Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Kwa Kisiri Sanawari katika wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, jioni hii ya 11/7/2024 umepatikana mwili wa mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 akiwa amefariki ndani.
Kwa mujibu wa taarifa ya mkewe imeeleza kwamba mume wake alikuwa anasumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu na juzi alikuwa ameenda kwenye maombi Dar lakini aliporudi akawa hajiskii vizuri mpaka pale mwanamke wake alipokuwa ametoka kwenda kwenye mihangaiko yake, akawa anampigia mume wake simu hapokei na akimtumia meseji hajibu.
Jambo hilo likamtia wasiwasi, akarudi nyumbani na kumkuta mume wake amelala chini huku akiwa ni wa baridi, tayari akiwa ameshafariki dunia.
Mke wake alisema mume alikuwa hajala siku tatu zote alizokuwa Dar mpaka aliporejea Arusha kwasababu vyakula vilikuwa shida kupatikana kutokana na wingi wa watu, na kutokana na mwanaume kuwa na vidonda vya tumbo hali haikuwa nzuri.