Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Hawajibu maswali waleScars nakufuatilia endelea.
Walichoniambia ni kuwa hilo swali atakujibu aliyekuleta.
Nikawaambia atanijibuje huyu wakati yeye bado sio mnufaika wa hii biashara kama nyinyi.
Hamuoni kama naye huyu yupo hapa kujifunza na moja ya sababu za kumfanya atoe hela ni pale anapokuwa hana mashaka na hii biashara.
Na mashaka yetu yanahitaji majibu mazuri kutoka kwenu ili yaweze kuondoka.
Hawakujibu kitu wakanisisitiza nije semina ya pili nitapatiwa majibu nikaamua kuwapotezea.