Aise nakuunga mkono wanaoongoza kumsingizia shetani ni wakristo.Unakuta mke wa mtu anatembea nje ya ndoa mume akijua wanasameheana hata mume naye anaingilia kati mke wangu shetani ndiye amefanya yote haya ni jambo zuri kweli kusameheana ila shetani anaingiaje hapo.
Waislam wao hakuna cha shetani wala nini ni talaka ya chap ila ukiamua kusamehe ni wewe mwenyewe.
Wakristo kila kitu ni shetani mtu anaugua magonjwa ya kurithi ya ukoo labda ukichaa anasingizia shetani
Naomba nisieleweke naleta ubishi wa kidini maana hata mimi ni mkristo ila tumezidi sana.
Mbele za mungu tukishitakiwa pamoja na shetani atamuambia muheshimiwa mungu vingine nilikuwa nasingiziwa watu wako vichwa ngumu sana.