Mkuu,
Hata mimi Magufuli sikumpenda, utawala wake sikuupenda.
Na bado naweza kuwa nuanced enough kuona habari za kumuita Magufuli "walking carcass" si tu hazina tija, bali pia zinaonesha frustrations. Ni kama habari za mtu ana hasira halafu hajui cha kufanya zaidi ya kuitukana maiti.
Hivyo, si kika anay3k3mea lugha hizi ni mfuasi wa Magufuli. Tuch3 hizi siasa simplistic za kukisa n8ance za kusema mtu akikemea ujinga wa lugha chafu dhidi ya Magufuki, basi ni mfuasi wa Magufuli.
Mimi naweza kuwa sijamkubali Magufuli na sikubali lugha chafu zisizo na tija dhidi yake, hususan sasa ambapo ameshafariki.
Ningewaona hawa watu wa maana sana kama wangejikita kuwa na katiba mpya itakayopunguza madaraka ya rais ili ujinga wa utawala wa Magufuli usijirudie.
Kumtukana mtu aliyekwishajifia zake hakusaidii kitu.
Zaidi, kunatupa maswali tu kwa nini huyu mtu anamtukana mtu ambaye hana influence mpya tena katika jamii?
Unataka kupigana na maiti ya Magufuli?