Pre GE2025 Aliyepinga Rais Samia kupitishwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM afukuzwa uanachama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, kimemfukuza uanachama kada wa chama hicho Mchungaji Godfrey Malisa kuanzia leo Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya Chama hicho.

Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.

Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 10, 2025 Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa.

Mwananchi ilipomtafuta Dk Malisa kuhusiana na uamuzi huo, amesema kuwa hakupewa taarifa wala kushirikishwa.

Pia soma: Pre GE2025 - Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Kama viongozi wenyewe wa Mkoa ninaona hii , basi, cham kitabaki na wale wa upande wa maoni ya upande moja , mambo maoni ya Mpina , au ya Tibaijuka na wengineo, yatakuwa kukiuka maadili na kuvunja Katiba
 
Kwa kuwa ni Mchungaji huenda akaitwa immigration kuhojiwa uraia wake!
 
Hao viroboto wa mama Kilimanjaro mnaaibisha.
 
Nimecheka kwa nguvu vibaya sana. CCM demokrasia kwao ni jambo wanalazimisha, na hakuna kitu kimewauma kama uchaguzi wa kidemokrasia ya kweli ya uchaguzi wa CHADEMA juzi. Na huyo mwanachama ajiandae kuhujumiwa shughuli yake ya kumuingizia kipato.
Marekani demokrasia haigmfuati ifuate ccm tanzania hiyo ni misamiati tu kama kiumbe mzito kwenye kanga
 
Mkutano mkuu wa CCM una mamlaka ya kuamua juu ya mgombea Urais wao!! Harakati Za kitoto zinatia aibu!
Utaratibu ulifuatwa?? Walichofanyiwa Mkutano Mkuu ni kuletewa majina ya Wagombea. Na aliyeyaleta nae Mgombea pekee. Na mwenye Mamlaka na isitoshe yuko Madarakani. Kwanini hata ule ushauri wa Job Lusinde haukufanyiwa kazi??

Siyo kama Wajumbe hawakuwa na lakuzungumza la hasha. Walijawa na hofu kwani hakuna asiyefahamu CCM ilivyo kwa sasa.

M/Kiti wa CCM Taifa anapoingia kwenye Kikao cha Chama, haishii tu kuwa kiongozi wa chama bali Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Kwa namna nyingine atakushughulikia kwenye chama na hata Serikalini pia. Nani angethubutu kunyayua pua yake pale?? Ukipingana na Mwenyekiti umepingana na Rais/Serikali. Je utabaki salama??
 
Mkutano mkuu wa CCM una mamlaka ya kuamua juu ya mgombea Urais wao!! Harakati Za kitoto zinatia aibu!
Mkutano Mkuu wa CCM uliamua kutoka kwenye agenda ya kikao Gani?
Kwa maelezo Yako, Mkutano Mkuu walikuja na agenda ndani ya mkutano mkuu,ambapo ni kinyume na katiba ya CCM!
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, kimemfukuza uanachama kada wa chama hicho Mchungaji Godfrey Malisa kuanzia leo Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya Chama hicho.

Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.

Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 10, 2025 Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa.

Mwananchi ilipomtafuta Dk Malisa kuhusiana na uamuzi huo, amesema kuwa hakupewa taarifa wala kushirikishwa.

Pia soma: Pre GE2025 - Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Huyu Dr. Godfrey Malisa ni chizi Wala huijui Katiba ya Nchi Wala ya CCM!!
 
Mkutano Mkuu wa CCM uliamua kutoka kwenye agenda ya kikao Gani?
Kwa maelezo Yako, Mkutano Mkuu walikuja na agenda ndani ya mkutano mkuu,ambapo ni kinyume na katiba ya CCM!
Agenda ya Adam Kimbisa!! Au hujui mjumbe yeyoye wa mkutano mkuu anao uwezo wa kuleta ajenda mbele ya mkutano mkuu na ukaridhia ama kuikataa ajenda husika kama ambavyo mbunge anaweza leta hoja bungeni?

Wabongo mnajifanyaga wajuaji kwenye mambo msiyoyajua ama kuyaelewa!!
 
Kama viongozi wenyewe wa Mkoa ninaona hii , basi, cham kitabaki na wale wa upande wa maoni ya upande moja , mambo maoni ya Mpina , au ya Tibaijuka na wengineo, yatakuwa kukiuka maadili na kuvunja Katiba
Michawa ya Mother inaharibu Chama
 
Wangemjibu kwa vipengele vya Katiba pekee wangepungukiwa nini?
Wangeumbuka zaidi. Kwani sidhani kama Mkutano Mkuu upo juu ya Katiba ya Chama chao. Ni vyema yangefanyika kwanza mabadiliko ya Katiba ndipo style hiyo ingefanyika. Jamaa kaenda mbali zaidi na kuwatuhumu kuwa wamevunja Katiba ya JMT.
JK alitoa angalizo kuwa wakaangalia kama mchakato ule upo ndani ya sheria na kanuni!
 
Back
Top Bottom