Yaani hadi inatia hasira, kwanini vijana wa siku hizi hatuna ufuatiliaji wa mambo, unaambiwa kuhusiana na Kampuni usiyoifahamu vyema kama msomi na mkononi una simu janja kazi kufuatilia stori za mwijaku na baba levo, unashindwa kuingia Google uandike Alliance Global utapeli uone kama utapata walahu dondoo kuhusu experience za users i.e kwenye Google kuna makala ya gazeti la Mwananchi kuhusiana na utapeli wa Alliance Global huko Kilimanjaro n.k, Umeshindwa huko basi pitia Jamii Forums, Haya tuseme facebook ingia search andika Alliance Global moja kwa moja itakuijia video ya makala ya Ripoti Maalum kutoka ITV..June 15, 2022 kuhusiana na matukio ya hawa matapeli n.k