ALLIANCE GLOBAL: Kampuni ya kitapeli inayoendelea kuliza wasomi wengi nchini

Dah! Mkuu ahsante sana kwa simulizi yenye kufundisha.

Mara nyingi utapeli unaonasa na kukumata ni ule utapeli unaounganishwa kwa kupitia jamaa yako wa karibu ama ndugu ili kukutoa wasiwasi wa kupeleka shingo kibra!

Na mtu akiisha ingia kwenye target ya kupigwa huwaga ni vigumu sana kumnasua kutokana na namna ambavyo matapeli wanajua sana namna ya kuinterrupt saikolojia ya mhanga.
 
Ni kweli kabisa mkuu, mtu akishakuwahi akakuteka akili na kuiharibu saikolojia yako kujinasua ni mbinde mno, uwezi amini kuna ng'ombe iko busy sasa hivi na mafundisho ya Alliance global licha ya kusoma uzi huu lakini inaingia kibla na haitaki kukubaliana na ukweli kuwa inachokifanya si sahihi.
 
Huwa wanasikia basi?wanaona kama unawazibia riziki,kuna kakijana ka huko singida basi kalifika mjini mwanza sasa kutokana na kalivyonichukulia kama dada yake basi nikakauliza kamekuja kufanya nini mjini ndo kaanza kunielezea nikajua ni wale wa ajira!ajira nikakaelekeza vizuri,nikaona hakajaridhika sa ngapi hakajapigwa na kitu kizito mpaka nilikaonea huruma nikakakatia tiketi karudi kwao

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Bora hata sasa hivi kiasi imepungua,anko na kijana wake walipigwa 5M,binamu alikuwa chuo ghafla nikaanza kuona status akipost mambo,mara quotes za matajiri mara gari za ndoto zake,badae nikaona hapost tena kumbe ashapigwa na kitu kizito

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 

Hii generation inakabiliwa na mitihani migumu sana, vijana wanaumizwa mno na hawa matapeli na elimu hii kwa jamii haitolewi kwa mapana yake nadhani kwa kuwa vyombo husika na vile vya kusimamia haki navyo itakuwa kuna namna wananufaika katika mnyororo huu wa dhuluma lasivyo vitendo kama hivi visingeachwa viendelee katika jamii zetu pasipo kukemewa wala kukomeshwa.
 
Dah inauzunisha sana 5M huo ni mtaji ambao ungemtoa kabisa kimasomaso, ila kwa ujinga wake akaenda kuwakabidhi matapeli na yeye kurudia msemo wa ng'ombe wa maskini.
 
Hata hawa wazee wa Forever Living.
Ni hayo hayo, wazee wa pyramid schemes unafanya kazi kwa kushirikishwa nawe unashirikisha wengine, kisha unamuuzia mtu bidhaa zake kwa kuforce market, unapambana vilivyo ku-push mzigo uende hata kama soko ni gumu kiasi gani huko radhi hata kumdhulumu mteja kwa bei isiyo halali, mwisho unachoambulia ni kiduchu ukilinganisha na efforts pamoja na fedha ulizowekeza, kama ni mjanja na una-wish kufanya wanachofanya basi jifunze kuhusu mfumo wao unavyofanya kazi nawe anzisha wakwako otherwise achana na hizi mambo zimejaa utapeli na ubabaishaji mno.
 
huu ujinga niliukataa sana licha ya kuwa na marafiki wa karibu waliojiunga baadae walilia vilio vya mbwa mwizi
 
Dah inauzunisha sana 5M huo ni mtaji ambao ungemtoa kabisa kimasomaso, ila kwa ujinga wake akaenda kuwakabidhi matapeli na yeye kurudia msemo wa ng'ombe wa maskini.
Nadhani hawatosahau mpaka wanaenda kaburini,make anko aliugua pressure 5M ya kijijini sio mchezo

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani hawatosahau mpaka wanaenda kaburini,make anko aliugua pressure 5M ya kijijini sio mchezo

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Dah pole yake maisha haya sometimes yana ukatili mno, imagine umetendewa hivyo afu unakutana na washenzi hao hao mahali pengine kwenye miangaiko yako eti bado wanaendelea na dhuluma za kuwapotosha wengine waingie mkenge na uruhusiwi kuwaghasi kisa wapo kisheria.
 
huu ujinga niliukataa sana licha ya kuwa na marafiki wa karibu waliojiunga baadae walilia vilio vya mbwa mwizi
Utapeli ni laana kubwa mno maana licha ya kunufaika na jasho la mtu visivyo halali moyoni unajibebea msalaba wa manung'uniko, simanzi na majonzi ya wale unaowatapeli. Kimwili unaonekana ni tajiri lakini kiroho umedhoofu na wala amani haipo nafsini mwako, kwani matendo yako maovu uendelea kukuwinda milele.
 
ni kweli kabisa mkuu, nna classmate wa chuoni hadi leo hii anateseka na haya maaliance sijui karogewa
 
ni kweli kabisa mkuu, nna classmate wa chuoni hadi leo hii anateseka na haya maaliance sijui karogewa
Kuna tapeli mmoja nilikuwa nabonga nae pasipo yeye kutambua kama namchora, akanitonya kuwa wakati wa Magufuli hizi mambo zilipigwa stop ila awamu ya Mama ndiyo inaupiga mwingi, chakujiuliza je serikali hii inauchungu na affair za wananchi wake hasa vijana?

Kwa maana kampuni za namna hii hivi sasa zimeenea nchi nzima na zinakusanya pesa za walalahoi kama njugu na zinapotosha vijana wadogo wadogo waliomaliza form four mpaka ngazi za juu za elimu kwa kuwakamua wazazi masikini pesa kwa njia ya ulaghai na serikali yao ikibariki suala hili, pesa ambazo zingetumika kuwaendeleza vijana hawa kujiajiri, kiujuzi au kibiashara.
 
Ni kama akina chenza, unapewa sabuni na mafuta utembeze mitaani kama mchuuzi! Ukileta mtu unapewa commision huku ukiwa na matumaini ya kufika level za meneja [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni kama akina chenza, unapewa sabuni na mafuta utembeze mitaani kama mchuuzi! Ukileta mtu unapewa commision huku ukiwa na matumaini ya kufika level za meneja [emoji23][emoji23][emoji23]

[emoji23]bora hii mtaji ni nguvu zako mwenyewe utachagua unyoe au usuke kuliko hawa akina forever unapigwa panga hata kabla ya kuanza hustle yenyewe[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nyuzi kama hzi za kuwatahadharisha kuhusu utapeli ni nyingi sana sema watu nikama wamelogwa ivi wanekuwa vichwa vigumu kuelewa .....huwezi amini pamoja na ushauri wote huu utakuta kuna punguani mwingine atajichanganya aka tapeliwe na kuja hapa kulia lia ..... kwenye haya maisha hakuna shortcut kwenye mafanikio utapigwa kama ngoma na usomi wako na kugeuzwa fursa
 
Mwendelezo tafadhali [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…