Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break, Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima

Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break, Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima

BAADA YA KUDHIHAKIWA NA ALIKAMWE, JUMA MGUNDA AMPA JIBU

🗣️"Yanga ni Club yetu pekee Tanzania inayotuwakilisha kwenye fainaly hii ya CAF na kwa bahati iliyonjema inacheza na Club Inayotoka nje ya nchi yetu.

🗣️Sijui kinachopelekea mimi kuwa miongoni mwa kampeni hii ya matusi na kunidhalilisha Nilidhani kampeni itakuwa ni kushinda fainally, kuliko hiki alichokifanya Mwanangu Ally Kamwe.

🗣️Namuombea kwa Mungu awe na mwisho mzuri, mimi nimeshuhudia watu wengi wakifanya kazi Yanga na Simba na sasa wapo nje ya mfumo.

🗣️Kama nilipaswa kutukanwa ili Yanga ishinde basi nimekubali ili Taifa langu lijivunie .

🗣️Tusiposhinda kesho nitashangaa sana kwanini tumefungwa wakati kilichotakiwa kifanywe kimefanywa juu yangu na familia yangu" Kocha Juma Mgunda.

Akiwa ktk kampeni za mechi ya tarehe 28/05/2023 huko Zakhiem Mbagala aliwauliza mashaabiki kati ya "Mgunda na andazi" utachagua nini. Mashaabiki wakaitikia "andazi" . Hakutosheka akauliza tena"kati ya wasimamizi wa Feisal na andazi utachagua nini. Mashaabiki tena wakajibu "andazi".

Sasa mimi kama mtu mzima naona Ally Kamwe alichofanya ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa malezi na makuzi ya wazazi wake. Huwezi kumlinganisha mtu mzima mwenye umri sawa na baba yako na "andazi".

Mgunda amekuwa Hana utani wa Simba na Yanga hata ktk media sjawahi kumskia akitoa maneno ya shobo kwa Wana Yanga. Iweje leo mbele ya watu tena wa rika tofauti tofauti umlinganishe na andazi.

Haya sasa kakujibu kiutu uzima kama baba. Kazi kwako.

Mimi siyo mshabiki wa mipira, lakini kwa hili, huyu Ally aliyemkosea mzee heshima, akaanguke miguuni pa mzee Mgunda na kumuomba msamaha. Kukosea kupo, na ndiyo maana hata Mwenyezi Mungu anakubali toba ya kweli. Maana sisi sote hujikwaa na kukwazana mmoja na mwenzake.
 
Huyu mpumbavu kweli, Mgunda kaingiaje hapo na wala mechi haimhusu!!?

Sio kuomba radhi mtandaoni tu amfate kabla ya mechi la sivyo laaa siivyo , Yanga akipigwa huyo dogo atafurushwa, mashabiki watasema ni laana ya Mgunda kwake, wabongo hawana dogo.
 
Mimi siyo mshabiki wa mipira, lakini kwa hili, huyu Ally aliyemkosea mzee heshima, akaanguke miguuni pa mzee Mgunda na kumuomba msamaha. Kukosea kupo, na ndiyo maana hata Mwenyezi Mungu anakubali toba ya kweli. Maana sisi sote hujikwaa na kukwazana mmoja na mwenzake.
Utani mbaya utani mwingine unachoma mtu hana hata kikombe Cha kahawa unaenda kumfananisha na ANDAZI 😆
 
Wewe na huyo Ally akili zenu ziko sawa. Siyo kosa lako. Unaona tunakemea alichokifanya. Wewe unatuweka fungu moja.
🤣 Mgunda = Simba v Andazi, Mimi kusema ukweli sitaki kua mnafki nachagua ANDAZI nipo upande wa Andazi
 
Vitu vingine ni vya kawaida na watu kutaka kukuza Jambo tu....!, Kipindi manara yupo Simba alivyosema yanga wenye akili ni 2 Kuna aliyemwona kakosea?.
Ahmad Ally majuzi Kati alitamka watu wa Yanga ni sawa na MAITI Kuna aliyemnyooshea kidole?, Utamaduni huu wa kipuuzi umeasisiwa na watu wa Simba. BTW kwani mbona aliyesema Andazi ni bora kuliko CCM hajaonekana kuwa na dharau kwa CCM na Rais wa Nchi?.
Mkuu sisiem ni mtu? Au yanga ni mtu? Hapa nafikiri kinachozungumzwa ni kumshambulia Mgunda personally badala ya kuushambulia mpira ama mashabiki wa mpira wa upande wa pili kama angetaka. Kwa hili la kumfananisha Mgunda na Andazi, hata GSM hawezi kuwa na wewe. Omba radhi hadhani ili usamehewe.
 
Sema hujamwelewa Ally Kamwe ndio maana Mimi ni shabiki wa Yanga Ila pia ni Shabiki wa Ally Kamwe jamaa hakumaanisha mlivyochukulia nyinyi vichwa vidogo yeye kawaambia Mgunda akimaanisha Simba Ila kafunga semi kwani mgunda anafundisha team gani na hio team imeambulia Nini msimu huu ukipewa andazi na ukipewa Simba unachagua nini ? ANDAZI
Andazi wewe yaani mtu katajwa kwa jina unasema kataja timu. Hilo ni shambulio binafsi, acha ushabiki wa kishamba wewe.
 
Kwa navyozijua hizi Club, hilo sidhani kama litawezekana.

Zima Ego ya kujiona wao ndio the best hususani pale ambapo muathirika hana nguvu yeyote serikalini
Hawajui hesabu ya + na -,wanafanya business kimazoea. Biashara yao kwa hatua waliopoo siyo ya kujibizana wala kuwashambulia watani zao.
Labda km kweli wenye akili ni wawili tu (inasemekana aliwahi kuzungumza hivi Manara)
 
Sema hujamwelewa Ally Kamwe ndio maana Mimi ni shabiki wa Yanga Ila pia ni Shabiki wa Ally Kamwe jamaa hakumaanisha mlivyochukulia nyinyi vichwa vidogo yeye kawaambia Mgunda akimaanisha Simba Ila kafunga semi kwani mgunda anafundisha team gani na hio team imeambulia Nini msimu huu ukipewa andazi na ukipewa Simba unachagua nini ? ANDAZI
Asingesema wakati huu hata km ulikuwa ni utani.
Hiyo ni personal attack ndiyo maana wengi hatujapenda.
Nadhani hata boss wake hajafurahishwa na huo utoto aliofanya.
 
Hivi hiki cheo cha usemaji majukumu yake ni nini hasa!!!....maana naona huwa wanaongea upuuzi tu ambao hauna tija yoyote kwa soka letu...na kweli watu wengi sana wamepita simba na yanga kuna maisha nje ya hapo
 
Mabwabwa ya simba mmepata pa kujifichia.... 😅🤣 Msimu huu kazi yenu ni kushika ukuta tu mtoleww marinda hamna cha maana
 
Itamuumiza Sana hata kwenye huu mchezo akili yake haitakuwa sawa

Nadhani katajifunza maneno ya kuongea kwenye hadhira ya watu wengi usione wanaokushangilia ukaongea chochote

Haka kabwana kalishajiachia Sana kapo hewani kanaviutani vya kitoto na vya kiswahili na kuita watu SHEHE uutadhani mashabiki na wapenzi wa timu hiyo ni waimani Moja. Kajifunze kuongea na hadhira mchanganyiko watoto , wanawake, wanaume, wasomi, wasiosoma, maskini, matajiri, wazee, wakristu, waislamu, wapagani na wote wakuelewe bila kukwaza mtu au kumdhihaki katika maongezi yako
 
Back
Top Bottom