TANZIA Aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge afariki dunia nchini India

TANZIA Aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge afariki dunia nchini India

R.I.P tunashukuru kwa utumishi wako,na hata aliyekuteua aliteua mtu sahihi,you were very creative.
Kwa kipindi nilichokufahamu hakika ulikuwa mchapakazi sana tena hukuishia kutoa maagizo tu bali ulienda mwenyewe field.
JKT uliibadilisha kutoka kuwa ya kuroll kwenye mifereji ya maji machafu na ya kutumia nguvu mpaka kuwa productive na kutumia akili kitu ambacho kilikuwa na tija kwa taifa.
Pole kwa familia na watanzania kwa ujumla.
 
Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge amefariki dunia leo October 12,2024 alfajiri akiwa Nchi India alipokuwa akipatiwa matibabu.

August 02, 2024 Mbuge aliagwa rasmi Jeshini baada ya kulitumikia Jeshi kwa zaidi ya miaka 38 na aliagwa kwa kukagua gwaride rasmi la kijeshi katika Viwanja vya Mgulani (Twalipo Admistration Unit-TAU) Jijini Dar es salaam.


Soma:
1. Meja Jenerali Charles Mbuge astaafu utumishi wake jeshini

2. Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT, aliyekuwepo apelekwa Mgambo

3. Major General Mbuge Kuwa RC kutoka Mkuu wa JKT Kapanda Cheo au kashuka?
Kuna siri gani watumishi wengi wakistaafu tu uwa hawakai sana wanakufa.
Ila picha yake ya mwisho alipokuwa akiagwa na kugabidhiwa gari mwezi wa nane alionyesha hakuwa sawa kifya nilinotes hiko kitu.
 
Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge amefariki dunia leo October 12,2024 alfajiri akiwa Nchi India alipokuwa akipatiwa matibabu, kifo cha Mbuge kimethibitishwa na Mtoto wake wakati akiongea na @AyoTV_.

Itakumbukwa August 02, 2024 Mbuge aliagwa rasmi Jeshini baada ya kulitumikia Jeshi kwa zaidi ya miaka 38 na aliagwa kwa kukagua gwaride rasmi la kijeshi katika Viwanja vya Mgulani (Twalipo Admistration Unit-TAU) Jijini Dar es salaam.

Mbuge amepitia katika nafasi mbalimbali za Uongozi ikiwemo kuwa Mkuu wa JKT, Mkuu wa Mkoa Kagera na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu.View attachment 3122553
Poleni sana, Magufuli alimkubali sana, alimpandisha vyeo kabla ya muda
 
Back
Top Bottom