Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break, Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima


Mimi siyo mshabiki wa mipira, lakini kwa hili, huyu Ally aliyemkosea mzee heshima, akaanguke miguuni pa mzee Mgunda na kumuomba msamaha. Kukosea kupo, na ndiyo maana hata Mwenyezi Mungu anakubali toba ya kweli. Maana sisi sote hujikwaa na kukwazana mmoja na mwenzake.
 
Huyu mpumbavu kweli, Mgunda kaingiaje hapo na wala mechi haimhusu!!?

Sio kuomba radhi mtandaoni tu amfate kabla ya mechi la sivyo laaa siivyo , Yanga akipigwa huyo dogo atafurushwa, mashabiki watasema ni laana ya Mgunda kwake, wabongo hawana dogo.
 
Utani mbaya utani mwingine unachoma mtu hana hata kikombe Cha kahawa unaenda kumfananisha na ANDAZI 😆
 
Wewe na huyo Ally akili zenu ziko sawa. Siyo kosa lako. Unaona tunakemea alichokifanya. Wewe unatuweka fungu moja.
🤣 Mgunda = Simba v Andazi, Mimi kusema ukweli sitaki kua mnafki nachagua ANDAZI nipo upande wa Andazi
 
Mkuu sisiem ni mtu? Au yanga ni mtu? Hapa nafikiri kinachozungumzwa ni kumshambulia Mgunda personally badala ya kuushambulia mpira ama mashabiki wa mpira wa upande wa pili kama angetaka. Kwa hili la kumfananisha Mgunda na Andazi, hata GSM hawezi kuwa na wewe. Omba radhi hadhani ili usamehewe.
 
Andazi wewe yaani mtu katajwa kwa jina unasema kataja timu. Hilo ni shambulio binafsi, acha ushabiki wa kishamba wewe.
 
Kwa navyozijua hizi Club, hilo sidhani kama litawezekana.

Zima Ego ya kujiona wao ndio the best hususani pale ambapo muathirika hana nguvu yeyote serikalini
Hawajui hesabu ya + na -,wanafanya business kimazoea. Biashara yao kwa hatua waliopoo siyo ya kujibizana wala kuwashambulia watani zao.
Labda km kweli wenye akili ni wawili tu (inasemekana aliwahi kuzungumza hivi Manara)
 
Asingesema wakati huu hata km ulikuwa ni utani.
Hiyo ni personal attack ndiyo maana wengi hatujapenda.
Nadhani hata boss wake hajafurahishwa na huo utoto aliofanya.
 
Hivi hiki cheo cha usemaji majukumu yake ni nini hasa!!!....maana naona huwa wanaongea upuuzi tu ambao hauna tija yoyote kwa soka letu...na kweli watu wengi sana wamepita simba na yanga kuna maisha nje ya hapo
 
Mabwabwa ya simba mmepata pa kujifichia.... 😅🤣 Msimu huu kazi yenu ni kushika ukuta tu mtoleww marinda hamna cha maana
 
Itamuumiza Sana hata kwenye huu mchezo akili yake haitakuwa sawa

Nadhani katajifunza maneno ya kuongea kwenye hadhira ya watu wengi usione wanaokushangilia ukaongea chochote

Haka kabwana kalishajiachia Sana kapo hewani kanaviutani vya kitoto na vya kiswahili na kuita watu SHEHE uutadhani mashabiki na wapenzi wa timu hiyo ni waimani Moja. Kajifunze kuongea na hadhira mchanganyiko watoto , wanawake, wanaume, wasomi, wasiosoma, maskini, matajiri, wazee, wakristu, waislamu, wapagani na wote wakuelewe bila kukwaza mtu au kumdhihaki katika maongezi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…