Aliyetekwa akutwa ameuawa na kuzikwa nyumbani kwa mtu Tabora

Aliyetekwa akutwa ameuawa na kuzikwa nyumbani kwa mtu Tabora

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mtu mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Castory Madembwe ambaye alikuwa anatafutwa kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu kupatikana kwa taarifa zake kwamba ametekwa,hatimaye leo Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Mpera wamefanikiwa kuupata mwili wa mtu huyo ukiwa umezikwa nyumbani kwa mtu kisha juu ya shimo alilofukiwa kutengenezwa bustani ya nyanya kama sehemu ya kupoteza ushahidi wa mauaji hayo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Uledi Kata ya Mpera Manispaa ya Tabora John Peter amethibitisha tukio hilo la kufukuliwa kwa mwili wa mtu huyo ambaye alitafutwa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi baada ya kumkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo walifanya mahojiano nae ambapo akaeleza alimteka marehemu Castory Madembwe na baadaye akamuua na kisha akaufukia mwili wake kwenye eneo la nyumbani anakoishi mtuhumiwa mtaa wa Uledi kata ya Mpera.

Hata hivyo hadi Polisi wanamaliza tukio la kuufukua mwili wa mtu huyo hakuna ndugu wa marehemu aliyekuwa na taarifa kama ndugu yao amepatikana akiwa maiti.

 
Waje wale wanowasingizia polisi kwenye kila utekaji
Yea, si kila mtu..

20250708_183423.jpg
 
Mwenye hilo eneo ndio muhusika ?
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Back
Top Bottom