ALLIANCE GLOBAL: Kampuni ya kitapeli inayoendelea kuliza wasomi wengi nchini

ALLIANCE GLOBAL: Kampuni ya kitapeli inayoendelea kuliza wasomi wengi nchini

Hawajibu maswali wale

Walichoniambia ni kuwa hilo swali atakujibu aliyekuleta.

Nikawaambia atanijibuje huyu wakati yeye bado sio mnufaika wa hii biashara kama nyinyi.

Hamuoni kama naye huyu yupo hapa kujifunza na moja ya sababu za kumfanya atoe hela ni pale anapokuwa hana mashaka na hii biashara.

Na mashaka yetu yanahitaji majibu mazuri kutoka kwenu ili yaweze kuondoka.

Hawakujibu kitu wakanisisitiza nije semina ya pili nitapatiwa majibu nikaamua kuwapotezea.
Jambo ambalo mimi hushindwa waelewa hawa watu ni REASONING yao.

Kama unaweza washawishi watu wakatoa hela, kwanini wasizidirect kwenye shughuli halali na wakanufaisha watoa fedha na wao wenyewe?
 
Daaaaaah,umeamua kutuharibia mkuu!.
Nimesoma hakuna AJIRA,Ila nimeamua kujiajiri.
Mada Moto,wapenda ganda la ndizi matokeo ya elimu yetu ndo hiyo.

Siku hizi kamari mpaka TBC TAIFA.
Wakipona nite mbwa,nipo PALEEE.
 
MWISHO AKAJA KWENYE POINT


AKasema wamekuja na bidhaa ambayo ni package ya dawa lakini ni virutubisho. Wakasema wamefanya hivyo ili kuwasaidia watu hususani vijana watumie product hiyo kujikomboa kwenye umasikini.


Mchanganuo wa hiyo product sasa.

Ni kwamba kwanza unatakiwa uelewe kuwa hiyo product haitolewi bure. Ni package inayouzwa Shilingi 500,000.

Ndani yake kuna mchanganyiko wa dawa zenye kutibu magonjwa mengi ikiwemo kisukari, ugonjwa wa moyo, na Covid.

Hivyo unachotakiwa kufanya ni kutengeneza pair. Ukinunua hiyo package utafunguliwa account na kiasi fulani cha pesa utawekewa.

HAlafu ukimleta mtu mwingine hapa akanunua tena package yetu maana yake utapata shilingi 50,000 ambayo nayo itaingia kwenye account yako iliyotengenezwa.

KWa hiyo naye huyo mtu akileta mtu mwingine ndivyo utavyozidi kutengeneza hela kupitia pair.

MASWALI NILIYOWAULIZA

Niliponyoosha mkono kutaka kuuliza swali akaniruhusu.

SWali lilikuwa ni hili

Ikiwa kama kweli nyinyi mmeamua kumsaidia kijana ajitoe kwenye umasikini kwanini muweke gharama kubwa ya kununua hiyo bidhaa?

Je ni kweli mna amini mtu anayeweza kuwa na laki 5 ni mtu ambaye anahitaji kusaidiwa kuepukana na umasikini?

NImesikia kuna watu humu mnamiliki majumba na utajiri wa kifahari. Mwingine kasema ana
miliki 150M. Sasa akitoa 10M akatununulia hiyo product atakuwa amesaidia watu wangapi kuwainua kiuchumi?
Aahaaaa,alijibuje?
 
Kwamba. Waandika ada pamoja na cost zote ni dollar 4000 , ila ukifika chuoni hata. Gharama zote hazifiki 1000.......
Wanakuwa wameshajilipa cha juu zaidi ya asilimia 100 huku wanajifanisha kana kwamba wanakusaidia si ajabu na picha yako ukiwa airport unaagwa ikatumika kwenye matangazo kushawishi wengine.
 
Daaaaaah,umeamua kutuharibia mkuu!.
Nimesoma hakuna AJIRA,Ila nimeamua kujiajiri.
Mada Moto,wapenda ganda la ndizi matokeo ya elimu yetu ndo hiyo.

Siku hizi kamari mpaka TBC TAIFA.
Wakipona nite mbwa,nipo PALEEE.

Hali ni ngumu na kizazi hiki cha digitali bila ajira, vijana wanazidi kukosa mwelekeo na wapigaji nao kila uchao wanazidi kuboresha mbinu zao kulingana na muktadha, kuchomoka si rahisi.
 
hata universisty abroad ya mtu anaitwa Tonny ya kupeleka wanafunzi nje ya nchi ni matapeli kuliko matapeli wote duniani mshenzi sana huyo TONNY na genge lake ofisini
Hapa nakukatalia, nime fanya kazi na university abroad representative naijua in out acha kupotosha jamii

Sent from my itel A662L using JamiiForums mobile app
 
Jambo ambalo mimi hushindwa waelewa hawa watu ni REASONING yao.

Kama unaweza washawishi watu wakatoa hela, kwanini wasizidirect kwenye shughuli halali na wakanufaisha watoa fedha na wao wenyewe?
Lengo la msukaji mipango tokea mwanzo si kufanya biashara halali kunufaisha pande mbili bali yeye mwenyewe, kwa maana siku zote biashara halali ina risks/hasara na gharama zingine ikiwemo kodi, mishahara na mengineyo.

Huyu tapeli Mfilipino na wengine wa kariba yake hawana tofauti na wamiliki wa apps za social media na digital currency ulimwenguni ambao wanautajiri wa kufuru, wao utumia Mind psychology kuadaa na kuadict behavior ya watumiaji wa bidhaa zao kisha uchumia kivulini bila jasho, mlengwa aambulii chochote asipokuwa mjanja yeye anaishia kutoa tu mpaka awe mtupu.

Alliance Global kwa kulitambua hilo wanakufanya mlengwa uwalipe pesa ndefu kwanza baada ya hapo unakuwa mateka kwao ukijipa matumaini ya kurudisha ulichowekeza lakini pia ukiwaza kutoboa kimaisha kumbe ndiyo hivyo ushalevya na kutoka tena ni majaliwa na yeye CEO popote pale halipo pasipo kutumia nguvu kubwa uendelea kuchukua maokoto yake bila VAT wala tozo za mwigulu na hata biashara ikikumbwa na kashikashi yeye haimyumbishi anafungua tu tawi katika taifa jingine ambalo bado lipo usingizini mostly Africa maisha ya utapeli yanaendelea.
 
Kwanini unasema hivi mkuu
Kwani na wewe ni mlengwa mkuu?
Tunasema hivyo kwa kuwa biashara yeyote ile ina ethics zake hata kama unatengeneza faida kubwa upaswi kumfanya mteja wako mtumwa/ndondocha asiyefaidika na mfumo wa toa-nami nitoe, biashara haiwezi kuwa upande mmoja tu ndiyo unatoa kila kitu na upande mwingine unapokea na kuneemeka tu.
 
Ajira Hamna...vijana kujiajiri hawana mtaji ..bush hawataki kukaa... Wazazi wamewachoka.

Wacha waje mjini.
Bila Shaka hawatotoka bure.
Ndiyo washatoka bure hivyo unless wajiongeze waingie kitaa kusaka michongo lasivyo hali si hali mle kambini unaamka na ubao huku ukishindia mafunzo ya namna ya kuchojolewa zaidi.
 
Hali ni ngumu na kizazi hiki cha digitali bila ajira, vijana wanazidi kukosa mwelekeo na wapigaji nao kila uchao wanazidi kuboresha mbinu zao kulingana na muktadha, kuchomoka si rahisi.
Yaani Mambo si Mambo,ila elimu yetu nayo inachangia ndugu.
Konection ndogo,Bongo hii msemo wa YOUNG D.Bongo bahati mbaya.
BASATA wakaufungia ule wimbo,ukweli ndo uleeeeeee wameuning'iniza kwenye KITANZI.
 
Yaani Mambo si Mambo,ila elimu yetu nayo inachangia ndugu.
Konection ndogo,Bongo hii msemo wa YOUNG D.Bongo bahati mbaya.
BASATA wakaufungia ule wimbo,ukweli ndo uleeeeeee wameuning'iniza kwenye KITANZI.
Bongo kweli nyoso..bongo balaa![emoji124][emoji124][emoji24]
 
Hatari sana ni scammers wenye mitaji ya kukodi hadi ukumbi matata ili uamini tu upigwe

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
Ikiwa wale maajenti njaa wa suti nyeusi wanakodiwa mpaka magari ya kutembelea kwa ajili ya ku-fake life hili kuingiza kuku wengi bandani, watashindwa nini kwenda kukodi kumbi za gharama huku wakijua unadhifu uficha umasikini[emoji23][emoji23]akili kumkichwa..[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hapo bado ujaoneshwa picha za kina Trump na mabilionea kadhaa (Photoshop) wakitumia bidhaa zao za virutubisho na kuvisifia ubora wake, yaani utake usitake lazima uingie kingi.[emoji23]
Hapo kahsaletwa mrembo mkaliii anakokota begi

Eti katua kutokea Ohayo Missouri kwenye maonyesho na kilele Cha mafaniko ya bidhaa na testimonies za watu mashuhuli..... Eti huyo ndio yule tulikuwa tunaongea nae akiwa kwa Flight ameunga kuwawahi ..me mbavu sina.😂😂
 
Ikiwa wale maajenti njaa wa suti nyeusi wanakodiwa mpaka magari ya kutembelea kwa ajili ya ku-fake life hili kuingiza kuku wengi bandani, watashindwa nini kwenda kukodi kumbi za gharama huku wakijua unadhifu uficha umasikini[emoji23][emoji23]akili kumkichwa..[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ahahaha na wabongo tunavyoamini mtu anae miliki Gari ndio mwenye pesa na tajili lazima watu walizwe [emoji848] watu wanacheza na akili tu

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom