Kwa mara kwanza Tanzania imekua ranked ya pili Tanzania kwa matumizi sahihi ya teknolojia serikalini.
Nimeona hii taarifa kwenye gazeti la The Citizen la leo, nikaona waziri wa TEHAMA Nape naye amezisoma taarifa hizi kwa Rank ya kidunia Tanzania ipo GROUP A ambalo lina nchi kama GERMANY, FRANCE na wengine wengi.
Uanzishwaji wa malipo ambayo ni centralized (matumizi ya Control number), utumiaji wa mifumo ambayo imetengenezwa na serikali yenyewe kupitia taasisi ya EGA, umechochea mabadiriko makubwa sana ya TEHAMA serikalini.
Kwa sasa taasisi nyingi za serikali zinatumia mifumo ya kidigitali kutekeleza majukumu yake.
EGA imeanza toka awamu ya nne chini ya Rais Mstaafu Kikwete apewe maua yake. Mkurugenzi wa kwanza ambaye kama sikosei alihamishwa Miaka kama mitatu toka sasa alikua anaitwa Dr JABIRI KUWE apewe maua yake.
Serikali ya awamu ya Tano iliendeleza wazo la serikali ya awamu nne , na sasa SERIKALI ya mama Samia imeipa nguvu zaidi taaisi hii ambayo sasa imewezesha nchi yetu kuwa ya pili Afrika kwa matumizi ya TEHAMA si TEHAMA tu bali TEHAMA ambayo iko matured.
WORLD BANK wametupa maua yetu watanzania. KONGOLE EGA (E-GOVERNMENT), Dr JABIRI KUWE, Dr KIKWETE, Dr Samia Suluhu mna nafasi yenu peponi.
Mmeliheshimisha taifa, vijana wazalendo na wapambanaji waliopo taasisi ya EGA pokeeni maua yenu, endeleeni kuilinda nchi yetu kidigitali.
Yalikua maono sahihi kuanzisha taasisi hii inayoratibu matumizi ya TEHAMA Serikalini.
View attachment 2620688