Aliyewahi kumiliki hili gari atuambie sifa yake

Kama sio mtu wa fashion na kufuata mikumbo ya kitoto hilo ni gari la maana sana kwa matumizi na mazingira yetu.

Fundi hutomuona mara kwa mara na ukimuona % kubwa utakayekutana naye atajua namna ya kurekebisha tatizo.

Kama bado unajijenga kiuchumi, Nunua hilo malizana na ishu ya usafiri endelea na mambo mengine. Mbadala wake carina Ti.
 
Niliwahi kuimiliki

Gari imara, body ngumu na zina nguvu si haba.

Nilikuwa najaza lita 2.5 daily - natembea kama km 15 hivi location Mbeya (kwenda kazini, misele michache na kurudi home)

Sevisi yake ya kila baada ya miezi minne

Kidumu cha lita 5 na kimoja cha lita 1 (TOTAL - Rubia S)kwajili ya Engine - 60,000

vidumu vya lita 1 (TOTAL - Fluid ii D)vinne kwajili ya gearbox - 60,000

Oil Filter - 10,000

Hela ya fundi - elf 15

Ukibanwa kuna muda unaipeleka garage baada ya miezi 6 sevisi itakuvumilia.

Nje ya sevisi Mambo ya kwenda garage ilikuwa mara chache sana, niliwahi tu kubadili shockup moja elf 60.

Breki zinakaa sana, nilikuwa nabadili breki baada ya miaka miwili, nadhani ni elf 55

Ila kama vipi vuta kabisa Toyota Carina Ti, zinafanana vitu vingi kama na wenzake kina corolla, sprinter, ila ndio inakubalika zaidi





credit: picha kutoka google
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…