Ni kweli Mkuu, Kenya juzi kati walikumbwa na baa la nzige sasa Masanja juzi karopoka mbele ya Wageni waalikwa akiwemo Rais wa Kenya. Ni vyema akachagua cha kuzungumza asilipukelipuke tu, na awe na mipaka na anayozungumza.Binafsi juzi nilikuwa uwanjani nilikwazika na kauli yake hiyo. Kingine alitamka baadhi ya watu mnasema Mama yaani Mh Rais anasafiri sana mnataka baba yenu ndio asafiri? kauli kama hizo mbele ya maelfu ya Watanzania waliokuwa uwanjani sioni kama zina afya. Masanja ajifunze kuwa na busara.