Aliyewahi kumiliki hili gari atuambie sifa yake

Aliyewahi kumiliki hili gari atuambie sifa yake

Safi, zote una maanisha Carina TI na SI au Carina TI na hiyo corona Premio?

Sent using Jamii Forums mobile app
Carina TI

Nilitokea kuupenda design yake, japo vingi vinafanana

1692132579860.png
 
kwa uchunguzi wangu usio na ushahidi ni kwamba, gari nyingi za saloon huwa zinawahi mapema sana kutoka kwenye peak.
kwa mfano
baloon, mark ii, chaser, mark ii grande, cresta, verosa, mark x, haya crown ndo huyo anaanza kupigwa vita.

ila hizi station wagon naona hazifutiki mapema kwenye kupendwa na watu
kwa mfano
stalet, vitz, rav 4, raum, harrier, ist, vanguard, n.k hizi naona zitatumika hadi ziombe poo.
 
Gari iliyooneshwa na mleta mada ni Premio na sio Carina...

Ni;iwahi kuimiliki

gari imara, body ngumu na zina nguvu si haba.

Nilikuwa najaza lita 2.5 daily - natembea kama km 15 hivi location Mbeya (kwenda kazini, misele michache na kurudi home)

Sevisi yake ya kila baada ya miezi minne

kidumu cha lita 5 na kimoja cha lita 1 (TOTAL - Rubia S)kwajili ya Engine - 60,000

vidumu vya lita 1 (TOTAL - Fluid ii D)vinne kwajili ya gearbox - 60,000

Oil Filter - 10,000

Hela ya fundi - elf 15

ukibanwa kuna mda unaipeleka garage baada ya miezi 6 sevisi itakuvumilia.

Nje ya sevisi Mambo ya kwenda garage ilikuwa mara chache sana, niliwahi tu kubadili shockup moja elf 60.

Breki zinakaa sana, nilikuwa nabadili breki baada ya miaka miwili, nadhani ni elf 55

Ila kama vp vuta kabisa Toyota Carina Ti, zinafanana vitu vingi kama na wenzake kina corolla, sprinter, ila carina ina muonekano flani hivi amazing

View attachment 2718481

View attachment 2718482

credit: picha kutoka google
 
Back
Top Bottom