Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Hivi wewe unajikutaga nani kwenye hii forum?
Kudadadeki zako chagua mdole ✋
 
Hichi unachokifanya hapa si uungwana hata kidogo, acha kumdhalilisha Marehemu.

..Grow up....
Marehemu alimdhalilisha Mwenyezi Mungu, allikuwa mbaguzi kwa watu waziwazi, alijivika sifa ya uunga ati akasema katika watanzania zaidi ya mil 60 aliowauba Mwenyezi Mungu hakuona anayeweza kufanya afanyayo isipokuwa yeye tu. Hii kufuru zaidi ya dharau.

Aliitwa mungu, yesu n.k.

Haya tuseme yalikuwa ni uungwana, hayakuwa udhalilishaji kwa waja wanaomwabudu na kumsujudu Mungu wao kila uchao. Isipokuwa mrehemu mzalendo wenu JPM ndio watu wanakuwa sio waungwana na kuwa wadhalilishaji.

Mnachomwa dozi ya sindano za Kristapeni na kwinini ili mpone kifafa kisiwarudie tena.
 
Magufuli hayupo ila hakauki kwenye vinywa vyenu...jamaa kafa ila bado anaishi kwenye 'vinywa vyenu'.

Watu wazima wanapambana na aliyekwisha kuzikwa hata aibu hamna.

Badala ya kurekebisha alipokosea yeye, mnapambana na asiyekuwa hata na hayo madaraka tena

Endeleeni kumsema huenda mkapona majeraha yenu.

...Shame on you...
 
Kati yenu mnayemlalamikia mfu na mimi ninayewaambia mambo ya kubadili taasisi nani analialia?

Endeleeni hivi hivi, CCM watawatawala mpaka mfe na watoto zenu nao wakiendelea hivi watatawaliwa hivyo hivyo.

Mark my words.
Tusipangiane majukumu. Wewe shughulikia Katiba, sisi tuachie mtu wetu tuhangaike naye maana ameacha wajinga wengi sana.
 
Aisee Kweyunga. Umepiga upper cut mkuu.
Need we say more?
 
Binadamu wote ili mradi unaishi ni walking carcass, maana wote njia yetu ni kifo tunatofautiana zamu tu za kutangulia.......kiburi cha uzima kisikupofushe ukaongea kufuru.
Ni kweli binadamu wote tutakufa, lakini anapotangulia Dikteta aliyetaka kutawala milele ni sherehe kwetu.
 
Hichi unachokifanya hapa si uungwana hata kidogo, acha kumdhalilisha Marehemu.

..Grow up....
Yeye alipokuwa anatudhalilisha kwa miaka 5 yote ulichukua hatua gani? Alifuta mikutano ya vyama vya siasa, alibana uhuru wa maoni, aliiagiza Mahakama ziamue anavyotaka na akaliendesha bunge kwa remote.

Ni zamu yake tunapiga spana mpaka afe mara ya pili huko huko kaburini
 
Kazi ya kwanza nadhani ni kuwavua nguo watu mnaoshabikia ujinga wa viongozi wapuuzi wa katiba ya nchi na haki za binadamu.
Mbili, ni kuipigania katiba ya wananchi
 
Kwa hiyo mnalipa kisasi kwa aliyekwisha kuzikwa ?....itakuwa mna ugonjwa wa akili nyie.
 
Wapi amesema alikuwa sawa kufanya hayo???

Hivi nyie..kutokuwa sawa kwa magufuli ndiko kunakofanya watu waendelee kuwa wajinga kiasi hiki cha kuendelea kutukana marehemu??
Haya matusi yanasaidia nini sasa??
Mtu alishakufa!
Ni sawa na firauni anapolaaniwa kwa utawala fedhuli japo ashakufa
 
Ni sawa na firauni anapolaaniwa kwa utawala fedhuli japo ashakufa
Hizo laana zinatusaidia nini kama taifa??
Zinasaidia nini kwenye mfumuko wa bei??
Zinasaidia nini kwenye hali ngumu za maisha za watanzania?
 
Kweyunga unamwaga madini ya kutisha kuliko hata aliyeanzisha thread. Pamoja sana Mkuu, nimekukubali. Maana hata huyu Kiranga muumini wa Magufuli umekwishampoteza kwenye hoja zake zote
 
You must be stupid,frustrated,aggressive and a nincompoop to think in this way. Sorry!
 
Mmmh binadamu sisi!!
Hakuna hata ajuae sekunde moja ijayo atakuaje Bali MUNGU tu.

Tazameni sana yawatokayo yasijegeuka miiba kwenu.
Kuongea kufurahisha genge ila amini kila mnachosema kina impact.
Sijui mmekulia malezi gani,mmegeuka wasema ovyo,kurusha matusi ovyo hivi hamskii aibu?
Surely mnatukana Mtu aliyelala?
Nahisi hamjawahi fiwa,ila tu omba yasikukute.

Tuko safarini wote,mmegeuka Taifa la kutusi maiti!
Ninyi kiburi cha uzima kinawadanganya.
Wengi wenu ni vijana wadogo,na hamjui kitu mnachojitengenezea.
Anyway endeleeni......
 
Logic
Logic yako ni kutaka watu wenye kutofautiana kimtazamo waandamane ili iweje?

Watu huonesha hisia na misimamo yao kwa njia tofauti kwa jinsi walivyochagua.

Sasa binafsi si kuelewi kwa nini unataka watu watumie njia yako ya maandamano badala ya kwenye social platform.
Nini kinakuuma hapa?
 
Ni kweli binadamu wote tutakufa, lakini anapotangulia Dikteta aliyetaka kutawala milele ni sherehe kwetu.
Hawa waliopo kama hawana tamaa ya madaraka iweje wanakwepa mchakato wa katiba mpya.....
 
Vivo hivyo kwa Firauni ila bado tunamsema
 
Are you sure hatujawahi fiwa?
What about those Magufuli killed and others in bags at beaches?
Ninyi ndio mna machungu sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…