TANZIA Aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge afariki dunia nchini India

TANZIA Aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge afariki dunia nchini India

RIEP Maj Gen wana Ruvu tutatukukumbuka daima, laiti Magufuli angekuwa hai ungeshakuwa CDF Kitambo sana, kina Msuguri na mwenzie Sarakikya bado wanadunda tu
Sarakikya ana miaka 90, yupo Imara mpaka sasa, anaongea na anakumbukumbu nzuri, yaani sijui Siri ya uimara wake ni nini.
 
Mkuu jeshini kuna vyeo ukifika hata ukistaafu, unaendelea kuhudumiwa bure mpaka unakufa, kuanzia kanali nafikiri kwahiyo hiyo haikuwa sababu
Kuanzia Cheo cha Meja Jenerali, anaendelea kulipwa asilimia themanini ya Mishahara yake mpaka kufa kwake, na anaendelea kulindwa na wanajeshi, na kupewa V8, na posho zingine, kwanza pesa anayopewa akistaafu ni kubwa, Hawa jamaa wana hela sana, hawakatwi mifuko ya hifadhi ya jamii ila pensheni zao ni kubwa mno kuliko watumishi wa umma wanaokatwa.
 
Tuliopitia jkt tunajua huyu mzee alikuwa hapendi kuruta aonewe, akikuta askari anamuonea kuruta anaweza hata akampa adhabu lakini pia alikuwa mtu poa hata kwa wanajeshi wenzie, kwa kifupi alikuwa anakubalika ndio maana wengi walisikitika alivyonyimwa u-cdf baada ya magu kufariki
Mabeyo kaondoka 2022, huyu akiwa na miaka 59.....
ulitaka apewe u-cdf akiwa bado mwaka kustaafu?
 
Binadamu hata uwe na vyeo vya aina gani lazima utakufa tu.
Jambo la msingi ni upendo kwa binaadamu wenzako.
Viongozi wenye vyeo msiwanyanyase walio chini yenu, tendeni haki.
 
Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge amefariki dunia leo October 12,2024 alfajiri akiwa Nchi India alipokuwa akipatiwa matibabu, kifo cha Mbuge kimethibitishwa na Mtoto wake wakati akiongea na @AyoTV_.

Itakumbukwa August 02, 2024 Mbuge aliagwa rasmi Jeshini baada ya kulitumikia Jeshi kwa zaidi ya miaka 38 na aliagwa kwa kukagua gwaride rasmi la kijeshi katika Viwanja vya Mgulani (Twalipo Admistration Unit-TAU) Jijini Dar es salaam.

Mbuge amepitia katika nafasi mbalimbali za Uongozi ikiwemo kuwa Mkuu wa JKT, Mkuu wa Mkoa Kagera na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu.View attachment 3122553
832Kj op kikwete, RIP mkuu wa kambi
 
Back
Top Bottom