Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amesema kuwa Abdulrahman Kinana ambaye jina lake limependelezwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mtu mwenye uwezo mkubwa na kuwataka kuachana na mambo ya nyuma.
Kauli yake hii inakuja kutokanana na swali aliloulizwa na wanahabari nje ya ya ukumbi wa Jakaya kikwete unakofanyika mkutano mkuu wa CCM jijini Dodoma ambapo amesema kuwa mambo yaliyopita hayana msingi kwa sasa.
"Hakuna ubishi juu ya uwezo wa Mzee Kinana" ameeleza Hapi
Hapi ameeleza kuwa Kinana ni mtu mwenye uwezo, maarifa na uzoefu mkubwa kwenye siasa na ni mwalimu kwa watu wengi kwenye chama hicho.
"Kama vijana ambao tunaendelea kujifunza kwenye siasa za chama mambo ya nyuma nadhani hayana msingi kwa sasa hivi" aliongeza
Kama hujui siasa ni nini unaweza mlaumu Ally Happy kwa maneno yake haya.
Ila kwa kuwa siasa ni uwezo wa kubadilika badilika kama kinyonga kulingana na mazingira, wakati, na mtu aliye juu yako kijana Happy yuko sahihi kabisa ikizingatiwa kuwa ipo siku atautaka ubunge wakati huu wa mwenyekiti mpya mbali na uhakika wa kuendelea kuwapo katika nafasi ya uRC anayoshikilia hivi sasa.
Kama hujui siasa ni nini unaweza mlaumu Ally Happy kwa maneno yake haya. Ila kwa kuwa siasa ni uwezo wa kubadilika badilika kama kinyonga kulingana na mazingira, wakati, na mtu aliye juu yako kijana Happy yuko sahihi kabisa ikizingatiwa kuwa ipo siku atautaka ubunge wakati huu wa mwenyekiti mpya mbali na uhakika wa kuendelea kuwapo katika nafasi ya uRC anayoshikilia hivi sasa.
Watu walitaka Hapi aendeleze msimamo uleule ili amwagwe,cjui ada za watoto wake watamsaidia kulipa,kuwa na msimamo sio jambo rahisi kama washabiki wa siasa wanavyopenda.Hata Mbowe na misimamo yake kwenye swala la kumkaribisha Lowasa alikula matapishi yake mwenyewe.