TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

Tunawapa pole wafiwa wote na Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali inapostahili kutokana na matendo yake hapa duniani .
 
R.I.P mzee kandoro. Ila kuna la kujifunza hapa Kwa huyu mzee, yaani ccm wengine wakifa page ya kwanza huwa inajaaga washangiliaji Kwa huyu mzee imekuwa tofauti viongozi wengine wa ccm jipangeni
 
Tunawapa pole wafiwa wote na Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali inapostahili kutokana na matendo yake hapa duniani .
 
Kandoro pamoja na kuwa RC lakini alikuwa mtu mwenye roho nzuri. Aliwaongoza watu bila ya kuwanyanyasa kutokana na ufuasi wao wa vyama vya siasa, tofauti na wakuu wengine wengi wa mikoa.

Mungu mwenye huruma amjalie pumziko jema.
 
Lo ,masikini kaka yangu Abbas Kandoro.
Alikuwa mtu mwadilifu sana, hakuwa na mizaha mizaha kazini.
Na alimsikiliza kila mtu, na hakuwa mtu wa makuu.
Kitaaluma alikuwa economist, na kwenye planning alikuwa vizuri sana.

Majuzi wiki iliyopita, nikitoka Mbeya, pale karibu na Ifunda , Iringa, nyumbani kwao,nikawakumbusha wenzangu kwenye gari kuwa pale ndio kwao Abbas Kandoro, aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa ya DSM , Mbeya Mwanza n.k.
He led a simple life.

RIP Abbas Kandoro

Sasa nyie watu wa Magufuli inabidi mjifunze kitu toka kwa hawa waliowatangulia; wengi wenu mnajiona kuwa mtakuwa hapo mlipo milele!! Hivyo vyeo mlivyonavyo ni dhamana tu.
 
Haya ndio madhara ya kukimbia kimbia kupost uonekane wa kwanza kujua
 
Back
Top Bottom