Pre GE2025 Aliyepinga Rais Samia kupitishwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM afukuzwa uanachama

Pre GE2025 Aliyepinga Rais Samia kupitishwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM afukuzwa uanachama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM wanaweka kumbukumbu mbaya. Wao wanatakiwa wawe mfano wa vyama vingine. Hii inaleta picha ya kwamba mwanachama haruhusiwi kutoa maoni. Ni wazi katiba ya chama imepindwa, huyu wangemuacha tu, sijui nani katoa wazo la afukuzwe
Ni haki yake kuuliza, imekuwaje? Au ni hofu kuwa atawaamsha waliolala?
Vya
 
Ila hawa sisiem ni wahuni sana,
mtu anafukuzwa uanachama kwa kosa la kukiuka katiba kwa kuwa alihoji kwanin katiba imekiukwa 😅
 
Kwa ninavyowajua CCM na dola walivyo na nongwa hapo hawajamalizana naye, lazima watampeleka kaburini tu, tukifanya rejea ya kilichomkuta yule dogo Chaula aliyechoma picha ya Samia, mahakama ilimtia hatiani na akahukumiwa kifungo au faini, wasamaria wema wakamchangia faini akawa huru lakini hawakuridhika wakamteka na kumpoteza hadi leo maiti yake haijaonekana.
Kwani wao hawatakufa , tusiogopeshane ujinga , kila apumuaye apa duniani siku yake ilisha andikwa tu, asema Bwana , shida ni lini ,wakati gani ,kwa mazingira gani.

Bwana asipo ulinda mji wake ................????? asema Bwana
 
Ccm hakuna demokrasia hata kidogo ! Pale kuna ndioooo hakuna hapanaa!!!
 
Narudia tena, maumivu yako nayaelewa. Sina tatizo na jazba zako, ila kila chenye mwanzo kina mwisho. Mwisho wa Mbowe kuwa mwenyekiti ulifika.
Pole sana unaonekana bado una mentality Za kitoto tena Za kishenzi
 
Kwani wao hawatakufa , tusiogopeshane ujinga , kila apumuaye apa duniani siku yake ilisha andikwa tu, asema Bwana , shida ni lini ,wakati gani ,kwa mazingira gani.

Bwana asipo ulinda mji wake ................????? asema Bwana
Siyo tunaogopeshana ujinga, hawa watu ni wauaji kweli sasa tunapoyasema au kuandika tunawa preempt ikiwa ni defensive mechanism.
 
Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.
Hii tu inatosha kuelezea yeye ni mtu wa aina gani. Ndani ya miaka 4 ya uanachama unagombea vyeo vyote hivyo kwa mantiki ipi ?!
Anyway, atajiunga chadema.
 
Siyo tunaogopeshana ujinga, hawa watu ni wauaji kweli sasa tunapoyasema au kuandika tunawa preempt ikiwa ni defensive mechanism.
Nakuelewa mkuu wangu, hata binafsi nimeandika kwa kuwalenga wao , kwamba wasitutishe na kifo , leo tz nzima ipo na makaburi mangapi mpaka tishika, na wao watakufa wapende au wasipende.
Sorry mkuu kama hukunielewa vizuri.
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, kimemfukuza uanachama kada wa chama hicho Mchungaji Godfrey Malisa kuanzia leo Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya Chama hicho.

Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.

Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 10, 2025 Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa.

Mwananchi ilipomtafuta Dk Malisa kuhusiana na uamuzi huo, amesema kuwa hakupewa taarifa wala kushirikishwa.

Pia soma: Pre GE2025 - Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Katiba ya ccm inanguvu kwa atakaye pinga uhuni wa kujipitisha ila aliye jipitisha kabla hata ya kuchukua fomu na kupata ushindan hapo sheria huwa haitumiki
 
Back
Top Bottom