Ibrahim HC
Member
- Oct 8, 2021
- 56
- 88
Habari za wakati huu Wapendwa.
Binafsi nipende kuwashukuru wadau wote jamiiforum hakika nimejifunza mengi katika baadhi ya machapisho ya wadau nimekuwa motivated Sana kuingia kwa mara nyingine katika ufugaji.
Pamoja na kujifunza mengi Kuna baazi ya mambo Hadi hivi sasa yananitatiza ningependa kuwashirikisha, naimani ntasaidika kutokana na uzoefu wa watu wengi katika ufugaji.
Niende kwenye hoja ya msingi.
Mwaka 2017 niliingia katika ufugaji baada ya kumaliza chuo, nilikuwa ninaelimu kidogo juu ya maswala ya ufugaji na changamoto zake.
Nilianza na kuku 22 wakubwa kati ya 22 majogoo yalikuwa 3, lakini jirani yangu yeye alianza na kuku wawili tu mitetea na jogoo aliazima, baada ya miezi Kama minne jirani yangu alikuwa na kuku zaidi ya 40 pamoja na vifaranga, lakini Mimi walibaki wale wale 22 pamoja na kufanya kila kilichotakiwa kufanyika na sikuwahi kupoteza kuku kwa sababu ya ugonjwa, niliweza kuwatibu kwa dawa za asili na zilifanya vizuri.
Changamoto iliyonikuta
Kuku wangu walikuwa wanataga vizuri tu bila changamoto yoyote shida ilikuja walipoanza kuatamia mayai, wengi walikuwa wakiatamia baada Kama ya wiki ya pili wanaacha kuatamia, na walioweza kuangua vifaranga kiukweli baada ya wiki unakuta kuku Hana kifaranga hata mmoja vilikuwa vinakufa katika mazingira tata bila hata kuugua.
Kumbuka nilikuwa nafata kanuni zote za ufugaji na chakula nilikuwa nawapatia lakini jirani yangu yeye nikuwafungulia wanajitafutia na hata ikitokea changamoto ya ugonjwa kwake alikuwa hajisumbui kutibu kuku yeye ni mwendo wa kichinja tu na bado yeye alifanikiwa mara mbili zaidi ya Mimi ambaye niliamini nafaham kila kitu.
Baada ya hayo ilibidi kuwashirikisha wazee na wenyej wa mahali husika wakadai ya kuwa eti mifugo yangu halikuwa na ulinzi, wengine wakasema eti nilikuwa nakaribishwa na wenye mji japo nilifugia mashambani, nikaona isiwe tabu kuliko kukosa kabisa nikawauza wote nikaachana na ufugaji Hadi hivi leo naandika haya.
Niombe radhi kwa andiko refu, kifupi nimehamasika kurudi Tena katika ufugaji naona kabisa Kuna dhahabu iliyojificha ukiondoa changamoto ambazo zipo katika nyanja yoyote Ile katika maisha.
Jamani kwa yeyote aliyewahi kukutana na changamoto Kama yangu ningeomba tushirikishane uliitatua vipi ili nasi tujifunze, pia mnawezaje kulinda mali zenu dhidi ya mambo ya ulozi?
Natanguliza shukrani Wapendwa 🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻