Uko sahihi mkuu. Akimuoa wakati ndoa ya awali haijafa basi ndoa yao mpya haitakuwa halali Kisheria.
Cha kufanya, mwanamke apeleke Mahakamani ombi la talaka. Lkn ombi la talaka haliwezi kusikilizwa Mahakamani bila mwanamke kuwa na hati ya Usuluhishi ya maswala ya ndoa kutoka kwenye mabaraza ya usuluhishi yaliyopo misikitini (bakwata), makanisani au kwenye kila kata. Haya mabaraza yatajaribu kuwasuluhisha, ikishindikana, itaandaliwa hati ambayo itaambatanishwa na maombi ya talaka yatakayopelekwa Mahakamani.
Hati ya usuluhishi halitakuwa takwa la lazima kama mwanaume atakataa kwenda kwenye hilo Baraza.
Moja ya sababu ambayo Mahakama itaizingatia kabla ya talaka kutolewa ni wanandoa kutengana kwa zaidi ya miaka mitatu. Mtoa mada anasema huyo mwanamke wake katengana na mume wake kwa miaka 7; so sababu ya msingi ipo.
Apeleke kesi Mahakama ya mwanzo au ya wilaya. Mahakama ikiamua kwamba waachanishwe ndiyo jamaa anaweza kufunga ndoa mpya halali ambayo itatambulika kisheria.
Kwa sasa ni hayo tu, namtakia kila la kheri.