Ukweli mchungu ni kuwa, hawa watu wameshafanya makosa mengi sana yakiwemo ya jinai kama vile tuhuma za wizi na ufisadi, mauji,kuteka na kupoteza watui na nyingine nyingi. Hivyo, si rahisi kwa wao kuaachia madaraka kwa hofu ya kushughulikiwa na kwahiyo wanalazimika kuhakikisha wanabaki madarakani kwa gharama yoyoyte ile.
Hata hivyo, hali hii haiondoi ukweli kuwa wao kama binadamu, wanaishi na nafsi zinazowasuta kwa matendo yao maovu ingawa machoni mwa watu wanajitahidi kupeleka picha tofauti na moja ya ushahidi wa hiki nachosema ni hii nguvu kubwa wanayotumia waonekana wanakubalika mbele za watu na kwamba wana furaha na amani katika mioyo yao.
Kitendo cha CHADEMA kukataa kushirikia katika huu uchaguz, ni pigo kubwa sana kwao na wanona aibu sana katika nafsi zao huku roho zikiwasuta kwani wanajua kuna mamilioni ya watanzania wanaipenda CHADEMA na wamewanyma hiyo nafasi kwa kushindwa kwao kuweka uwanja wenye ushindani sawa na wa haki kwenye uchaguzi.
Mmejiuliza nini kimemfanya huyo Mama kusema na kuna vyama vimekimbia uchaguzi? Kuna mtu alimuuliza?
Jibu rahisi: Nafsi inamtesa na anajishitukia sana sawa na mtu alifenya dhambi ya kuua na sasa anaishi kwa hofu na mashaka. Huyo ndio Mama na hali hio ni kwa wenzake wote.
Option waliobaki nayo ni kushupaza shingo tu hata mkisema nini lakini ukweli ni kwamba mioyoni mwao nafsi zinawasuta na bilsa shaka hata amani ya moyo hawana japo wanapata kila wanachokitaka.
Kwa kifupi, hawana tofauti na mtu anaeteseka baada ya kudhulumu mali ya mtu tena mtu masikini.