Aliyetoka kwenye mkesha wa Mwamposa Dar afia ndani

Aliyetoka kwenye mkesha wa Mwamposa Dar afia ndani

kwa kisiri sanawari katika wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, jioni hii ya 11/7/2024 umepatikana mwili wa mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 akiwa amefariki ndani.

Kwa mujibu wa taarifa ya mkewe imeeleza kwamba mume wake alikuwa anasumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu na juzi alikuwa ameenda kwenye maombi Dar lakini aliporudi akawa hajiskii vizuri mpaka pale mwanamke wake alipokuwa ametoka kwenda kwenye mihangaiko yake, akawa anampigia mume wake simu hapokei na akimtumia meseji hajibu.

Jambo hilo likamtia wasiwasi, akarudi nyumbani na kumkuta mume wake amelala chini huku akiwa ni wa baridi, tayari akiwa ameshafariki dunia.

Mke wake alisema mume alikuwa hajala siku tatu zote alizokuwa Dar mpaka aliporejea Arusha kwasababu vyakula vilikuwa shinda kupatikana kutokana na wingi wa watu, na kutokana na mwanaume kuwa na vidonda vya tumbo hali haikuwa nzuri.
View attachment 3040469
Uchawi mtupu pale hakuna Injili.
 
Nice job! You missed the joke.

Hint: Sarcasm
View attachment 3040595
... GREAT! 😅
1720801739513.png
... YOU CAN DO IT!
 
Mchungaji akiomba gari anachangiwa hela ya kununulia lakini muumini akiomba gari anafanyiwa maombi ili apate gari dah!
Maajabu (Kwa sauti ya mzee Likoma)
 
Huwa napata shida sana utasikia watoto wamekutwa msikitini katika mazingira yasiyo sahihi wakifundishwa elimu ya dini,
Dk Sulle na Pete zake plus pesa za majini,Mara Mzee wa Upako,kiboko ya wachawi ukigeuka kulia unakutana na Mwamposa ukigeuka kushoto unakutana na Nabii Tito na kanisa lake.
Ukiwatathmini maamuma /wafuasi utagundua wamechakwaza na umaskini pamoja na maradhi mbele yao kuna wahubiri wa hizo dini wakizidi kuwa matajiri.
Watanzania tunahitaji kujifunza zaidi kuhusu dini Kuna mahala viongozi wa dini zetu wanatupeleka chaka.
 
Kwa Kisiri Sanawari katika wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, jioni hii ya 11/7/2024 umepatikana mwili wa mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 akiwa amefariki ndani.

Kwa mujibu wa taarifa ya mkewe imeeleza kwamba mume wake alikuwa anasumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu na juzi alikuwa ameenda kwenye maombi Dar lakini aliporudi akawa hajiskii vizuri mpaka pale mwanamke wake alipokuwa ametoka kwenda kwenye mihangaiko yake, akawa anampigia mume wake simu hapokei na akimtumia meseji hajibu.

Jambo hilo likamtia wasiwasi, akarudi nyumbani na kumkuta mume wake amelala chini huku akiwa ni wa baridi, tayari akiwa ameshafariki dunia.

Mke wake alisema mume alikuwa hajala siku tatu zote alizokuwa Dar mpaka aliporejea Arusha kwasababu vyakula vilikuwa shida kupatikana kutokana na wingi wa watu, na kutokana na mwanaume kuwa na vidonda vya tumbo hali haikuwa nzuri.
View attachment 3040469
Dar haijawahi kuwa na uhaba vyakula isee waseme mengine..
 
Namna yako ya utoaji taarifa ina inafikirisha
1. Aliyetoka shambani afariki dunia
2. Aliyetoka kwenye sherehe afariki dunia
3. Aliyetoka sokoni afariki dunia

Kutoka sehemu fulani kuna uhusiano gan na kufa, au kuna sehemu ukitoka hutakiwi kufa?😆😆
 
Wajinga ndio waliwao
Sasa kafia nyumbani kwake Mwamposa anahusikaje? Kuwa mtu akienda kwa Mwamposa ataishi milele au ? Kuwa hata siku yake ya kufa aliyopangiwa na Mungu asife au?

Wewe ndie mjinga.Watu walienda kwa Yesu wakapona lakini leo hatunao duniani ulitaka kuwa sababu Yesu aliwaponya kuwa walitakiwa kuwa hai hadi leo wasife au?
 
Back
Top Bottom