ALLIANCE GLOBAL: Kampuni ya kitapeli inayoendelea kuliza wasomi wengi nchini

ALLIANCE GLOBAL: Kampuni ya kitapeli inayoendelea kuliza wasomi wengi nchini

jamaa yangu aliitwa na wale jamaa wanajiita Qnet 2018[emoji28][emoji28]akapigwa seminar ya kutosha kwa maelezo yake anasema aliwaelewa kabisa,kimbembe kikawa kiingilio.

anasema aliporuhusiwa kuuliza swali akiwa tayari na goosebumps akauliza,sasa bro si unikope hiyo 5mln niingie then baada ya mwezi nikianza kuingiza $$$$ unakata percent yako mpaka hela yako irudi[emoji28][emoji28],jamaa akamjibu kwa swali,kwani hakuna hata sehemu unaweza kukopa au hata kuuza mali uliyo nayo ukapata hiyo hela???

mwamba kwa swali hilo akili ikafunguka,kumbe lengo hapa ni hii 5mln yangu sio mimi nifanikiwe,akaaga na kusepa[emoji23][emoji23]

Hii siyo spiritual tena hii inaitwa koridoni awakening kabla ya kufikia malango ya kupigwa,[emoji23] ilipaswa huyu mshikaji akachinje kuku asherehekee ama aende akatoe fungu la kumi kwa kunusurika kuzama katika domo la mamba.
 
Vanilla Vanilla Vanilla [emoji51]
Kilo1 ni shilingi milioni 1 utajiri nikufumba na kufumbua kwani bado unangoja nini? wekeza nasi sasa...baada ya hapo watu wakaota mbawa wawekezaji wakaambulia vumbi tu[emoji23]wakati mwingine bora kuwa mjinga ujifanye kama fursa zingine huzioni mpaka uone kama yaliyomo yamo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nimesoma hichi kitu nimecheka sana wakuu, kwa nini nimecheka! Nimekumbuka jambo moja limenitokea Songea mwezi mmoja uliopita mambo ya utapeli haya haya nikikumbuka nacheka hadi nalia.

[emoji15]Ilikuwaje? Tupe ubuyu mkuu.
 
Watotl wa kibongo wengi wanapenda mafanikio ya haraka mwisho wengi wanaishia kutapeliwa
Siyo wakibongo tu bali kwa sasa ni dunia nzima vijana wanatamani kufanikiwa haraka na kuenjoy maisha kama wanavyoyaona katika social media kutokana na utandawazi, ila kinachowaponza ni njia wanazopitia, ambazo si namna bora na salama ya kufanikisha ndoto zao hizo ndipo wanapokumbana na matapeli ambao nao wanania na pesa za haraka haraka hivyo unageuka kuwa mchezo wa kuwaiana.
 
Afu hawa bado nawasikia kwenye kipindi cha michezo cha Wapo Radio wanaendelea kufanya promosheni

Japo humu kuna mdau alileta habari kuwa tayari watu washapigwa, ila inaonekana Vanilla hawajafikia malengo ya idadi ya watu waliopanga kuwapiga na ndio maana promo inaendelea
Ukiona hivyo ujue shetani bado yupo kwenye kampeni kwa maana hela siku zote huwa hazitoshi na ukiona hawa matapeli wamepotea kabisa mitaani ujue kuna chimbo jipya wamelianzisha mahali na kama bado hawajapata idea mpya ya utapeli lazima waendelee kuwaganda kama kupe hata mkiwazodoa hawaondoki wanaonga mamlaka na kuendelea kuzurura humu humu kukusanya maokoto.
 
Uje na ushuhuda kuhusu huyu jamaa! Nilikuwa namuoma ni mtu smart sana kila nilipokuwa nikimtazama kwenye TV akihamasisha vijana kusoma nje ya nchi kupitia university abroad!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Si ndiyo hawa naowasikia kuwa kila kijana anayepeleka maombi ni lazima afaulu na mwisho wa siku haendi popote.

Hakuna cha abroad wala kutimiza ndoto zake zozote za maana?

Na ukiingia kwenye 18 zao unageuzwa mtumwa
 
[emoji15]Ilikuwaje? Tupe ubuyu mkuu.
Nilikuwa safarini mkoani humo nikatafuta logde nikapata nikaingia ndani nikalipia chumba nikajisikia njaa nikauliza wapi wanapika chakula wakaniambia humo ndani kuna restaurant so nikaelekezwa, nikaenda kufika nakuta watu wamejaa upande mmoja na wamepanga viti kama kuna kikao maalum nami nikatafuta sehemu nzuri nikatulia zangu nikawa busy na simu yangu huku nikisubiri chakula kiandaliwe.

Baada ya mda kidogo kaja kijamaa na pikipiki mpya, kwanza kaingia kwa mkwara mzito sana kafika na kuingia ndani naona anapokelewa na wale vijana kwa full shangwe huku neno boss likirindima sana kuna wengine vidada vizuri vikampa hug za kutosha pale.

Basi bhana baada ya yote hayo mara ghafla nikasikia naomba tusimame wote na kuanza kupeana soma namna ya kumtengeneza mteja na tuzidi kuwa mamilionea, daah nikashtuka hawa wawe mamilionea au mie sijaelewa vizuri nikaona ngoja niongeze umakini huku nikizuga nipo busy na simu,.

Baada ya mda ndio somo likakolea wakifundishwa kwanza namna ya kuvaa wanapoenda kwa mteja na namna ya kuongea na mteja, loooh nikastuka nikajua tayari vijana wanaopigwa hapa, basi mmi nikala chakula changu na kuagiza maji na kujifanya kunywa taratibu kinafki ili tu kutaka niendelee kudaka umbea.

Mara ghafla nikakumbuka nina kitype recorder kidogo kidogo tu nikaenda room nikakitoa nikajifanya kukaa kiti cha karibu nami kuanza kurecord taratibu jamaa akajimwaga weeee, mwisho kabisa akanikaribisha na mimi akaniambia wewe unaweza lipa milioni 2 utapewa saa nzuri na mimi naweza kuiuza milioni 6 hadi 7 hivi nami nikamjibu fedha nilionayo ni ndogo sana, akaniuliza nina kiasi gani nikamwambia nina laki 5 tu akaniambia unaweza anza nayo hiyo tu inatosha.

Baada ya maneno mengi mengine nilikuwa hata simsikilizi maana kuna mda nilikuwa natamani kucheka kwa namna vile ananipanga, baadae bhana wakamaliza wakaondoka, kesho yake wakafika tena asubuhi na mapema vijana kama 60 hivi daah ngoja niishie hapa ila kiufupi niliwachoma jamaa akaja kudakwa fasta.
 
Nilikuwa safarini mkoani humo nikatafuta logde nikapata nikaingia ndani nikalipia chumba nikajisikia njaa nikauliza wapi wanapika chakula wakaniambia humo ndani kuna restaurant so nikaelekezwa, nikaenda kufika nakuta watu wamejaa upande mmoja na wamepanga viti kama kuna kikao maalum nami nikatafuta sehemu nzuri nikatulia zangu nikawa busy na simu yangu huku nikisubiri chakula kiandaliwe.

Baada ya mda kidogo kaja kijamaa na pikipiki mpya, kwanza kaingia kwa mkwara mzito sana kafika na kuingia ndani naona anapokelewa na wale vijana kwa full shangwe huku neno boss likirindima sana kuna wengine vidada vizuri vikampa hug za kutosha pale.

Basi bhana baada ya yote hayo mara ghafla nikasikia naomba tusimame wote na kuanza kupeana soma namna ya kumtengeneza mteja na tuzidi kuwa mamilionea, daah nikashtuka hawa wawe mamilionea au mie sijaelewa vizuri nikaona ngoja niongeze umakini huku nikizuga nipo busy na simu,.

Baada ya mda ndio somo likakolea wakifundishwa kwanza namna ya kuvaa wanapoenda kwa mteja na namna ya kuongea na mteja, loooh nikastuka nikajua tayari vijana wanaopigwa hapa, basi mmi nikala chakula changu na kuagiza maji na kujifanya kunywa taratibu kinafki ili tu kutaka niendelee kudaka umbea.

Mara ghafla nikakumbuka nina kitype recorder kidogo kidogo tu nikaenda room nikakitoa nikajifanya kukaa kiti cha karibu nami kuanza kurecord taratibu jamaa akajimwaga weeee, mwisho kabisa akanikaribisha na mimi akaniambia wewe unaweza lipa milioni 2 utapewa saa nzuri na mimi naweza kuiuza milioni 6 hadi 7 hivi nami nikamjibu fedha nilionayo ni ndogo sana, akaniuliza nina kiasi gani nikamwambia nina laki 5 tu akaniambia unaweza anza nayo hiyo tu inatosha.

Baada ya maneno mengi mengine nilikuwa hata simsikilizi maana kuna mda nilikuwa natamani kucheka kwa namna vile ananipanga, baadae bhana wakamaliza wakaondoka, kesho yake wakafika tena asubuhi na mapema vijana kama 60 hivi daah ngoja niishie hapa ila kiufupi niliwachoma jamaa akaja kudakwa fasta.
[emoji122]hongera mkuu, kwa kazi iliyotukuka ya kujitwalia kiti cha mbele peponi, hiyo ndiyo dawa yao peleka polisi huko wakachezee virungu.
 
Aloo.. Chuo hiyo nikauza products zao.. Wala haziuziki.🤣🤣
Tena kidogo niliambiwa nauza bangi.
Badae nkaona sokapohapa mwaisa 🤣🤣🤣 maisha ni kuchagua na nimechagua kwenda mbele sirudi tena nyuma.
Anyway nilijifunza na siwezi rudia makosa ya kiufundi kama hayo.
 
Goodmorning bilionear, hata iwe saa mbili usiku salam yao ni hiyo tu.
Your next bilionear, unaambiwa ni bilionea mtarajiwa wakati hata kula yako ni shida.
Duka mtandao..
Nimekumbuka kipindi cha ripoti cha ITV mwaka jana...
Hapo ulipo kaa kwenye hiyo siti tayari wewe ni bilionea, ule mlango uliopitia ushakuwa bilionea.
 
Nilitamani sana umalizie simulizi alizokueleza huyo mdada na namna ulivyomuokoa kupigwa.
Katika simulizi yake; yeye ni graduate na hana kazi, sasa katika pilika pilika za kutafuta job akaambiwa na baba yake ambaye ni msataafu kuwa kuna kijana wa mzee fulani anayefahamiana naye toka kijiji X kwa sasa kafanikiwa huko jijini Mwanza kimaisha baada ya kuajiriwa kwenye kampuni fulani inayodili na biashara ya online marketing.

Pia kijana huyo alimwahidi baba yake kuwa atamuunganisha binti yake aajiriwe halipo yeye, kikubwa huyo baba (mstaafu anajulikana siku zote pensheni inasoma) awe tiyari kuchangia bidhaa zao za virutubisho kwani nje na kumtibia BP pia itamwongezea (bintiye) sifa za ziada kwa mabosi wake kumkubalia kirahisi kuungana nao kwenye biashara hiyo, bila hiyana mzee wa watu kwa ajili ya bintiye kupata kazi akaona isiwe tabu akakubali kupigwa kwa kununua kwanza bidhaa hizo za virutubisho (kwa Tsh.200,000)na akasafirishiwa kwa njia ya basi hadi huko kijijini kwao.

Baada ya hapo ni zoezi la kuja mjini ambapo mzee akahakikishiwa kuwa binti yake aje tu kwanza na kiasi cha shilingi 30,000 ambazo ni kwa ajili ya kitambulisho na kujiandikisha, ila asiofie pakufikia mwanaye kwani huko kazini wanahosteli nzuri na salama kwa ajili ya kufikia wafanyakazi wao waliotoka mbali, mpaka pale watakapozoea mazingira ya kazi wanaeza enda kupanga kikubwa aje na pesa ya kula tu (kwa kuwa kijana anahaminika kwa wazee na pale kijijini ni mtu mwenye heshima yake mzee akamruhusu binti achangamkie fursa)

Binti anaeleza kuwa mojawapo ya kitu kilichomvutia kuhusu kazi husika ni pamoja na kuambiwa kuwa atafanya kazi katika kampuni nzuri, yenye ofisi kubwa na makompyuta ya kutosha kinachotakiwa ni yeye tu kuja kuripoti na kuelekezwa mara moja namna ya kuuza bidhaa mtandaoni kisha aanze kuvuta mshahara wa bila jasho kwa kuwa wao hawatembezi bidhaa juani kama machinga, wao shughuli zao zote huishia mtandaoni na unalipwa vizuri kila sekunde unapofanya mihamala hawasubiri tu hadi mwisho wa mwezi (japo mshahara mwisho wa mwezi pia upo palepale)

Sasa binti anakwambia kuwa alikuwa akiwasiliana na huyo tapeli X kwa njia ya simu tokea ameondoka kwao mpaka anafika stendi ya mabasi Nyamhongolo kila mara alikuwa anapewa maelekezo ya namna ya kufanya, sasa siku ile anakuja kwa bahati mbaya gari alilopanda (binti) lilipata hitilafu likaharibikia njiani hivyo akafika Mwanza mida ya jioni kabisa, alivyowasiliana na tapeli X akamwambia kama vipi tafuta lodge yeyote iliyokaribu nawe ulale mpaka kesho ndiyo uje ofisini kwa maana sisi shughuli zetu mwisho saa 9:30 mchana hivyo hatuna namna ya kukusaidia.

Binti japo Mwanza hapajui ila alikuwa akipita maramoja moja akielekea huko chuoni kwao Morogoro kuna mtaa alikuwa ana-idea nao (Igoma) hivyo akaendazake kutafuta malazi hapo hadi kesho yake ambapo ndipo siku nilipokutana nae akiwa anaelekea kwa wazee wa kazi kupigwa....

"Tunaendelea sasa na pale tulipoishia...baada ya kugundua ni mgeni na kisha kunieleza vile kuwa kuna kampuni hapo mitaa ya CCM Kirumba sijuhi ameitishiwa kazi mara imepanda mara imeshuka mmh! nikawa na mashaka ndipo ikabidi nianze kumdodosa kiundani kuhusiana na kampuni husika.

Kumhoji dada wa watu kwani Kampuni yenyewe inaitwaje? Akaniambia hata na yeye hajui bado maana kila alipojaribu kumhoji jamaa ni kama alikuwa anamumunya maneno na hasikiki vizuri, kama utani nikamwambia wasije kuwa ni matapeli hao! Dada wa watu akashtuka ila kwa ujasiri akanijibu haiwezekani yule kaka hawezi kufanya hivyo tunaheshimiana sana, nikamuuliza kwani ndiye huyo muda wote mlikuwa mkizungumza nae, akanijibu hapana huyu ni mwingine kaniambia anaitwa X naye anafanya kazi kampuni hiyohiyo kapewa namba zangu na yule mtu aitwaye X hili aje anipokee, sasa ndiye mara kwa mara nawasiliana nae (hapa kwa uzoefu tu nikawa nishausoma mchezo unaoendelea siyo mzuri wenda kuna shida mahali)

Hapo hapo nikauvaa moyo wa huruma nakadhamira kale ka kusaidia jambo lisilonihusu ikawa inaniijia akilini ila najaribu kuyashinda majaribu, hatimaye tukafika Natta japo sikuwa na mpango wa kushuka ila nikajikuta nashukia pale kumsaidia binti wa watu na kazini nikapiga simu ya hudhuru ya kuchelewa kidogo (sijui kwa kuwa ni mrembo ndiyo maana
najikuta mwana wa Zebedayo[emoji23])

Nikamsindikiza mpaka stendi ya daladala ya makoroboi, palepale akapigiwa simu kuulizwa alipo (nikamwambia ajibu vipi) hapohapo jamaa akatuma meseji kuwa kuanzia hapo wawasiliane kwa meseji kwani yupo ofisini, basi tokea hapo chating zikawa ni zile za namna ile nilishazizungumzia mwanzoni hatimaye tukafika kituo cha daladala cha misheni jirani na rock city mall mahali tuliposhukia,

Wakati tunatembea kuitafuta furahisha kwa mujibu wa maelekezo ya tapeli nambari mbili, ikanibidi nitafute jambo la kupotezea ka muda hili nimchane binti hatari inayomkabili na nimpange cha kufanya kwa kuwa muda sasa ni karibia saa nne asubuhi najua tumbo linadai nikampitisha mgahawa mmoja jirani na hapo uwanja wa furahisha kupata kifungua kinywa (ambao ulikuwa hauna wateja wengi nyakati hizo) nikamfungukia wasiwasi wangu wote kuhusiana na kampuni hiyo X ninayohisi ni ya kitapeli na nikampanga cha kwenda kufanya akifika huko (mwanzoni alionesha kutoniamini kabisa tena kuna kale kamtizamo ka dharau fulani hivi machoni mtu akiwa anakueleza jambo usilokubaliana nalo alikuwa nako, ila akazidi kunihakikishia kuwa anajua hamna shida anaamini hizo ni hisia zangu tu ila hamna inshu)

Baada ya chai mie nikampa assignment ya kuniripotia kila kinachoendelea kwa SMS na aende ila asitoe pesa wala chochote kile hata begi lake ikitokea ameombwa lipelekwe mahali popote pale asikubali, nikamwacha mie nikaenda zangu kazini,

Sasa yaliyoendelea huko seminani ndiyo hayo nilishayaelezea yote, baada ya kutoka job ikabidi nimpitie binti wa watu hapo VILLA PARK (mahali walikokita kambi-matapeli) nikampeleka kwenye restaurant za jirani kula huku ananisimulia kila kilichojiri tokea tumeachana mpaka muda huo, nikamwambia sasa si unaona nilichokueleza tokea mwanzo,

Palepale binti bila kujizuia akaanza kuangua kilio akifikiria alivyodanganywa na uhalisia ulivyo, pili akinishukuru kwa wema niliomwonesha, kama gentleman nikajiongeza na leso mkononi hili binti afute machozi huku nikimfariji kwa kuishinda mitihani ya utapeli na punde mipango ya kurejea alikotoka ikafanyika nami sikuwa na la ziada tena katika simulizi hii nikawa sina budi kuishusha kalamu yangu chini kufikia hitimisho.
 
Aloo.. Chuo hiyo nikauza products zao.. Wala haziuziki.[emoji1787][emoji1787]
Tena kidogo niliambiwa nauza bangi.
Badae nkaona sokapohapa mwaisa [emoji1787][emoji1787][emoji1787] maisha ni kuchagua na nimechagua kwenda mbele sirudi tena nyuma.
Anyway nilijifunza na siwezi rudia makosa ya kiufundi kama hayo.

Nikisangatiti unaweza ukatamani utupe mzigo wote ila ukifikiria kwa umakini dhamira inakusuta kuwa mzigo wenyewe ndiyo hela yako uliyopoteza, unaweza tamani kulia ila machozi hayatoki mwishowe unaamua kufa kiume.. kutenda kosa siyo kosa la muhimu ulijifunza[emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
  • Thanks
Reactions: apk
Mkuu unachosema ni kweli. Hawa jamaa wa Alliance ni WEZI wa kutupwa! Kuna siku walitukusanya kwenye jengo moja kali la ghorofa wakawa wanatupa "semina" ya utajirisho kupitia motivational speakers matapeli wa kukodi kutoka Dar, nikawashtukia mapema nikasepa.

Halafu wao kila wakati wanapoongelea MAFAIKIO wanaonyesha picha za magari ya kifahari. Hawahubiri mafanikio mengine zaidi ya magari. Lakini kuna motivational speaker mmoja alijichanganya akasema mojawapo ya zile picha za magari aliyokuwa anatuonesha zilikuwa photoshoped. Yaani baada ya kusikia hilo nikakata tamaa kabisa.

Bahati nzuri kwa sasa katika mkoa huu tayari wamesitisha operations zao baada ya watu kuwashtukia na wale waliokuwa wamejiunga nao tangu mwanzo wamewakimbia baada ya kuwagundua kuwa ni matapeli wa kutupwa.

Ndugu zangu mliomo Alliance na ambao mnafikiria kujiunga, nawashauri muachane na matapeli hawa. Watawafilisi muda si mrefu aisee!
Asante mkuu, kwa kuwa shuhuda wa haya matukio ya hawa matapeli wengine wakiona tunazungumza humu wanadhania haya mambo ni mzaha au upuuzi ambao haupo mpaka pale yatakapowakumba wao au jamaa zao.
 
Back
Top Bottom