Aliyezusha kifo cha binti aliyebakwa Yombo atiwa mbaroni

Aliyezusha kifo cha binti aliyebakwa Yombo atiwa mbaroni

Muliro buana ,watu wanataka waliobaka na aliyewatuma na sio huyo jamaa ambaye unaona kabisa ana tatizo la afya ya akili maana kikawaida 54 yrs hauwezi kufanya aliyoyafanya.
Sasa hivi wenye miaka iyo ya 50 na 60 na kitu ndio wenye matatizo ya akili sana. Wala hakuna cha kushangaza hapo tunajua wengi wao wenye miaka iyo ni wagonjwa wa ubongo
 
#Aliyesambaza taarifa kapatikana waarifu Bado hawajapatikanašŸ˜‚#

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Amos Lwiza (54) mkazi wa Tegeta Wazo wilaya ya Kinondoni mkoani humo, kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuwa binti mkazi wa Yombo Dovya ambaye video zake zilisambaa mitandaoni akibakwa na kulawitiwa na vijana watano kuwa amekutwa tayari kashafariki dunia.

Kamanda Muliro amesema binti huyo anayedaiwa kulawitiwa na kubakwa bado yupo hai hajafa, kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na kwamba uchunguzi wa tukio hilo la kikatili bado unaendelea.

#KitengeUpdates

Pia Soma
- Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa na wanaume watatu

- Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam: Binti anayedaiwa kulawitiwa na kubakwa bado yupo hai, hajafa kama ambayo imeripotiwa katika baadhi ya mitandao
Kwahiyo huyo ni mbaya zaidi kuliko wale wabakaji?
 
Wale vijana wa 5 wameshakamatwa ni kwa vile kuna hatua za kufuata kushughulikia hili, Comfirmed. Tena kama yule mchukua selfie ni ajira ya mwaka jana masikini. Mama Captain bado hajaguswa hadi sasa…. Mnatuambia nini? Hawa vijana wakitumwa kulinda amani Victims wa vita watapona kweli?

Jeshi kazieni discipline kwenye recruitment , vile vivuta bangi mmevitoa wapi? Vile vikijana ni vishoga, Kijana straight anawezaje kuvua nguo na kuwa uchi vile mbele ya kijana mwenzie jinsia moja?

Hatua kali zichukuliwe wiser, Sisi wana mtandao (wanachi) hatutawaelewa.

#JeshiLimechafuka#
Hivi kumbe ni wanajeshi na siyo polisi
 
Hivi kumbe ni wanajeshi na siyo polisi
Jioni nilikuwa naulizia kwa ā€œmtuā€ kama wamekamatwa or not akanipa hiyo taarifa ya kukamatwa tu sikumuuliza kama ni wajeshi au mapolisi, Ila katika kuongea ongea ndio akaniambia huyo mwenye uso mpana ni ajira mpya (aliongea kwa kumuhurumia) .

Nikachukulia moja kwa moja kuwa ni wajeshini.

Btw, Miss you Jadda.
 
Hmna
Jioni nilikuwa naulizia kwa ā€œmtuā€ kama wamekamatwa or not akanipa hiyo taarifa ya kukamatwa tu sikumuuliza kama ni wajeshi au mapolisi, Ila katika kuongea ongea ndio akaniambia huyo mwenye uso mpana ni ajira mpya (aliongea kwa kumuhurumia) .

Nikachukulia moja kwa moja kuwa ni wajeshini.

Btw, Miss you Jadda.
Aliekamatwa mbona mnapenda kudanganywa sana
 
Back
Top Bottom