Sasa kitambi ndio kilimuokoa deo bonge,
Angekuwa kimbaumbau, angeshasahaulika.
Usiwazarau sana Mbaumbau, kwenye hatari sense, na mashinary za mwili zote hufanya kazi.
Mwaka 2015 nilinusurika kutekwa kwenye mkoa ambao wala sikua na ili wala lile sina ungovi na mtu ,ila nafikili kibegi changu ndo kilitaka kuniponza wakati hapakua na cha maana nje ya vitu vyangu vidogo vidogo ambavyo vilifanya kibegi changu kutuna. au kwa sababu zingine maana ndo uchaguzi ulikua umepamba moto
Ilikua saa moja usiku, natoka kituo kimoja kwenda kituo kingine, sasa usafili wa njia ile zipo Hiece, ila ghafla nilipokua nimesima nasubiri hiece , ilikuja Noha moja na kuanza piga debe kwamba inaelekea njia ambapo nilikua naenda.
Binafsi nikaona isiwe shida nikapanda , siti ya mbele wakasema ipo na abiria nikaa sit ya kati , mda mfupi akaja bwana baunsa akaomba kaa upande wa dirisha, mara wakaja watatu ,mmoja akakaa siti ya nyuma ,mwingine pembeni yangu upande wa mlango, mwingine upande wa dereva ,then dereva akaingia , mlango ukafungwa gari ikatoka. Safari ikaanza,cha kushangaza story zao ni kama wanafamiana na wote wamejaza mili yao( mabaunsa).
Binafsi pale pale nikaanza kuhisi sipo sehem salama.
Ile njia mwanzo ipo na sehem zimechangamka ila mbele hua kuna kama shamba la minazi na mchanganyiko wa vichaka kama km moja ambapo barabara inapita mle, ila kabla ya kuanza icho kipori shamba mwanzo kabisa kuna kijiwe kemechangamka ,moyoni nikasema hawa pale ndo natakiwa nicheze mchezo wa kutoka kwenye imaya yao. Japo pale sikua nafamiana na mtu yoyote.
Basi bwana wakati tunaendelea na safari mmoja akawa ananiuliza vimaswali vya kizushi, mara bro unakaa wapi, unatokea wapi , huku uendako kuna ndugu ,so mimi nikawa nacheza na maswali yao vizuri tu huku moyoni najua what is my plan, tulipofika pale kwenye kile kijiwe kabla ya kuanza shamba pori , nikamwambia suka ,
Aisee Suka naomba kwanza niache kamzigo kangu haka nimsalimie dada kama dakika mbili nimpe ujumbe wake alafu twendelee ,suka asema poa , akasogeza gari mbele kidogo ambapo mwanga umefifia , na kusimama nikashuka na kuacha kwanza kibegi changu.
Nilivyoshuka tu moja kwa moja mpaka pale kwenye kijiwe ,pale wanachoma chips, kuku, mishikaki, nikajifanya nauliza bei ya vitu ,kule wanasubili.
Kama dakika tatu nikarudi pale nikawambia wale jamaa waliokaa nyuma kwamba naomba icho kibegi nimtolee dada mzigo wake ,wakanipa , pale nikachukua nauli yao na kuwapa ilikua elfu tatu , wakasema usijali si bado tunaendele na safari utalipa tu ,nikasema poa , nikachukua kibegi na kuludi kwenye chipsi ,nikaagiza chips na kuacha kibegi changu na kurudi ilipo ile gari lakini apo nimemwambia muuza chipsi kwamba ngoja niwalipe wale nauli yao nakuja.
Nikawafuata tena nikawambia aisee dada anasema naweza kulala kwake leo nyie endeleni na safari nauli yenu hii hapa , mjinga mmoja siti ya nyuma alisonya , ( wajinga mmealibu kazi) mimi nikarudi kwenye chipsi na kukaa , jamaa walikaa pale kama robo saa bila kuondoa gari , nilivyoona vile nikaagiza na soda mdogomdogo , mda kidogo ikaja Hiece ya abiria ikitokea nilipo kua naenda ikielekea nilipokua natoka nikaludi zangu wala sikuendelea na safari siku iyo. Nimefika nasimulia wenyeji wanasema barabara hiyo kama ni usiku usipande gari isiyo ya abiria kamwe.
Note inawezekana hata Mzee kibao(R.I.P) aliondoka kwenye basi bila vurugu akijua anaweza kuwa na plan B ila mijangili ikamlia timing