Niliwahi kuimiliki
Gari imara, body ngumu na zina nguvu si haba.
Nilikuwa najaza lita 2.5 daily - natembea kama km 15 hivi location Mbeya (kwenda kazini, misele michache na kurudi home)
Sevisi yake ya kila baada ya miezi minne
Kidumu cha lita 5 na kimoja cha lita 1 (TOTAL - Rubia S)kwajili ya Engine - 60,000
vidumu vya lita 1 (TOTAL - Fluid ii D)vinne kwajili ya gearbox - 60,000
Oil Filter - 10,000
Hela ya fundi - elf 15
Ukibanwa kuna muda unaipeleka garage baada ya miezi 6 sevisi itakuvumilia.
Nje ya sevisi Mambo ya kwenda garage ilikuwa mara chache sana, niliwahi tu kubadili shockup moja elf 60.
Breki zinakaa sana, nilikuwa nabadili breki baada ya miaka miwili, nadhani ni elf 55
Ila kama vipi vuta kabisa Toyota Carina Ti, zinafanana vitu vingi kama na wenzake kina corolla, sprinter, ila ndio inakubalika zaidi
credit: picha kutoka google