KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Mkuu 'Hamatan', tafadhali tusivunjiane heshima. Hana sifa wala uwezo wa kunitumia mimi!!!! EeeenHeeee!Samia alisema hafoki ila anatumia kalamu.
Samia ananena kwa kalamu, na bila kupepesa anaonesha anavyozipinga kwa nguvu zote zilizokuwa sera za marehemu kuhusu uhusiano wa kimataifa, sera za uwekezaji na biashara, sifa za wanaostahili kushika ofisi mbalimbali, n.k. Ndani ya miaka 3 ijayo, wateule wa marehemu katika ofisi mbalimbali, itatakiwa kutumia kurunzi kuwaona. Kama wapo wenye uelewa japo mdogo, wajiandae kisaikolojia na kimikakati namna ya kuendesha maisha yao tofauti na nafasi walizo nazo sasa.
Lakini ninakuelewa unalonena. Ni katika mlengo huo huo anatumia hicho kifaa (sio mimi) kuendeleza maovu ya aliyempa zawadi ya utawala, kama hii kesi ya akina Mbowe. Lengo ni lile lile kuua upinzani ili akandamize kimya kimya.
Sasa nikuulize swali, binafsi ungependa yupi, yule anayepiga makelele na kutisha waziwazi, au anayenyemelea kimya kimya huku akikuzaba vibao?