TANZIA Aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge afariki dunia nchini India

Nimefuatilia koment kuanzia peji ya kwanza hadi hii ya sita nimegundua mwamba hakuwa na makandokando mengi maana jf huwa haicheleweshi
 
Hii familia ya Mbuge, almost asilimia 80 ya Wana familia ni Maaskari wa Jeshi pia maana Marehemu Baba yao, Mzee Mbuge alistaafu akiwa Mkuu wa Kambi moja wapo Mkoa fulani

Marehemu Charles Mbuge, alikuwa maarufu kuliko Wana familia wengine kutokana na kujiingiza kwenye burudani miaka ile ya Mwanzoni mwa 2000 akiimbwa na Twanga Pepeta akiwa na Cheo cha Captain, lakini umaarufu wake ulipanda zaidi wakati wa Utawala wa JPM, maana alitokea kupendwa na kupandishwa Cheo haraka haraka mno hadi wengine kusema "the CDF who was never be"

Poleni wote mlioguswa na Msiba huu

Tutaonana baadaye 😭😭
 
Kipindi chake pale Ruvu hapakua na kazi nyingi kama sio Bustani ni kwenye kuku ila baada ya pale alivokuja Mnyani tulikoma kila akiona sehemu ya wazi alitaka palimwe
 

Maisha ni ya ajabu sana.amestaafu tu na kufariki.yaani sidhani hata kama mafao yake yalikuwa yameshatoka.by the way huyu ndiyo yule alisimamia ujenzi qa ukuta wa mererani? pia sijui ni yeye mwenye shamba kubwa sana la kisasa huko kisarawe?
 
Sarakikya ana miaka 90, yupo Imara mpaka sasa, anaongea na anakumbukumbu nzuri, yaani sijui Siri ya uimara wake ni nini.
Huwa anapanda mlima Kilimanjaro kila mwaka yule

Ni askari hasa hadi leo
 
Baba yake na Mbuge, alistaafu akiwa kanali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…