Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,017
- 16,431
Mimi huwa sipandi KLM kwa hivyo mambo ya KLM siyajui vizuri. Mimi hupanda Emirates na Qatar. Eti KLM ilianza direct flights between Kilimanjaro na Amsterdam mwaka gani?Hamna kitu kibaya kama kuongelea kitu usichokijua. KLM wamekuwa na direct flights za Amsterdam - Dar es Salaam-Amsterdam (baadae via Kilimanjaro na Zanzibar) kwa miaka yote tokea waanze kuja Tanzania.
Haijawahi kumlazimu mtu yeyote kutoka Tanzania kupitia JKIA kuifuata KLM. Mimi ni abiria wa miaka mingi wa KLM na sijawahi kupitia Nairobi kuifuata.
Halafu hamna kitu kama hub ya KLM East Africa, Wakenya mna ujinga mwingi sana bila kujijua.
Mabadiliko yaliyofanywa na KLM ni ya muda mfupi kutokana na kupungua kwa wasafiri wakati huu wa covid-19. Hali ikitengamaa safari zao zitarudia kama kawaida.
Abiria wa kutoka Dar es Salaam kwenda Amsterdam hawatashuka Nairobi hata kidogo zaidi ya kuongezea abiria wa kutokea Nairobi. Ndege itayotumika ni hiyo hiyo (B787-9 au B787-10 ya KLM).
Swiss International Airlines wana route ya aina hiyo kwa miaka mingi sasa. Route yao ni Zurich-Nairobi-Dar es Salaam - Zurich.
Punguza hisia zako kwenye vitu usivyovifahamu.