Aliyetekwa akutwa ameuawa na kuzikwa nyumbani kwa mtu Tabora

Mtu mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Castory Madembwe ambaye alikuwa anatafutwa kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu kupatikana kwa taarifa zake kwamba ametekwa,hatimaye leo Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Mpera wamefanikiwa kuupata mwili wa mtu huyo ukiwa umezikwa nyumbani kwa mtu kisha juu ya shimo alilofukiwa kutengenezwa bustani ya nyanya kama sehemu ya kupoteza ushahidi wa mauaji hayo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Uledi Kata ya Mpera Manispaa ya Tabora John Peter amethibitisha tukio hilo la kufukuliwa kwa mwili wa mtu huyo ambaye alitafutwa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi baada ya kumkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo walifanya mahojiano nae ambapo akaeleza alimteka marehemu Castory Madembwe na baadaye akamuua na kisha akaufukia mwili wake kwenye eneo la nyumbani anakoishi mtuhumiwa mtaa wa Uledi kata ya Mpera.

Hata hivyo hadi Polisi wanamaliza tukio la kuufukua mwili wa mtu huyo hakuna ndugu wa marehemu aliyekuwa na taarifa kama ndugu yao amepatikana akiwa maiti.

Kiukweli video tu imenisisimua mwili mambo ya DUNIA yanatisha kama mnyama Ivo duuh
 
R.I.P mdogo wangu.
Binadamu ni zaidi ya mnyama.
Kisa milioni 50 sijui 60 ya ransom ndio wakupoteze?
Moyo unaumia sana tena sana
Screenshot_20250710-234252.jpg
 
Nawaza tu walichomfanya kwenye chumba cha mahojiano hadi akasema ukweli. Chamzo nini?
 
Mtu mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Castory Madembwe ambaye alikuwa anatafutwa kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu kupatikana kwa taarifa zake kwamba ametekwa,hatimaye leo Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Mpera wamefanikiwa kuupata mwili wa mtu huyo ukiwa umezikwa nyumbani kwa mtu kisha juu ya shimo alilofukiwa kutengenezwa bustani ya nyanya kama sehemu ya kupoteza ushahidi wa mauaji hayo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Uledi Kata ya Mpera Manispaa ya Tabora John Peter amethibitisha tukio hilo la kufukuliwa kwa mwili wa mtu huyo ambaye alitafutwa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi baada ya kumkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo walifanya mahojiano nae ambapo akaeleza alimteka marehemu Castory Madembwe na baadaye akamuua na kisha akaufukia mwili wake kwenye eneo la nyumbani anakoishi mtuhumiwa mtaa wa Uledi kata ya Mpera.

Hata hivyo hadi Polisi wanamaliza tukio la kuufukua mwili wa mtu huyo hakuna ndugu wa marehemu aliyekuwa na taarifa kama ndugu yao amepatikana akiwa maiti.

Je, huyo aliyeua alikuwa ni kada wa CCM au? Tunapenda mtoe habari iliyokamilika jamani.
 
Huu utekaji Kwa 90% ni mabiff miongoni mwa jamii kwa jamii,hasa dhulma,hakuna kitu kinaumiza mioyo ya watu mpaka kuwafanya kuwa makatili wa kutisha kama kudhulumiwa jasho lako na mdhulumaji kujitapa humfanyi lolote!
 
Back
Top Bottom