ALLIANCE GLOBAL: Kampuni ya kitapeli inayoendelea kuliza wasomi wengi nchini

Scars nakufuatilia endelea.
Hawajibu maswali wale

Walichoniambia ni kuwa hilo swali atakujibu aliyekuleta.

Nikawaambia atanijibuje huyu wakati yeye bado sio mnufaika wa hii biashara kama nyinyi.

Hamuoni kama naye huyu yupo hapa kujifunza na moja ya sababu za kumfanya atoe hela ni pale anapokuwa hana mashaka na hii biashara.

Na mashaka yetu yanahitaji majibu mazuri kutoka kwenu ili yaweze kuondoka.

Hawakujibu kitu wakanisisitiza nije semina ya pili nitapatiwa majibu nikaamua kuwapotezea.
 
Yaani hadi inatia hasira, kwanini vijana wa siku hizi hatuna ufuatiliaji wa mambo, unaambiwa kuhusiana na Kampuni usiyoifahamu vyema kama msomi na mkononi una simu janja kazi kufuatilia stori za mwijaku na baba levo, unashindwa kuingia Google uandike Alliance Global utapeli uone kama utapata walahu dondoo kuhusu experience za users i.e kwenye Google kuna makala ya gazeti la Mwananchi kuhusiana na utapeli wa Alliance Global huko Kilimanjaro n.k, Umeshindwa huko basi pitia Jamii Forums, Haya tuseme facebook ingia search andika Alliance Global moja kwa moja itakuijia video ya makala ya Ripoti Maalum kutoka ITV..June 15, 2022 kuhusiana na matukio ya hawa matapeli n.k
 
Mkuu waache waliwe tu. Kila siku wanaambiwa Ponzi Schemes ni biashara za kihuni hawasikii.
Ukibahatika kufika mle ndani zinapoendeshwa shughuli hizi na ukiwa na ufahamu juu ya hawa mbweha utatamani kulia kuona umati wote ule wa vijana wenye matumaini na kesho yao, waliosafirishwa mbali na makwao wapo pale kutafuta kisichokuepo badala yake wanaandaliwa kutapeliwa, fikra inaweza ikakuambia simama paza sauti uwaambie tokeni nje hapo mnaibiwa au uwatandike makofi uwazindue usingizini but wahenga walishasema sikio la kufa...
 
Hawawezi kuwa na majibu yeyote yale kwa mtu anayefikiria kwa kina kwa kuwa mara nyingi vijana hawa huwa wanapikwa na kukaririshwa wanachopaswa kuongea, majority wanaupeo mdogo na wanaowaseminisha nao ujifanya kondoo kwa kuiga tabia ya unadhifu na ustaarabu walioukuta mahali pale, hivyo kuna ile kasumba ya nitaonekaje nikiuliza swali ambalo si la kitaalamu? Au pengine kupitia kuuliza swali la namna hii, vipi nikiikosa hii nafasi na gharama zote ambazo nimekwisha tumia? Hivyo unakaa kimya huku masomo yakiendelea kukoza mwisho wa siku unajikuta umekuwa zombi uambiwi wala husikii juu ya kuachana na hao watu yaani ni addiction mbaya kuliko uumini kwa pasta Makenzie wa Shakahola au mfalme Zumaridi.
 
Goodmorning bilionear, hata iwe saa mbili usiku salam yao ni hiyo tu.
Your next bilionear, unaambiwa ni bilionea mtarajiwa wakati hata kula yako ni shida.
Duka mtandao..
Nimekumbuka kipindi cha ripoti cha ITV mwaka jana...
[emoji23]yaani wana-upuuzi mwingi wa kudanganya wafuasi wao na maneno matamu matamu ya kwenye vitabu vya motivation, utafunzwa kuhusu Power of Mind ya kuwa utajiri uanzia katika fikra zako yaani ukiamini ni tajiri basi wewe tiyari ni tajiri hivyo ukiitwa bilionea unajiona kama tiyari una hisa DP World, wakati huo kumbe wewe ndiye bandari yenyewe[emoji125][emoji125][emoji125][emoji1787]
 
Nimecheka aisee khaaa uwiii
 
Kwa vijana hawa wanaoshinda Instagram kuwafatilia kina mwijaku na mwenzake baba levo na wengine wapo busy kujua maisha ya kajala na mwanae yapoje? hata sishangai kwanini wamekuwa mandezi wakutapeliwa kijinga hivyo.
 
Ilikuwaje tena huko
Baada ya sakata la Bandari kuna vijana wetu pia wanaelekea kusaini mkataba na Alliance Global ambao hauna win-win situation yaani unamlipa mwajiri mshahara wa 600k na 30k (sitting allowance) na gharama zilizobaki ni juu yako hata ukifa na njaa yeye hausiki, hili akupe bidhaa zake ambazo yeye binafsi kashindwa kuziuza ili ukamuuzie pia hapo hapo umletee na wafanyakazi wengine wawili au watano hili aangalie uwezekano wa kukulipa na kaposho kidogo, kwa kweli hili halikubaliki tusimame tuwapambanie waathiriwa.
 
Hao jamaa sijui ndo walikiwa DERM. PLAZA hapa MAKUMBUSHO kama mwezi hivi mana nilikuwa naona pilika za vijana sana kwenye LIFT mpk lift inazidiwa ujazo
Nikahisi tu kutakuwa na SEMINA floor ya 10 sijui 12 huko
Nikawaacha tu vijana na SEMINA zao nikawa busy na mambo yangu ila nilijua tu SEMINA dizaini hizo
 
Kwa vijana hawa wanaoshinda Instagram kuwafatilia kina mwijaku na mwenzake baba levo na wengine wapo busy kujua maisha ya kajala na mwanae yapoje? hata sishangai kwanini wamekuwa mandezi wakutapeliwa kijinga hivyo.
Hawa Alliance Global walishaona vijana kwao ndicho kichochoro cha kujipatia kipato bila jasho, tena kwa hiki kizazi cha mtandao na mambo ya kipuuzi yaani nikukung'utwa tu mihela kila mwaka na watu hawakomi kuwapelekea, na wanaopigwa matukio nao hawasemi wanakaa kimya hili wengine nao waingizwe mkenge.
 
Ndiyo wenyewe hao wazee wa location, ukodi sehemu fulani amazing na maandalizi ya shughuli zao wakiamua si haba, pale parking wanakuwa wamepachafua kwa ndinga za kuazima na suti zao nyeusi utadhani waombolezaji, lengo ni kunasa windo lao ambalo ni vijana na wanaopenda kuegeshea life au wepesi wa kushawishiwa.
 
Wale mambwa ni matapeli
 
Wamejaa madem wa kaskazini na Singida
Kuna mmoja alinletea issue za izo global nikamkaza na mambo ya global akaacha kuniambia

Mmenikumbusha nijarbu kutafuta handle yake upya npashe kiporo namba zake za simu nlipoteza
kiufupi ukatibu tatizo kwa tatizo...[emoji23]au tuseme ukaona fursa kwa mleta fursa na ukaitumia fursa bara'bara na kuikosesha kampuni mapato..[emoji125][emoji125] huwa wanawatumia wanawake warembo kwenye michezo yao hiyo ya kamari kukuingiza chaka kama ilivyo tu kwenye mikopo humiza[emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Goodmorning billionare, kuna dada namwona ktk status anauza hizobdawa huwa namzoom tu nilikuwa nataka kumtongoza nikagairi

Good morning billionaire, unakwama wapi? We mtokee tu lakini mistari sidhani kama itafanya kazi cha msingi nunua tu dawa zake na huwe tiyari kuunganishwa kwenye mfumo, nyapu utapewa kama zawadi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…