Aliyewahi kwenda Zanzibar kununua vitu vya electronic bei ipoje?

Bei haziachani sana na dar,alafu utakutana na Kodi bandarini hasa kama umenunua vitu vipya,
 
Kwahiyo mkuu unataka sema nikibeba ps4 slim mbili nikizisweka kwenye begi nitàlipa kodi maana nilisikia kuna scanner (metal detector)
Tatizo unashindwa kutofautisha kati ya kodi na gatepass kodi inategemea na ukubwa wa mzigo ila gatepass ni compulsory yaani lazima ulipe ambayo kwa zanzibar kule ilikuwa unalipa elfu 5 kama gatepass na dar ni elfu 9 ukibeba TV chini ya nchi 32 unalipa tu gatepass mimi nilikuwa nabeba TV nchi 24 nafunga mbili mbili nabeba na kwenye begi langu nina pass nina heater na blender hyo scanning unayozungumzia lengo lake kubwa ni kukagua vitu visivyoruhusiwa kubebwa kama bangi na madawa ya kulevya pamoja na silaha hatarishi ila sio kwamba inakagua vitu ulivyobeba wakukamate narudia kitu chochote unachoweza kubeba mwenyewe aidha kwenye begi au mkononi vidogo vidogo kama nilivyotelea mfano havina shida mkuu na jamaa wa AZAM ukiwa tayari nitakupa namba zake PM utamcheck yeye ndo mambo yake hayo.
 
Mkuu ni vitu used tu ndo bei chee au hata vya dukani navyo bei chee na eneo gani vinapatikana zaidi
 
Nimenunua tv flat Sony iko bomba kinyoko, na friji mwaka wa nne huu...bandarini easy tu ongeaa na wale staff wa kwenye boti utapewa connection

NB bei ni karibu na bure
 
Sema mnafichua Siri asee[emoji849]
 
Mfano kama nikienda kununu Tv moja ya laki 350,000 nayo inalipiwa ushuru? Na kitu kama hiyo PS ya kuweka kwa begi unalipia ushuru? Na kama ushuru ni bei gani?
Kwa Bei ya 350 ushuru Ni sh elfu sitini bandarin 60,000. dar wakala anakutolea mzigo wako nje anakupa , na hiyo sitini unalipia kabisa kipindi unanunua mzigo mwenye duka anawasiliana na agent wake wewe unapokea mzigo bila Shaka ki halali kabsa.
 
Mkono mtupu fanya kazi na mabaharia wale wanajua chocho zote za mafisadi
 
Mi sitoi mzigo wowote nowdays
Nanyoosha miguu unanifikia ulipo

Nimeandika hapo natumia agents.
Nyoosha maelezo mkuu taratibu za kutumia ajent zipoje na kwa tv ya inch 43 ajent analipwa pesa ngapi na huyo ajent ni wa bongo au visiwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…