Akiwa mkoani Iringa, Ali Hapi alimjibu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kufuatia kauli yake ya kuwa Rais Samia hana haki ya kutoa maamuzi ya kinachoendelea bara kwa kuwa yeye ni Mzanzibar.
Hapi alidokeza kwamba kwa kuwa mchakato wa kuhalalisha mfumo wa vyama vingi pamoja na mapinduzi ya kiuchumi yaani Ubepari yaliletwa na Rais Mwinyi ambaye ni Mzanzibar, je CHADEMA haina haki ya kuwepo kwa sababu aliyeleta mapinduzi ni Mzanzibar.
Aidha Hapi alihoji pia kuhusu ubadhirifu na mgogoro unaoendelea ndani ya chama cha CHADEMA ambapo alidokeza kuwa iwapo chama hicho kimeshindwa kujiendesha kwa amani ndani, je kitaweza kuongoza nchi?
Your browser is not able to display this video.
My Take
Tuhitimishe au tuendelee kuwasubiri wengine?
Huyo Happy Arudi kwanza Darasani afundishwe namna ya kutafsiri mambo ya kisheria bila kutaja mifano isiyo lingana na hoja mezani, vinginevyo ni aibu kwa waalimu wake wa sheria
Huyu naye IQ ndogo sana, badala ya kujibu hoja za msingi za umiliki ardhi zanzibar kwa wabara au mgawanyo wa majimbo ulivyo unfair bara na visiwani anakimbilia kuongelea watu kuvaa ngozi!! irrelevant reply.