Nilitamani sana umalizie simulizi alizokueleza huyo mdada na namna ulivyomuokoa kupigwa.
Katika simulizi yake; yeye ni graduate na hana kazi, sasa katika pilika pilika za kutafuta job akaambiwa na baba yake ambaye ni msataafu kuwa kuna kijana wa mzee fulani anayefahamiana naye toka kijiji X kwa sasa kafanikiwa huko jijini Mwanza kimaisha baada ya kuajiriwa kwenye kampuni fulani inayodili na biashara ya online marketing.
Pia kijana huyo alimwahidi baba yake kuwa atamuunganisha binti yake aajiriwe halipo yeye, kikubwa huyo baba (mstaafu anajulikana siku zote pensheni inasoma) awe tiyari kuchangia bidhaa zao za virutubisho kwani nje na kumtibia BP pia itamwongezea (bintiye) sifa za ziada kwa mabosi wake kumkubalia kirahisi kuungana nao kwenye biashara hiyo, bila hiyana mzee wa watu kwa ajili ya bintiye kupata kazi akaona isiwe tabu akakubali kupigwa kwa kununua kwanza bidhaa hizo za virutubisho (kwa Tsh.200,000)na akasafirishiwa kwa njia ya basi hadi huko kijijini kwao.
Baada ya hapo ni zoezi la kuja mjini ambapo mzee akahakikishiwa kuwa binti yake aje tu kwanza na kiasi cha shilingi 30,000 ambazo ni kwa ajili ya kitambulisho na kujiandikisha, ila asiofie pakufikia mwanaye kwani huko kazini wanahosteli nzuri na salama kwa ajili ya kufikia wafanyakazi wao waliotoka mbali, mpaka pale watakapozoea mazingira ya kazi wanaeza enda kupanga kikubwa aje na pesa ya kula tu (kwa kuwa kijana anahaminika kwa wazee na pale kijijini ni mtu mwenye heshima yake mzee akamruhusu binti achangamkie fursa)
Binti anaeleza kuwa mojawapo ya kitu kilichomvutia kuhusu kazi husika ni pamoja na kuambiwa kuwa atafanya kazi katika kampuni nzuri, yenye ofisi kubwa na makompyuta ya kutosha kinachotakiwa ni yeye tu kuja kuripoti na kuelekezwa mara moja namna ya kuuza bidhaa mtandaoni kisha aanze kuvuta mshahara wa bila jasho kwa kuwa wao hawatembezi bidhaa juani kama machinga, wao shughuli zao zote huishia mtandaoni na unalipwa vizuri kila sekunde unapofanya mihamala hawasubiri tu hadi mwisho wa mwezi (japo mshahara mwisho wa mwezi pia upo palepale)
Sasa binti anakwambia kuwa alikuwa akiwasiliana na huyo tapeli X kwa njia ya simu tokea ameondoka kwao mpaka anafika stendi ya mabasi Nyamhongolo kila mara alikuwa anapewa maelekezo ya namna ya kufanya, sasa siku ile anakuja kwa bahati mbaya gari alilopanda (binti) lilipata hitilafu likaharibikia njiani hivyo akafika Mwanza mida ya jioni kabisa, alivyowasiliana na tapeli X akamwambia kama vipi tafuta lodge yeyote iliyokaribu nawe ulale mpaka kesho ndiyo uje ofisini kwa maana sisi shughuli zetu mwisho saa 9:30 mchana hivyo hatuna namna ya kukusaidia.
Binti japo Mwanza hapajui ila alikuwa akipita maramoja moja akielekea huko chuoni kwao Morogoro kuna mtaa alikuwa ana-idea nao (Igoma) hivyo akaendazake kutafuta malazi hapo hadi kesho yake ambapo ndipo siku nilipokutana nae akiwa anaelekea kwa wazee wa kazi kupigwa....
"Tunaendelea sasa na pale tulipoishia...baada ya kugundua ni mgeni na kisha kunieleza vile kuwa kuna kampuni hapo mitaa ya CCM Kirumba sijuhi ameitishiwa kazi mara imepanda mara imeshuka mmh! nikawa na mashaka ndipo ikabidi nianze kumdodosa kiundani kuhusiana na kampuni husika.
Kumhoji dada wa watu kwani Kampuni yenyewe inaitwaje? Akaniambia hata na yeye hajui bado maana kila alipojaribu kumhoji jamaa ni kama alikuwa anamumunya maneno na hasikiki vizuri, kama utani nikamwambia wasije kuwa ni matapeli hao! Dada wa watu akashtuka ila kwa ujasiri akanijibu haiwezekani yule kaka hawezi kufanya hivyo tunaheshimiana sana, nikamuuliza kwani ndiye huyo muda wote mlikuwa mkizungumza nae, akanijibu hapana huyu ni mwingine kaniambia anaitwa X naye anafanya kazi kampuni hiyohiyo kapewa namba zangu na yule mtu aitwaye X hili aje anipokee, sasa ndiye mara kwa mara nawasiliana nae (hapa kwa uzoefu tu nikawa nishausoma mchezo unaoendelea siyo mzuri wenda kuna shida mahali)
Hapo hapo nikauvaa moyo wa huruma nakadhamira kale ka kusaidia jambo lisilonihusu ikawa inaniijia akilini ila najaribu kuyashinda majaribu, hatimaye tukafika Natta japo sikuwa na mpango wa kushuka ila nikajikuta nashukia pale kumsaidia binti wa watu na kazini nikapiga simu ya hudhuru ya kuchelewa kidogo (sijui kwa kuwa ni mrembo ndiyo maana
najikuta mwana wa Zebedayo[emoji23])
Nikamsindikiza mpaka stendi ya daladala ya makoroboi, palepale akapigiwa simu kuulizwa alipo (nikamwambia ajibu vipi) hapohapo jamaa akatuma meseji kuwa kuanzia hapo wawasiliane kwa meseji kwani yupo ofisini, basi tokea hapo chating zikawa ni zile za namna ile nilishazizungumzia mwanzoni hatimaye tukafika kituo cha daladala cha misheni jirani na rock city mall mahali tuliposhukia,
Wakati tunatembea kuitafuta furahisha kwa mujibu wa maelekezo ya tapeli nambari mbili, ikanibidi nitafute jambo la kupotezea ka muda hili nimchane binti hatari inayomkabili na nimpange cha kufanya kwa kuwa muda sasa ni karibia saa nne asubuhi najua tumbo linadai nikampitisha mgahawa mmoja jirani na hapo uwanja wa furahisha kupata kifungua kinywa (ambao ulikuwa hauna wateja wengi nyakati hizo) nikamfungukia wasiwasi wangu wote kuhusiana na kampuni hiyo X ninayohisi ni ya kitapeli na nikampanga cha kwenda kufanya akifika huko (mwanzoni alionesha kutoniamini kabisa tena kuna kale kamtizamo ka dharau fulani hivi machoni mtu akiwa anakueleza jambo usilokubaliana nalo alikuwa nako, ila akazidi kunihakikishia kuwa anajua hamna shida anaamini hizo ni hisia zangu tu ila hamna inshu)
Baada ya chai mie nikampa assignment ya kuniripotia kila kinachoendelea kwa SMS na aende ila asitoe pesa wala chochote kile hata begi lake ikitokea ameombwa lipelekwe mahali popote pale asikubali, nikamwacha mie nikaenda zangu kazini,
Sasa yaliyoendelea huko seminani ndiyo hayo nilishayaelezea yote, baada ya kutoka job ikabidi nimpitie binti wa watu hapo VILLA PARK (mahali walikokita kambi-matapeli) nikampeleka kwenye restaurant za jirani kula huku ananisimulia kila kilichojiri tokea tumeachana mpaka muda huo, nikamwambia sasa si unaona nilichokueleza tokea mwanzo,
Palepale binti bila kujizuia akaanza kuangua kilio akifikiria alivyodanganywa na uhalisia ulivyo, pili akinishukuru kwa wema niliomwonesha, kama gentleman nikajiongeza na leso mkononi hili binti afute machozi huku nikimfariji kwa kuishinda mitihani ya utapeli na punde mipango ya kurejea alikotoka ikafanyika nami sikuwa na la ziada tena katika simulizi hii nikawa sina budi kuishusha kalamu yangu chini kufikia hitimisho.