana wanaopewa endesha au simamia vituo wapuuzi tu, hata uongonzi hayajui, afya tz imeanza leo katika vituo vya umma?
 
Aya matukio ni mengi hawa vijana wana lilia ajira wakipata wanakua wangese sana uko kazini wana sahau kila kitu
Kuna watu wanaitwa maboss huko maofisini, Hawa ndio chanzo Cha uharibifu, vikao vyao na watumishi ni vitisho, kuvishana hofu na kutetemeshana, hili linasababisha watumishi wa chini kutokutumia akili na utu sababu mda mwingi Wana hofu
 
Wasanii wanatibiwa bure Jakaya Kikwete HI,Wakuu Mikoa,Wikaya ,wakurugenzi ,nk wanatembrlea magari ya Mil250+ ;Wananchi wanaichagua CCM kwa Asilimia 99😒😒🥴
😂😂😂 Mbavu zanguuuuuu😂😂😂😂😂
 
Huyo mganga mfawidhi hajitambui na ni mjinga kabisa.Ka kwepa kumsaidia mwananchi Kwa kumsukumizia awaombe wakati mwenye kutoa ruhusa ni yeye.Hawa watumishi wa Samia sijui anawaokota wapi?
 
Kwa hiyo huyo juliana alijuwa na i phone ya milioni nne mfukoni mwake? Huku akisumbuka vichakani kuokoteza vimboga vya kuilisha familia yake? Kweli ma ccm mna roho mbaya kuliko shetani,ila siku yenu yaja, mtakufa kwa uchungu mkuu, tunaomba mkono wa Mungu uwaguse ili mjutie ukatili wenu, Amen
Gentleman,
kifo cha mwendazake Juliana,
kiwe funzo na changamoto kwa kila mdau wa JF, hususani kuanzia mwaka mpya 2025, kuweka kipaumbele cha kua na Bima ya afya.

kulalamika au kulaumu hakusaidii chochote. Ni muhimu kugeuza changamoto kua fursa ya kujipanga na kuhakikisha una bima ya afya wewe na familia yako.

Epuka unafiki wa kujifanya una uchungu na mtu ambae tayari ameaga dunia na huna namna ya kumrejeshea uhai.

Bimba ya afya ni sehemu ya nusura ya maisha na uhai wako. Hakikisha una Bima ya afya na sio kumbwelambwela tu 🐒 🐒
 
Back
Top Bottom