Aliyeolewa akaachika miaka 7 sasa imepita ila hakupewa talaka, Anataka nimuoe. Je, naweza kumuoa?

Asante
 
Kiufupi hapo linatakiwa tamko tu la mwanaume wa mwanzo atoe talaka basi,
Ao mwanamke afanye khulus(ajivue ndoa irejeshwe mahari yake ndoa iishe,
Kama mwanaume atakataa basi nendeni kwa kadhi ataivunja ndoa hiyo....!
Ila hapo kumuoa huwezi maana bado mke wa mtu hata akae miaka 15 jamaa akirudi akihitaji mke wake huna ujanja
 
Ndoa ya kiislamu haivunjika kwa mwanaume kua mbali na mke wake miaka mingi na kisheria huyo mwanamke anamakosa yakuzini akiwa mke wa mtu...alichotakiwa kama alikua anaona hana mapenzi tena na huyo mwanaume basi awataarifu familia washenga au aliemuozesha kwakudai talaka na kama mwanaume hajaweza kutoa talaka basi aliruhusiwa kujivua kwakumrudishia mwanaume mahali yake na mwanamke kujivua eda yake ni mwezi mmoja baada hapo angeweza kuolewa tena.....lkn kwa kosa lililotendeka anaweza kurudi nyuma kwakurudi kwao na fanye toba ya zinaa kama alifanya kwakujua au kutokujua alf aendee na process zakujivua kwakuwafata hao niliowasema kwakudai talaka yake na kama hajatoa basi atajivua na kukaa eda ya mwezi ikiisha basi anaweza kuolewa tena na kama huyo mume akitoa talaka kwa hiyari basi eda ni miezi mi3 na baada ya hapo anakua yupo huru kuolewa tena
 
Punguza chuki na ujuaji ye alieishi nae miaka mitatu hajaona uzee wake we fasta umeuona khaaa wanaume wa jf punguzeni kiherehere
 
Mtoa mada ni mdogo kuliko huyo mwanamke anayetaka kumuoa still yuko kwenye mid 20's ndio maana nashangaa sana!
Cha kushangaza kipi hapo mpe ushauri kutokana na alichoomba haya mengine kama ya umri sidhani kama ni muhimu kwetu kama ye muhusika yuko poa nalo
 
Acha ushirikina, kwani anamwngilia kwenye mvi.
 
Akalete cheti cha talaka hakuna jingine
 
Naishi naye huu mwaka wa 3 bila ya ndoa.

" Anataka nimuoe kwaajili ya hii ramadhan .na nimeishi nae mwaka wa 3 sasa kama mke na mume

Karibuni

Kwahiyo Ramadhani zilizopita hazikuwa nzuri
 
Wengi wameniambia kuhusu taraka
Mimi
" Nimemwambia uyu mwanamke adai taraka
Akampigia mam mkwe wake ambae mama wa mme wake wa kipindi hicho akasema kwamba kwa sasa jamaa yupo jela maana madawa yamempanda na amepelekwa mahabusu yapata week sasa kwa kosa la kumshikia kisu mama yake mzazi
Yeye
Akawapigia tena familia yake uyu mwanamke kwao wanasema mwambie shem aje aoe tu.

Apo kitaaalamu imeekaaje
Pia nimezaa nae uyu mwanamke mtoto mmoja na kipindi na zaa nae bado alikuwa anaakaa kwako .
 
mbona huyo mkeo? mnamuoaje mkeo? miaka 3, ramadhani hii ndo Nini vile? mkeo huyooo bhana
 
Unataka kusema mpka Sasa huyo mwanamke Ana miaka 35??
 
Punguza chuki na ujuaji ye alieishi nae miaka mitatu hajaona uzee wake we fasta umeuona khaaa wanaume wa jf punguzeni kiherehere
Wanaume wa humu wengi wana wivu sana na wanawake nadhani wanatamani wangeumbwa wanawake ila ndo hivyo
 
Alafu pia hakujua kama jamaa anauliza ushauri wa namna gani, yeye alitaka kujua kisheria inakuwaje kama hawajapeana talaka na mumewe wa kwanza, na pia huyo ni kijana mdooogo kabisa anaamini ndoa ni za mabinti na vijana wadogo
 
Alafu pia hakujua kama jamaa anauliza ushauri wa namna gani, yeye alitaka kujua kisheria inakuwaje kama hawajapeana talaka na mumewe wa kwanza, na pia huyo ni kijana mdooogo kabisa anaamini ndoa ni za mabinti na vijana wadogo
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Hapo mwisho nimecheka sana. Bwana mdogo anaamini ndoa ni za vijana wadogo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…