Hatuna shida na Magufuli lakini malofa wafuasi wa praise team ambao leo wanataka kuendeleza kasumba ile ile ya Mzalendo wao ya kufumba watu midomo. Pia Magufuli alikuwa kiongozi alivyoendesha tasisi ya urais ni jambo la kuendelea kujadiliwa hata kama hayupo. Kuna funzo endelevu kwa pande zake mbili za uzuri na ubaya bahati mbaya ni kuwa mabaya yake kijamii yananuka sana hadi kunajisi mazuri yake akiwa kwenye taasisi yetu hivyo wafuasi kujisikia vibaya inapotibukiwa hiyo harufu chafu.
Hakuna kosa wala haramu yoyote kumsema hata kama kafa, amekufa yeye sio taasisi yetu ya Urais aliyoiachia najisi, tukiusema unajisi huu ili usuguliwe na kufutwa kabisa na waliochangia najisi hii wachunguzwe msituzibe midomo kwa kisingizio cha kasha jifia. Wajibu haufi, wajibu unabaki kuishi milele.
Alitunyamazisha kwa mateka, risasi na kutuwekea tiss wa ovyo mitaani tusinongone, aki-record watu, akisambaza wasiojulikana, akipoteza watu, akihujumu bunge, chaguzi n.k. mkamuinua kama sanamu yenu akawa juu akajisahau mkamuaminisha atatawala milele kumbe mnamdamganya na kudanganyika, sasa hawezi na nyie hamuwezi tena kutupumbaza na kutanya mazezeta kama mlivyofanywa nyinyi, acheni tumsema kama mnaumia saaaana kwa mapenzi mlio nayo kwake anaposemwa basi "......nendeni Chato mkazikwe naye mkaa pamoja naye....." By ZZK.
Huko huko mnaweza kubadili hata katiba ili aendelee kuwaongoza maana huko hatutaweza kuwaingilia wala kuwasema.