Aliyetekwa akutwa ameuawa na kuzikwa nyumbani kwa mtu Tabora

Maigizo tu ngoja tufatilie kesi ya huyo mtu,
Polisi wanajua kutengeneza ya kijingajinga kama hayo .
Hakuna cha mtu kutolewa sadaka wala nini .
Hayo ni maigizo ya Polisi .
Wajinga sana hao jamaa
kwa hiyo polisi walimteka,wakamuua,wakamfukia na kulima bustani ya nyanya kisha wakawa wanamwagilia?

Jeshi la polisi ni jeshi makini na lenye weledi mkubwa,haliwezi kufanya unyama huo,tuiache sheria ichukue mkondo wake kwa watuhumiwa.
 
Mtu mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Castory Madembwe ambaye alikuwa anatafutwa kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu kupatikana kwa taarifa zake kwamba ametekwa,hatimaye leo Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Mpera wamefanikiwa kuupata mwili wa mtu huyo ukiwa umezikwa nyumbani kwa mtu kisha juu ya shimo alilofukiwa kutengenezwa bustani ya nyanya kama sehemu ya kupoteza ushahidi wa mauaji hayo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Uledi Kata ya Mpera Manispaa ya Tabora John Peter amethibitisha tukio hilo la kufukuliwa kwa mwili wa mtu huyo ambaye alitafutwa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi baada ya kumkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo walifanya mahojiano nae ambapo akaeleza alimteka marehemu Castory Madembwe na baadaye akamuua na kisha akaufukia mwili wake kwenye eneo la nyumbani anakoishi mtuhumiwa mtaa wa Uledi kata ya Mpera.

Hata hivyo hadi Polisi wanamaliza tukio la kuufukua mwili wa mtu huyo hakuna ndugu wa marehemu aliyekuwa na taarifa kama ndugu yao amepatikana akiwa maiti.

Hizi ni sinema za jeshi la Polisi kujisafisha
 
kwa hiyo polisi walimteka,wakamuua,wakamfukia na kulima bustani ya nyanya kisha wakawa wanamwagilia?

Jeshi la polisi ni jeshi makini na lenye weledi mkubwa,haliwezi kufanya unyama huo,tuiache sheria ichukue mkondo wake kwa watuhumiwa.
Labda
 
Mtu mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Castory Madembwe ambaye alikuwa anatafutwa kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu kupatikana kwa taarifa zake kwamba ametekwa,hatimaye leo Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Mpera wamefanikiwa kuupata mwili wa mtu huyo ukiwa umezikwa nyumbani kwa mtu kisha juu ya shimo alilofukiwa kutengenezwa bustani ya nyanya kama sehemu ya kupoteza ushahidi wa mauaji hayo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Uledi Kata ya Mpera Manispaa ya Tabora John Peter amethibitisha tukio hilo la kufukuliwa kwa mwili wa mtu huyo ambaye alitafutwa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi baada ya kumkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo walifanya mahojiano nae ambapo akaeleza alimteka marehemu Castory Madembwe na baadaye akamuua na kisha akaufukia mwili wake kwenye eneo la nyumbani anakoishi mtuhumiwa mtaa wa Uledi kata ya Mpera.

Hata hivyo hadi Polisi wanamaliza tukio la kuufukua mwili wa mtu huyo hakuna ndugu wa marehemu aliyekuwa na taarifa kama ndugu yao amepatikana akiwa maiti.

Ukiua Mtu Dama yake huwezi kujificha hata kama hakuna aliyekuona wakati unatekelez tukio.

Sasa jamaa aliyemuua mbona amefichwa jina?
 
Waje wale wanowasingizia polisi kwenye kila utekaji
Hapa mzee hakuna kitu....Mwene shamba ametahwa jin? Mpaka muda huu taarifa imesema ameshikiliwa? Je amelala selo na Jtatu kesi itafunguliwa?
 
Ni sawa na yule aliyemchoma mkewe na mkaa.

Ukiwaza sana unaweza kusema ni uongo
 
Mnaolisingizia jeshi la polisi kuwa linahusika,kwani malehemu alikuwa na cheo gani mpaka wamfanyie unyama huo!
 
Marehemu kwenye kesi hiyo atatetewa na nani!
Kesi ya KIFO/MAUTI Mlalamikaji wa kwanza ni JAMUHURI/SERIKALI.

Mzazi/Ndugu/Mke/Mume/Watoto nyie mnabaki kama SHAHIDI mwenye kesi yake hapo ni SERIKALI

HUsikiagi unaambiwa wewe ni MALI YA JAMUHURI, ndio hapa sasa.
 
Bado sijapata majibu sahihi maana maswali bado yapo mengi..
Muuaji ni nani,
Wazee wa kazi wamepata taarifa kutoka kwa nani kumjua muuaji..
Mpaka sasa wamekamatwa watu wangapi kwenye huo ukatili maana ni ngumu mtu mmoja kufanya ukatili huo kwa mwanaume lazima walikua wengi..
 
Back
Top Bottom