Aliyerekodi tukio jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) apewe maua yake

Aliyerekodi tukio jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) apewe maua yake

Aliyerekodi atakuwa mmoja wao, na kama kawaida yao wakairusha Kama wale walionfanyia unyama yule binti.
 
Niaminivyo kuna maeneo ukiitwa usiende mwenyewe tafta back-up ambayo haitajulikana
Anaweza tangulia uendapo ama akaja baadae ..... msiongozaneee hahaaaaaa

Kuna mikoa wenza wakienda mahali .... mmoja anatangulia mwingine anakuja baadaeee

Hakun
 
hakuna mtekaji miongoni mwao hao, labda ni kundi la kulipwa kwenda kulipa kisasa huko uswahilini, huenda muungwana dhulumati mwenye madharau, jeuri mwenye dhihaka za kibabe kwenye biashara au familia za wengine mtaani, na ndiyo maana watu wengine wakawa nanashangaa tu kama nyumbu anavyotafunwa na simba wenzie wakishangaa tu..

ubabe sio dili nje ya eneo lako la kujidai. Ishi na watu vizuri 🐒
Pingu walizitoa wapi?
 
Ni dhahiri pia kuwa, watekaji ni waoga sana,

Na soon wananchi watatumia chance hivyo vyema,

Watekaji wamekimbia na kuacha pingu,

Ndugu huyu atumie hizo pingu kuwalocate Kwa finger print zao.
Wapi atakwenda kuwanya vipimo vya fingerprint?
Hivi wewe unaijua Tongonyika wewe?
Vipi yule wa kumtolea nape bastola ambaye alijulikana mpaka nyumba anayoishi mwisho wake ulikuwa vipi?
 
hakuna mtekaji miongoni mwao hao, labda ni kundi la kulipwa kwenda kulipa kisasa huko uswahilini, huenda muungwana dhulumati mwenye madharau, jeuri mwenye dhihaka za kibabe kwenye biashara au familia za wengine mtaani, na ndiyo maana watu wengine wakawa nanashangaa tu kama nyumbu anavyotafunwa na simba wenzie wakishangaa tu..

ubabe sio dili nje ya eneo lako la kujidai. Ishi na watu vizuri 🐒
Ni wenzako hao vilaza wa kutekateka watu au nawe ni kundi hilohilo? Umetoa conclusion kana kwamba kuna kitu unafahamu kuhusu hao majuha ambacho wengi hatukifahamu, guts za hao mafala kutoa silaha na pingu hadharani wakijimbulisha kama polisi kwa sasa sisi wengine tutaendanayo hiyohiyo until proved otherwise.
Serikali nzima na apparatus zake ni genge la vibaka, watekaji na wauaji mpaka pale watakapowakamata hao wahuni na nchi ikaonyweshwa hatua zinazochukuliwa. Nakumbuka yule 'kibaka' aliyemtolea Nape bastola ndiyo walewale. Guts za kutoa silaha hadharani with people watching si jambo jepesi.
 
Salaam, Shalom!

Wakati umma wa watz ukilaumu watu waliokuwa wakiangalia tukio lile la ndugu bonge akijaribu kutekwa na wasiojulikana,wenye pingu na silaha za moto.

Kwa jicho la Umakini, yupo shujaa aliyetumia vizuri simu yake na kurekodi tukio Zima tena sauti zikisikika kabisa, hii Ina maana kuwa alikuwa karibu sana na tukio hili.

- Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Hii ni hatua kubwa huko tuendako maana ujasiri wa wenye Nchi kujilinda utaenda ukiongezeka.

Shujaa huyu hakuogopa KUPIGWA risasi na dreva aliyekuwa ndani ya gari, Abarikiwe huko aliko shujaa wetu.

Na Hadi hivi sasa wasiojulikana wamejulikana katika tukio lile Kwa picha na sura zao, na soon Majina Yao yatakuwa wazi maana wanatoka ndani ya JAMII zetu, tutajua ni Ushimen wa nani, na ni Jirani wa nani,

What comes around, goes around.

Mungu Mbariki mpiga picha.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Na walaaniwe Hawa waovu, na wote tuseme aamin!
What goes around comes around, kinachokuzunguka kina kuja karibu, (kwako)
 
Sasa kitambi ndio kilimuokoa deo bonge,

Angekuwa kimbaumbau, angeshasahaulika.
Usiwazarau sana Mbaumbau, kwenye hatari sense, na mashinary za mwili zote hufanya kazi.

Mwaka 2015 nilinusurika kutekwa kwenye mkoa ambao wala sikua na ili wala lile sina ungovi na mtu ,ila nafikili kibegi changu ndo kilitaka kuniponza wakati hapakua na cha maana nje ya vitu vyangu vidogo vidogo ambavyo vilifanya kibegi changu kutuna. au kwa sababu zingine maana ndo uchaguzi ulikua umepamba moto

Ilikua saa moja usiku, natoka kituo kimoja kwenda kituo kingine, sasa usafili wa njia ile zipo Hiece, ila ghafla nilipokua nimesima nasubiri hiece , ilikuja Noha moja na kuanza piga debe kwamba inaelekea njia ambapo nilikua naenda.

Binafsi nikaona isiwe shida nikapanda , siti ya mbele wakasema ipo na abiria nikaa sit ya kati , mda mfupi akaja bwana baunsa akaomba kaa upande wa dirisha, mara wakaja watatu ,mmoja akakaa siti ya nyuma ,mwingine pembeni yangu upande wa mlango, mwingine upande wa dereva ,then dereva akaingia , mlango ukafungwa gari ikatoka. Safari ikaanza,cha kushangaza story zao ni kama wanafamiana na wote wamejaza mili yao( mabaunsa).

Binafsi pale pale nikaanza kuhisi sipo sehem salama.

Ile njia mwanzo ipo na sehem zimechangamka ila mbele hua kuna kama shamba la minazi na mchanganyiko wa vichaka kama km moja ambapo barabara inapita mle, ila kabla ya kuanza icho kipori shamba mwanzo kabisa kuna kijiwe kemechangamka ,moyoni nikasema hawa pale ndo natakiwa nicheze mchezo wa kutoka kwenye imaya yao. Japo pale sikua nafamiana na mtu yoyote.

Basi bwana wakati tunaendelea na safari mmoja akawa ananiuliza vimaswali vya kizushi, mara bro unakaa wapi, unatokea wapi , huku uendako kuna ndugu ,so mimi nikawa nacheza na maswali yao vizuri tu huku moyoni najua what is my plan, tulipofika pale kwenye kile kijiwe kabla ya kuanza shamba pori , nikamwambia suka ,

Aisee Suka naomba kwanza niache kamzigo kangu haka nimsalimie dada kama dakika mbili nimpe ujumbe wake alafu twendelee ,suka asema poa , akasogeza gari mbele kidogo ambapo mwanga umefifia , na kusimama nikashuka na kuacha kwanza kibegi changu.

Nilivyoshuka tu moja kwa moja mpaka pale kwenye kijiwe ,pale wanachoma chips, kuku, mishikaki, nikajifanya nauliza bei ya vitu ,kule wanasubili.

Kama dakika tatu nikarudi pale nikawambia wale jamaa waliokaa nyuma kwamba naomba icho kibegi nimtolee dada mzigo wake ,wakanipa , pale nikachukua nauli yao na kuwapa ilikua elfu tatu , wakasema usijali si bado tunaendele na safari utalipa tu ,nikasema poa , nikachukua kibegi na kuludi kwenye chipsi ,nikaagiza chips na kuacha kibegi changu na kurudi ilipo ile gari lakini apo nimemwambia muuza chipsi kwamba ngoja niwalipe wale nauli yao nakuja.

Nikawafuata tena nikawambia aisee dada anasema naweza kulala kwake leo nyie endeleni na safari nauli yenu hii hapa , mjinga mmoja siti ya nyuma alisonya , ( wajinga mmealibu kazi) mimi nikarudi kwenye chipsi na kukaa , jamaa walikaa pale kama robo saa bila kuondoa gari , nilivyoona vile nikaagiza na soda mdogomdogo , mda kidogo ikaja Hiece ya abiria ikitokea nilipo kua naenda ikielekea nilipokua natoka nikaludi zangu wala sikuendelea na safari siku iyo. Nimefika nasimulia wenyeji wanasema barabara hiyo kama ni usiku usipande gari isiyo ya abiria kamwe.

Note inawezekana hata Mzee kibao(R.I.P) aliondoka kwenye basi bila vurugu akijua anaweza kuwa na plan B ila mijangili ikamlia timing
 
Pingu zinauzwa wapi wewe hayawani?
Huyo ni moja kati ya matahila hapa JF,Mimi nimimuignore kitambo, so nawashangaa mkiendelea kubishana nae.

Imagine Hapo sijasoma alichoandika maana sioni lakini ameandika utumbo tuu bila shaka
 

Attachments

  • IMG_5924.png
    IMG_5924.png
    144.2 KB · Views: 2
Hakika Mpiga Picha apewe Maua yake. Jamaa hatimaye wamejulikana
Hawa ndio wanaotumiwa kuteka na kuua, jamani Mungu waue woteeee mbwa hao, na waseme walikowapeleka vijana wetu yule wa mbeya na wale kina soka na wenzake. Na hawa ndio waliomteka na kumuua kada wa chadema kwenye basi, abiria waliokuwemo wajaribu kutambua sura hizi jaman
 
Msichokijua ni kwamba wasiojulikana na watekaji si Jeshi la Polisi kama mnavyo dhani bali ni kikundi ambacho kipo chini ya Chama cha mapinduzi (CCM) kikiratibiwa na Umoja wa vijana UVCCM.

Asante sana kwa hii taarifa.
 
Back
Top Bottom